Ufafanuzi kuhusu Kikokotoo kipya cha Mafao ya 33%

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,383
8,132
Kumekuwepo na hofu kubwa miongoni mwa wafanyakazi tangu kikokotoo kipya katika mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kianze kutumika hapo Julai 1, 2022. Kikotoo hicho ni matokeo ya makubaliano ya pamoja kati ya Serikali, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Moja kati ya malalamiko makubwa kuhusiana na kikokotoo hicho ni madai kwamba Serikali imeamua kupunguza malipo kwa wastaafu, huku wakosoaji wakitaja kushuka kwa malipo ya kiinua mgongo kutoka asilimia 50 mpaka asilimia 33 kama ushahidi wa malalamiko yao hayo.

Licha ya kikokotoo hicho kufanya kazi kwa takriban mwaka mmoja sasa, bado malalamiko yameendelea kuwepo miongoni mwa wafanyakazi na wastaafu, hali iliyoisukuma TUCTA kujitokeza hadharani hivi karibuni na kuitaka Serikali itoe elimu zaidi kuhusiana na suala hilo nyeti.

Akizungumza mjini Morogoro hapo Machi 9, 2023, Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya alisema kwamba moja kati ya makubaliano yao na Serikali ni kwamba Serikali ihakikishe inatoa elimu ya kutosha kwa wafanyakazi ili waelewe kikokotoo hiki kipya ni nini.

Mimi siyo mtu wa Serikali lakini nikiwa kama mtaalam wa masuala ya hifadhi ya jamii nimehisi kuwiwa kutoa mchango wangu ikiwa ni sehemu ya kusaidia juhudi hizi za kuelimisha umma kuhusiana na jambo hili muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi, wastaafu, na taifa kwa ujumla.

Usalama wa kifedha

Ni muhimu kwanza tukafahamu kwamba mfumo wa hifadhi ya jamii, ambao hufadhiliwa na wanachama wa mfuko husika kwa njia ya michango ya kila mwezi, hulenga kuhakikisha kuwa wanachama wanapata huduma za kijamii kama vile afya, elimu, pensheni, na huduma nyingine za kijamii.

Mbali na malengo hayo, hifadhi ya jamii pia huhakikisha usalama wa kifedha kwa wanachama wake pindi mwanachama apatapo janga lolote litakalosababisha yeye kupoteza kipato, ikiwemo kustaafu, ulemavu, kufiwa, uzazi, na kukosa ajira.

Kwenye fao la pensheni, mfuko hutumia zana maalum kuhesabu kiasi cha pensheni ambacho mwanachama atapokea baada ya kustaafu.

Zana hii huzingatia mambo mbalimbali kama vile muda wa kuchangia, kiwango cha michango ya kila mwezi, kiwango cha riba kinachopatikana, na muda wa malipo ya pensheni.

Kwa kutumia taarifa hizi, zana hii inaweza kutoa makadirio ya kiasi cha pensheni ambacho mwanachama atapokea baada ya kustaafu. Hii zana ndiyo huitwa kikokotoo.

Ulipaji

Kwenye malipo ya pensheni, mnufaika hulipwa kwa awamu mbili: awamu ya kwanza inaitwa mkupuo, au kiinua mgongo, na awamu ya pili ndiyo wengi tunaifahamu inaitwa pensheni ya mwezi ambapo mnufaika hupokea malipo ya pensheni kila mwezi.

Nataka niseme hapa kwamba siyo kweli kwamba kiwango cha pensheni kimepanda au kimeshuka kwa mnufaika tangu Serikali itangaze matumizi ya kikotoo kipya hapo Julai 2022.

Kilichobadilika baada ya kutangazwa kwa kikotoo hicho ni njia za kukokotoa haya malipo katika awamu zote mbili za malipo, yaani kiinua mgongo na malipo ya kila mwezi.

Zamani kabla ya hiki kikokotoo kipya cha asilimia 33, mnufaika wa pensheni alikuwa analipwa asilimia 25 katika malipo ya mkupuo, yaani malipo ya awamu ya kwanza, kwa kutumia kanuni ya CP = (1/580*N*APE) *12.5*25%) na malipo ya awamu ya pili akilipwa asilimia 75 kwa kutumia kanuni ya MC = (1/580 * N*APE)*75%*1/12).

