Ufafanuzi kutoka kwenye sheria ya ajira na mahusiano kazini mwaka 2004

YAKUTA

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
405
168
Habari ya saa hii

Naomba kukumbushwa kwa wajuzi wa sheria

Katika sheria ya ajira na mahusiano kazini mwaka 2004
naomba mnikumbushe ni kipengele kipi kinampa mtumishi wa umma hiyari kuchangia michango hasa kana ya mwenge ambayo haijapitishwa mahakamani kuchangia KILAZIMA
 
Mfanyakazi hawezi kulazimishwa kuchangia Mchango wowote ambao haujatambuliki kisheria. Makato ya kisheria ni PAYE, mifuko ya jamii(PPF, pspf, lapf, NHIF ) . makato mengine kama yale ya vyama vya wafanyakazi lazima ujaze fomu na. 6 kuidhinisha mwajiri wako akate toka kwenye mshahara wako vinginevyo akikata kabla hujajaza hiyo form unaweza kumshitaki kwenye MAHAKAMA ya kazi na ataamuliwa kurejesha fedha aliyokukata na gharama ulizotumia ktk shauri.

Mchango wa mwenge ni hiari yako .sasa waajiri huwa wanatisha watummish
 
NB MAHAKAMA haina mamlaka ya kuidhinisha michango kama hiyo ya mwenge. Kazi ya MAHAKAMA ni kutafsiri sheria na kutoa haki kisheria
 
ahsante ndugu richard kwa huo ufafanuzi mzur

ila naomba kama nitapata kifungu cha sheria itakuwa vzur zaid
 
Hakuna hicho kifungu ila jambo lolote ambalo haliko katika sheria haliwezi kukubana kama utalitenda au kutolitenda. Kuna msemo ktk sheria kuwa jambo lolote ambalo sheria haikatazi kulifanya ukilitenda huwezi kubanwa na sheria
 
Mfanyakazi hawezi kulazimishwa kuchangia Mchango wowote ambao haujatambuliki kisheria. Makato ya kisheria ni PAYE, mifuko ya jamii(PPF, pspf, lapf, NHIF ) . makato mengine kama yale ya vyama vya wafanyakazi lazima ujaze fomu na. 6 kuidhinisha mwajiri wako akate toka kwenye mshahara wako vinginevyo akikata kabla hujajaza hiyo form unaweza kumshitaki kwenye MAHAKAMA ya kazi na ataamuliwa kurejesha fedha aliyokukata na gharama ulizotumia ktk shauri.

Mchango wa mwenge ni hiari yako .sasa waajiri huwa wanatisha watummish
Ukiwa mtumishi wa umma maagizo ya mwajiri au bosi wako ni halali kisheria.
 
Siyo maagizo yote kutoka kwa mwajiri huwa halali.
Maagizo ambayo ni ya kisheria ndiyo tu yanayoweza kuwa halali. Suala la kulipia mwenge siyo halali bali kulazimisha. Kama lingekuwa halali lingewekwa kwenye pay roll. Kwa hiyo hata ukikataa kulipa mwajiri hawezi kukuchulia hatua kwani agizo hilo ni batili kisheria
 
Back
Top Bottom