Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Naandika kwa ufahamu na uzoefu wangu kutokana na kuwa mhudumu wa chumba cha maiti(mochwari) hapo kabla.. Nimewahudumia marehemu wengi kwa nyakati tofauti na wa jinsia na rika tofauti
Tangu tuhuma zilipotolewa siku mbili zilizopita na makamu wa rais jijini Mwanza akituhumu maji ya kuoshea maiti kama kisababishi cha ugonjwa wa saratani (sijui ni ipi mojawapo maana ziko nyingi) kutokana na kutumiwa kwenye kitoweo cha samaki na wafanyabiashara wa hiyo mboga.. Nilisita sana kuweka hii mada lakini kwenye kila uzi uliohusu hiyo tuhuma nilijitajidi kutoa ufafanuzi lakini nimegundua bado mkanganyiko ni mkubwa
Sasa iko hivi je maji ya mochwari ya kuoshea maiti ninini?
Haya ni maji ya kawaida kabisa yale ya kuuzwa dukani ama ya kisima ama ya DAWASA
Ni maji ya kumsafisha marehemu marehemu ama kumuogesha kwa ajili ya kumuandaa kwa safari yake ya mwisho na kumvisha nguo nzuri.. Hakuna la zaidi kama kumuogesha tu mtu yoyote anayetaka kuoga mwenye uchafu wa kawaida mwilini usoni sehemu za siri nk
Tunawaogesha ama kuwaosha marehemu kama maandalizi ya safari yao ya mwisho kwakuwa mara nyingi kwenye kitanda cha ugonjwa hawaogi/ogeshwi vizuri, ama kama ni mwili wa ajali kuwa na damu, vumbi tope nk..
Naendelea
Kimsingi si kumuogesha bali ni kumsafisha kwa taulo na maji ya sabuni, kumfutafuta na kumuosha sehemu mbali mbali za mwili
Kifuatacho ni kumpaka mafuta na kumremba, kumpulizia marashi fulani makali yanayodhibiti harufu yoyote kwa haraka kisha kumpulizia chemicali ya fomalin inayozuia mchakato wa mwili kuoza haraka.. Maana baada ya pumzi tu kuacha mwili kuoza na kuharibika ni haraka mno
Kwahiyo maji ya kuoshea maiti maarufu kama maji ya mochwari hayana tofauti na yale maji unayooga wewe.. Labda tu ni kwamba yale yanaosha mfu
Haya maji hayamwagwi hovyo na si maji ya kuyaweka muda mrefu maana yana uchafu wa mfu unaooza na kunuka sana
Maji ya mochwari kwenye ulimwengu wa roho ni maji mfu yasiyofaa chochote kwenye kutengeneza ngekewa mvuto nk iwe wa kimapenzi au kibiashara.. Ni maji yanayotumika kishirikina kuharibu kufisha, kuua, kutengenisha nknk.. Kamwe huwezi kuyatumia kuweka kwenye kitoweo cha samaki waliokufa.. Wataoza chini ya masaa 6
Sasa basi ninnini kilichoitwa maji ya mochwari? Hicho kitu ni ile chemikali ya fomalini inayozuia uharaka wa kitu chenye nyama kuoza haraka
Wavuvi wengi hawana majokofu ama vyombo vya kuhifadhi muda mrefu samaki wao kabla ya kumfikia mlaji wa mwisho.. Hivyo hupata fomalin kwa njia za magendo na kuitumia kuhifadhia mawindo yao.. Na hii sio kwenye samaki tu bali hata kwenye mabucha mbali mbali nchini ya nyama nyinginezo
Matumizi ya fomalin kwa ajili ya kuhifadhia vitoweo vya nyama tuhuma zake ni za muda mrefu sana tangia enzi za mzee ruksa, lakini kwa vile madhara yake si ya papo kwa papo.. Wafanyabiashara wasio wazalendo na watumishi wasio waaminifu wameendelea kutuumiza. Na si fomalin zote zinatoka mochwari nyingine hazifiki kabisa
Makamu wa rais anapaswa kurudi kwenye media na kutoa ufafanuzi kuepusha mkanganyiko kwenye jamii

karibu mtani niulize tuu.. Lakini yale ni maji mfu hayana jema ndio maana hayamwagi hata mtaroni wala hayafukiwi ardhini isipokuwa kwa sababu maalum