Kilichobadilika ni kwamba sasa hivi mnufaika wa pensheni atakuwa analipwa kiinua mgongo, yaani malipo ya awali, asilimia 33 kutoka asilimia 25 na malipo ya kila mwezi atakuwa analipwa asilimia 67 kutoka asilimia 75.

Kwa hiyo, tunaweza kuona hapa kwamba kilichoongezeka ni malipo ya awali huku malipo ya kila mwezi yakipungua. Lakini malipo kwa ujumla yako vilevile, yaani asilimia 100 (33 + 67 = 100) kama inavyoonekana hapo juu.

Mnufaika alipwe pesa zote?

Kwa mtazamo wangu, faida moja wapo ya kikokotoo hiki kipya ni kwamba mnufaika wa pensheni atalipwa kiinua mgongo kikubwa tofauti na zamani, na hivyo kumfanya kuwa na uwezo mkubwa wa kuwekeza na kufanya mambo yake mengine baada ya kustaafu.

Nafahamu baadhi ya madai ambayo yamekuwa yakitolewa na wafanyakazi, wastaafu, na wadau wengine wakishinikiza walipwe pesa zao zote baada ya kustaafu.

Hata hivyo, nasikitika kuhitimisha kwamba jambo hili ni gumu kulitekeleza kwani siyo tu lipo nje ya sheria na miongozo ya hifadhi ya jamii Tanzania bali pia ni kwenda kinyume na dhana nzima ya hifadhi ya jamii.

Duniani kote, pia, hakuna sehemu ambako utaratibu kama huo unatumika.

Nihitimishe safu hii kwa kukumbusha kwamba lengo kubwa la pensheni ya kustaafu/uzee ni kukulinda/kumlinda mnufaika wa pensheni kwenye kipindi chote cha uzee mpaka pale atakapo kufa.

Zipo hasara nyingi za kiuhifadhi wa jamii endapo kama wanufaika watalipwa malipo yao yote kwa asilimia 100, kwa ujumla, pale anapo staafu.

Hizi ni hasara zinazogusa pande zote, mfuko husika na mnufaika pia!

THE CHANZO
 
Kwanini hamfanyi hivyo na kwa Wabunge kwa kuwapa 33% wanapomaliza miaka yao mitano kule Bungeni?

Acheni bla bla zenu hapa. Fedha ni ya mstaafu, na amechangia mfuko kwa miaka mingi! Hiyo haki ya kumpangia matumizi yake mnaitoa wapi?

Acheni janja janja zenu. Wapeni wastaafu hela zao, ili wakafanyie mambo yao ya msingi. Na msipofanya kabla ya 2025, mtakuja kunipa mrejesho.
 
Nihitimishe safu hii kwa kukumbusha kwamba lengo kubwa la pensheni ya kustaafu/uzee ni kukulinda/kumlinda mnufaika wa pensheni kwenye kipindi chote cha uzee mpaka pale atakapo kufa.

Kwani ile miaka 12 baada ya kustaafu imebadilishwa? Kumbe sasa ni mpaka kufa? NA SWALI JINGINE, HIVI PESA ZA MAFAO YA KUSTAAFU HUWA NI ZA NANI? ZA MSTAAFU? ZA SERIKALI?
 
Kwa nini hamfanyi hivyo na kwa Wabunge kwa kuwapa 33% wanapomaliza miaka yao mitano kule Bungeni?

Acheni bla bla zenu hapa. Fedha ni ya mtaafu, na amechangia mfuko kwa miaka mingi! Hiyo haki ya kumpangia matumizi yake mnaitoa wapi?

Acheni janja janja zenu. Wapeni wastaafu hela zao, ili wakafanyie mambo yao ya msingi. Na msipofanya kabla ya 2025, mtakuja kunipa mrejesho.
Nakubaliana na maoni ya mtoa maoni kwa condition kubwa moja "Kama hicho Kikokotoo" Ni kizuri, ni Bora sana na waliokitengeneza Wana Nia njema sana na wastaafu, Basi Kuwe na Kikokotoo kimoja kwa wastaafu wote ikiwemo TABAKA la Wanasiasa.
 
Nihitimishe safu hii kwa kukumbusha kwamba lengo kubwa la pensheni ya kustaafu/uzee ni kukulinda/kumlinda mnufaika wa pensheni kwenye kipindi chote cha uzee mpaka pale atakapo kufa.

