Nimefurahi sana kupata ufafanuzi kutoka kwako bwana Kibanga. Naendelea kushauri.
Chadema waone umuhimu wa kuwa na Katibu mwenezi badala ya kuwa na kurugenzi yenye mchanganyiko wa majukumu.
Ukitazama hapo unaona Kiongozi wa hii kurugenzi ya uenezi Hemedi Alli ni mgeni masikioni na machoni pa wengi. Vyombo vikubwa vya habari Sidhani kama anafahamika au anavitumia vya kutosha.
Nahitimisha kuwa kuna tatizo la ki muundo wa chama na hii imesababisha chama kujieneza kwa njia za kimafia kupitia watu kama Mdude , Mange, na wengine.
Tatizo hili linawapa kazi ngumu Katibu mkuu na mwenyekiti kufanya shughuli za uenezi na kuwafanya kuzoeleka. Ndio sababu Polepole anamparamia Mbowe .Angalikuwapo Katibu mwenezi mwenye nguvu angewalinda viongozi wa juu kwa ku absorb pressure za chini na kufanya baadhi ya Press.
Chadema pokeeni ushauri huu.
Sent using
Jamii Forums mobile app