Ufafanuzi jamani manake hii ni aibu

Ufafanuzi jamani manake hii ni aibu

Nkissa

Member
Joined
Sep 7, 2012
Posts
51
Reaction score
9
Naomba kuwauliza wana jamvi,Mimi ninamzazi mmoja yaani mama ndo aliyebaki kwani Baba yangu alifariki miaka 8 iliyopita kwa upande wetu tumezaliwa wengi na tayari tuna watoto wa kuwazaa wanafikia kama 27 ( wajukuu wa mama ) cha kushangaza mama yetu ameanza tabia ya uzinzi na mbaya zaidi anamleta jamaa mpa home na kulala nae kitanda alichokuwa analala na marehemu Baba yetu,na pia anakuja nae mjini tunapoishi na kupokelewa na kaka yetu na analala na huyo jamaa kwa kaka.mimi hiyo hali napingana nayo na imenifanya nitengwe kwani nilikereka sana nilipogundua.

Nawasilisha
 
naomba kuwauliza wana jamvi,mimi ninamzazi mmoja yaani mama ndo aliyebaki kwani baba yangu alifariki miaka 8 iliyopita kwa upande wetu tumezaliwa wengi na tayari tuna watoto wa kuwazaa wanafikia kama 27 ( wajukuu wa mama ) cha kushangaza mama yetu ameanza tabia ya uzinzi na mbaya zaidi anamleta jamaa mpa home na kulala nae kitanda alichokuwa analala na marehemu baba yetu,na pia anakuja nae mjini tunapoishi na kupokelewa na kaka yetu na analala na huyo jamaa kwa kaka.mimi hiyo hali napingana nayo na imenifanya nitengwe kwani nilikereka sana nilipogundua.

Nawasilisha

we mtoto unataka kumshika mama yako ugoni?
Anyway,huwa haipendezi kama huyo mwanamme atakuwa na umri mdogo kuliko ninyi.lakini pia unaweza ukakaa na mama ukamweleza kitu ambacho hukipendi kuhusu yeye
 
dah.....huyo ni mama yako mzazi kabisa.......?.....ingekuwa mimi.....ningeficha siri ya mama singeisema hapa.....halafu.....kama baba amefariki.....mama haruhusiwi kupata huduma za msingi kama binadamu....?.....angekkuwa kafa mama.....baba yenu angeleta mama wa kambo.....nae pia ungekuja kutuuliza........?
 
Kimaadili huwezi kumhukumu mama yako hasa katika masuala ya uzinzi...Kaa mbali.
Waachie baba zako wadogo, wajomba, shangazi, bibi, babu na mama zako wadogo.
 
kiapo huwa "mpaka kifo kitutenganishe". Sidhani kama anakosea
 
SnowBall i see u here in this thread all u should know i miss u so much my brother
 
Last edited by a moderator:
Kimsingi wewe ni mtoto na hivyo una mipaka ya kimamlaka juu ya mzazi wako (mama) japo hali hiyo inakwaza nafsi, lakini kwa kua hujasema kama mama ameolewa tena basi atakua anazini lakini bado hatutakiwi kuwa majaji katika hili mi nadhani huyu jamaa anaedate na mama ndie anastahili kuwa mstaarabu maana hajaoa na hata kama angeoa hastahili kulala kitanda kile kile alicho lala marehemu mzee wenu mi nashauri ita ndugu zako mjadili kiutu uzima kisha mtumie wazee waongee na mama kama vipi aende kwa huyo jamaa nyie mmuhudumie huko siyo kutumia privacy za marehemu kwa stail hiyo.
 
Naomba kuwauliza wana jamvi,Mimi ninamzazi mmoja yaani mama ndo aliyebaki kwani Baba yangu alifariki miaka 8 iliyopita kwa upande wetu tumezaliwa wengi na tayari tuna watoto wa kuwazaa wanafikia kama 27 ( wajukuu wa mama ) cha kushangaza mama yetu ameanza tabia ya uzinzi na mbaya zaidi anamleta jamaa mpa home na kulala nae kitanda alichokuwa analala na marehemu Baba yetu,na pia anakuja nae mjini tunapoishi na kupokelewa na kaka yetu na analala na huyo jamaa kwa kaka.mimi hiyo hali napingana nayo na imenifanya nitengwe kwani nilikereka sana nilipogundua.

Nawasilisha
That is non of your business just step away from that.
 
dah.....huyo ni mama yako mzazi kabisa.......?.....ingekuwa mimi.....ningeficha siri ya mama singeisema hapa.....halafu.....kama baba amefariki.....mama haruhusiwi kupata huduma za msingi kama binadamu....?.....angekkuwa kafa mama.....baba yenu angeleta mama wa kambo.....nae pia ungekuja kutuuliza........?

'kuna taratibu za kufatwa sio kiholela tu,mama wa kambo mpaka anaitwa mama kuna taratibu zimefatwa ndoa thats why anaitwa mama wa kambo sio kukurupuka tu...'
 
Ni haki ya mama kudate mtu yeyote anayemtaka kama mume wake wa ndoa ameshatangulia mbele ya haki. tatizo litakuwa labda yeye kuja nyumbani. Kama huyu angekuwa mama yangu ningemuacha aenjoy maisha yake na tena kama watoto tuko na mishe mishe zetu za maisha inakuwa bora anapata mtu wa kuliwaza
 
Wewe unataka laana za wazazi wewe. Acha kabisa mambo hayo, kaka yako anaakili sana. Tena nakusihi
acha mambo ya mama yako, Jiepushe kabisa, tena mama!!! duh angekuwa baba. Mama kakulea miezi 9 tumboni

Tena umefanya kosa kubwa sana kuleta hapa JF.
 
Chamsingi usifumfuatilie huyo ni baba yako na angelikuwa ni mama amefariki hata baba yako angelioa mwingine hivyo usiteseke kwa hilo mpe heshima kama kawaida na jifanye huna unalojua kuhusiana na huyo baba
 
Shida ni kulala kwenye kitanda ambacho ur late father alikua pia analala au ni kuja kulala nae kwa kaka? Mi mbona naona poa tuu ili mradi ni mmoja tuu na sio mdogo kiumri.
 
Mama yako kwani siyo binadamu mpaka awe asiwe na nyege.
Ukiona mwanamke anaweka hadharani mambo yake ujue kabisa jamaa aliyenaye kampagawasha. Na mwanamke akipagawisha hata mfanye nini, ni sawasawa na kutwanga maji kwnye kinu.
Ukitaka kufanikiwa na usiumie moyo, toa ushawishi ili Mama na Baba wa kambo wafunge ndoa.
Na umchukulie huyo Baba as if ni Baba yako mzazi.
 
Back
Top Bottom