Kwani ile miaka 12 baada ya kustaafu imebadilishwa? Kumbe sasa ni mpaka kufa? NA SWALI JINGINE, HIVI PESA ZA MAFAO YA KUSTAAFU HUWA NI ZA NANI? ZA MSTAAFU? ZA SERIKALI?
Kama ni kwa nia njema fedha inayobakia baada ya mnufaika kufariki wapewe watoto wa mnufaika. Kwa nini serikari ihodhi fedha halari za mtumishi mstaafu.

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
NAOMBA UNISAIDIE KATIKA HILI KWA VITENDO NA SIO NADHARIA

Mfano msitaafu aliyemaliza utumishi wake akiwa na mshahara wa basic 1,500,000/= huku akiwa ametumikia serikali kwa miezi 300, kabla ya july 2022 mkupuo angelipwa kiasi gani na pensheni kiasi gani kila mwezi?, pia msitaafu huyo huyo mwenye sifa tajwa hapo juu angestaafu baada ya july 2022 mafao yake yangekuwaje?.
 
Wale watu waliokuwa wanakuwa wa kwanza Darasani, wakaenda mavyuo, Sasa ni watumishi, wale back banchers , walioshindwa kabisa hesabu na kiingereza waliofeli la Saba, waliopata zero na four form four Sasa hivi ni wafanyabiashara wakubwa, wafugaji na wakulima. Wana vitega uchumi vingi na wanajua ujasiriamali, yeye kwake hajui kitu kinaitwa kustaafu
 
Yaa,Kama anataka watu waelewe alete mfano halisi,sio maneno tu na kanuni
 
Wale watu waliokuwa wanakuwa wa kwanza Darasani, wakaenda mavyuo, Sasa ni watumishi, wale back banchers , walioshindwa kabisa hesabu na kiingereza waliofeli la Saba, waliopata zero na four form four Sasa hivi ni wafanyabiashara wakubwa, wafugaji na wakulima. Wana vitega uchumi vingi na wanajua ujasiriamali, yeye kwake hajui kitu kinaitwa kustaafu
Maisha hayako na formula hiyo. Acha kujiliwaza kijuha
 
Kwa nini hamfanyi hivyo na kwa Wabunge kwa kuwapa 33% wanapomaliza miaka yao mitano kule Bungeni?

Acheni bla bla zenu hapa. Fedha ni ya mtaafu, na amechangia mfuko kwa miaka mingi! Hiyo haki ya kumpangia matumizi yake mnaitoa wapi?

Acheni janja janja zenu. Wapeni wastaafu hela zao, ili wakafanyie mambo yao ya msingi. Na msipofanya kabla ya 2025, mtakuja kunipa mrejesho.
Kweli kabisa, wasipolekebisha kabla ya 2025 itakula kwao.
Wastaafu wengi wanalalamika mitaani.

Halafu,kama ni asilimia 33 kwa 67 (mkupuo + pensheni ya kila mwezi) kwanini isiwe 70 kwa 30? kwani nayo si 100%
 
Kama ni kwa nia njema fedha inayobakia baada ya mnufaika kufariki wapewe watoto wa mnufaika. Kwa nini serikari ihodhi fedha halari za mtumishi mstaafu.

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
Wezi tu hao. Hawana lolote. Wao wenyewe wanapeana mafao yote wanapostaafu. Halafu watumishi wa chini ndiyo wanawaletea hicho kikotoo chao cha kipuuzi.

Waanze wao kwanza kupeana hizo 33% halafu tuone kama watakubali. Hayo matakataka ya TUCTA ndiyo kabisaaa! Hata aibu hayana kwa kuwageuka wafanyakazi, na kushikamana na dola iliyojaa uonevu.
 
HIVI PESA ZA MAFAO YA KUSTAAFU HUWA NI ZA NANI? ZA MSTAAFU? ZA SERIKALI?

Ni za Mstaafu ila Serikali inazichukua na kufanyia mambo yake inayotaka mfano ile Hasara ya Ujenzi wa Ile Village kule Kigamboni ambayo imekwama na wanataka kuiuza halafu haipati mnunuzi.

Kwa mantinki hiyo hela inazochukua kwa watumishi zinakuwa hazitoshi kuwalipa kwa mkupuona ndio wakaamua kutunga sheria ya kulipa wastaafu kidogo kidogo(kikokotoo).

NAWAZA HIVYO KWA HERUFI KUBWA.
 
Back
Top Bottom