Ufahamu juu ya sheria

kamaka masunga

New Member
Jun 8, 2016
2
0
Wataaalam naomba nipate ufafanuzi kidgo je kwa mfano ukute mtu anatuhumiwa kosa dogo la kesi ya wizi japo mshtakiwa naye alikuwa anamdai na akatengenezewa kesi ya kuamua kuchukua Mali bila mhusika na kuiba hela na akakiri baadae akafikiria kuwa amefanyiwa uonevu japo alikubali je anaweza kukata rufaaa ili kesi ifanyiwe uchunguzi??????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa umeeleza kwa kupinda pinda ila nafikiri nia yako ni hii. Mtuhumiwa ameiba pesa lakini dhumuni la kuiba pesa hizo ni kufidia deni analodai kutoka kwa Mlalamikaji. Kweli hapo mtuhumiwa ametenda kosa na kama atafikishwa Mahakamani basi ili asalimike na kifungo itambidi atumie kifungu cha Sheria
SURA YA 16 KANUNI YA ADHABU
Kudai haki kwa
nia njema
9. Mtu hatawajibika kwa kosa la kijinai kutokana na na kosa
linalohusiana na mali iwapo kitendo kilichofanyika au kilichoachwa
kufanywa naye kuhusiana na mali hiyo kilifanywa kwa nia njema ya kudai
haki na bila ya nia ya kuiba.

Kuwa makini na kifungu hiki kilichoibwa kiwe kinaendana na anachodai pia awe na ushaidi utakaomsapoti kwenye hayo madai.Inaweza ikawa maelezo ya mlalamikaji mwenyewe au Nyaraka au vyovyote vile ili kuonesha kweli mtuhumiwa alikuwa anadai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Naomba kujua je kuna uhalali wiwote wa oral contract au mkataba wa makubaliano ya maneno na je unanguvu yoyote kisheria mahakamani
 
Mkuu Naomba kujua je kuna uhalali wiwote wa oral contract au mkataba wa makubaliano ya maneno na je unanguvu yoyote kisheria mahakamani
Mkataba waweza kuwa wa kuandikwa au ww maneno na zote mbili zinakubalika kisheria ikiwa tu zimefuata vigezo vyote vya mikataba halali. Hata hivyo kuna baadhi ya mikataba ni sharti iwekwe katika maandishi ndipo ipate nguvu za kisheria na moja wapo ya mikataba hiyo ni ile inayohusisha ununuzi ama kukodisha ardhi. Naomba kuwasilisha!
 
Thanks mkuu
 
Wakili naomba msaada, Nikweli mwajiri anaweza kusitisha huduma za matibabu yani (Medical Insurance) zilizo kwenye makubaliano ya kimukataba..!!? Pasipo kukupa taarifa zozote juu ya hilo nanukimuuliza anakwambia ameshindwa kukuhudumia kwa sababu za kiuchumi, naomba kuelewa hapa.

Maana Mimi mwajiri kasitisha huduma hii na nimemuandikia demand notice anilipe fidia ya M 200/ kwa kunisababishia usumbufu Mimi na familia yangu.
 
Back
Top Bottom