Ufahamu kuhusu MoU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufahamu kuhusu MoU

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Adm, Oct 21, 2012.

 1. A

  Adm Senior Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Habari wana jf,mimi ni mmojawapo kati ya wale ambao huwa tunasikia kuhusu MoU kitu ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele sana na ndugu zangu waislam. Hebu mwenye ufahamu na hiki atufahamishe kuwa MoU ni kitu gani hasa, kipo kwa sababu gani na kwa manufaa ya nani? Naomba kufahamishwa
   
 2. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  MoU ni kufupisho cha Maneno Memorandum of Understanding.

  Na Tafsiri ya haraka haraka ya Kiswahili ni Hati ya Makubaliano au pengine Waraka wa Makubaliano.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  MoU ipo sehemu zote si sector za kidini hata mkitaka kufanya bizness(cooperate) lazima kuwe na MoU-Yani Makubaliano yenu pande zote mbili....Haina uhusiano wowote na Dini
   
 4. A

  Adm Senior Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  inayopigiwa kelele na waislam wa tanzania inahusu nini
   
 5. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  MoU ni katika kutafuta Mutual benefit katika makubaliano fulani (more so) ya kibiashara yaani nani anatoa nini na nani anafaidika vipi ili kupata win-win situation. MoU inayopigiwa kelele na waislam ni kwamba pale ambapo serikali itatumia huduma ya kijamii ya taasisi ya kikristo basi serikali ichangie asilimia fulani ya gharama na hiyo huduma itoe huduma kwa usawa kwa watu wote bila kujali dini, jinsia, umri nk. Na hili limechochewa na serikali kuzidiwa kusambaza huduma hususan za afya. Utaona sehemu ambayo taasisi ya kanisa imeshajenga hospital, serikali inaipandisha hadhi kuwa DDH (District Designated Hospital) yaaani Hospital teule ya Wilaya na kuchangia baadhi ya gharama (sehemu nyingi haizidi 40%) na serikali badala ya kujenga hospital wilaya ile inapata fursa ya kujenga sehemu nyingine. Refer, wilaya mpya ya Kilolo, pia Ifakara, Kilosa nk.
   
 6. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ADM, jambo linalopigiwa kelele na Waislam lina historia ndefu, lakini kifupi linazihusha taasisi zote za Kikristo, na baadhi ya taasisi binafsi zinazotoa huduma za kijamii, kama Shule na Mahospitali, kufaidika na Msamaha wa Kodi wakati wanapoagiza vifaa kwa ajili ya shughuli hizo! Hoja ya msingi katika kufikia hapo ilikuja wakati Serikali ilipotangaza kuondoa misamaha yote ya Kodi mpaka katika mashirika ya Kidini ambayo hapo mwanzo yalikuwa yananufaika na msamaha. Hapo ndipo Mashirika haya YALIPOOMBA Kukaa na Serikali na kufanya majadiliano yaliyozaa MoU! Hapo ikatafasiriwa kuwa Serikali inawabeba Wakristo kwa kuwapendela kuwapa misamaha na ruzuku kuendeshea biashara hizo, wakati Serikali iko huru kuingia makubaliano kama hayo kutoka katika Taasisi za Kiislamu zenye kuhitaji kitu kama hicho. Naamni ziko taasisi za Kiislamu zinazonufaika, kwani milango iko wazi!
   
 7. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wakiristo(katoliki) wana hospitali kama Bugando,KCMC, serikali inakuwa kama mbia ktk kusaidia kuendesha hizi hospitali.
   
 8. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,573
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  Kama walivyoeleza waliotangulia MOU maana yake ni Memorandum of Understanding au waraka wa makubaliano.
  Na hii ilifanyika wakati wa uongozi wa mwinyi baada ya kuona ufanisi wa elimu katika shule za kikristo hasa shule za Katoliki, mwinyi akamtuma mjumbe Edward Lowasa aende kuongea na watu wa kanisa kwamba serikali inataka kushirikiana na kanisa katika masuala ya elimu. Kanisa likamwambia huyo mjumbe kwamba linakubali hila kwa mashariti, ndipo uliandikwa huo walaka (MOU).

  Kwanini kanisa llilifanya hivyo? Ikumbukwe kwamba katika uongozi wa hawamu ya kwanza Kanisa lilitaifishwa shule zake pamoja na hospitali zake, kutaka isije ikatokea kama mala ya kwanza wakaona watengeneze mkataba kama kinga. Miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na serikali kuchangia gharama za uendeshaji katika shule Hospitali, hii ilikuwa ni serikali ya Mwinyi ambaye ni muislamu angekuwa mkristo tungesema amependelea wakristo. Je, kwa hapo kanisa lina kosa gani?

  Kuhusu suala la kanisa kusamehewa kodi , nafikiri taasisi zote za dini zinasamehewa kodi hata zile za waislamu. Nafikiri tatizo la waislamu wanaona wakristo wanazo taasisi nyingi kuliko waislamu, ila hawakatazwi kuongeza taasisi.


  Nafikiri nimeenda kwa undani zaidi kuliko kile ulichokiuliza.
   
 9. M

  Mtoto wa tembo Senior Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ufafanuzi.
   
 10. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  sasa c unaona JF ilivyo jembe...darasa maradhiwa...kwa wote!
   
 11. moto2012

  moto2012 JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 2,166
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Huo waraka kama upo tunaomba mtuwekee hapa Jf watu tusome labda utsaidia!! Maneno ya kina ponda yanaweza yakawa ya uposhaji!! au hiyo MoU ni siri?

  Tafadhali kwa yeyote au hata viongozi wa dini wa Kikristo leteni hiyo MoU ili kuondoa maneno!!
   
 12. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
 13. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Fuata hii link hapa chini kupata MOU yenyewe ambayo inalalamikiwa.

  MoU kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini
   
 14. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chanzo cha mou ni selikali kushindwa majukumu yake hasa kujenga hospital na kuamua kuamua kuingia huu mkataba na makanisa, kinachosikitisha baada ya kuboresha hizi hosptal zimedumazwa hazijaendelezwa zaidi ya kuleta madakitari wanaolipwa na serikali na madakitari hao kuingiza rushwa katika hospital hizo na sasa huduma zake si zakitume tena kama awali ambapo kila mtu alitibiwa bila kujali dini, rangi au kipato, mbaya zaidi ni kuwa kuna kundi dogo linalojifanya waisilamu na kudai mkataba huu unawanyonya waisilamu wakati serikali kupitia mkataba huo imearibu ufanisi wa hospital hizo, naomba nichukue nafasi hii kumwomba kiongozi wangu KADINALI PENGO na balaza la maasikofu Tanzania kuvunja makubaliano yale, na kila misa kuwepo na matoleo maalumu kwa ajili ya kuchangia hospital zetu na ziboreshwe na ziendelee kutoa huduma safi kwa wote wakiwemo hawa wenye chuki na ukristu na huu ndio UKRISTU UNAVYOFUNDISHA na ni kazi ya kitume kwa wakristu kuchangia kwa ajili ya watu wote hata wale wanaokuangalia kwa jicho la husuda, tumeamriwa kuwapenda. KRISTUU TUMAINI LETU NA TUAINI LETU NI KRISTU.
   
 15. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  WAtu wa Biblia ni Jibu wabane watakutolea kopi; wanazo izo MoU nadhani. Nilisikia wakinukuu mahali.
   
Loading...