Uenezi CHADEMA jukumu la nani?

Nimefurahi sana kupata ufafanuzi kutoka kwako bwana Kibanga. Naendelea kushauri.

Chadema waone umuhimu wa kuwa na Katibu mwenezi badala ya kuwa na kurugenzi yenye mchanganyiko wa majukumu.

Ukitazama hapo unaona Kiongozi wa hii kurugenzi ya uenezi Hemedi Alli ni mgeni masikioni na machoni pa wengi. Vyombo vikubwa vya habari Sidhani kama anafahamika au anavitumia vya kutosha.

Nahitimisha kuwa kuna tatizo la ki muundo wa chama na hii imesababisha chama kujieneza kwa njia za kimafia kupitia watu kama Mdude , Mange, na wengine.

Tatizo hili linawapa kazi ngumu Katibu mkuu na mwenyekiti kufanya shughuli za uenezi na kuwafanya kuzoeleka. Ndio sababu Polepole anamparamia Mbowe .Angalikuwapo Katibu mwenezi mwenye nguvu angewalinda viongozi wa juu kwa ku absorb pressure za chini na kufanya baadhi ya Press.

Chadema pokeeni ushauri huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na Msemaji wa serikali mipaka yake inaishia wapi, mbona janga la Corona hatujamsikia akiisemea serikali?!
 
Na Msemaji wa serikali mipaka yake inaishia wapi, mbona janga la Corona hatujamsikia akiisemea serikali?!
Eneo la uenezi linahitaji mtu mwenye ushawishi huyu mtu awe na wdhifa mamlaka na huyu mtu apate wasaidizi makini vitendea kazi fungu la kutosha, akifahamu chama aifahamu nchi yake na aifahamu siasa ya nchi kihistoria na siasa ya kipindi.

Huyu ofisa anapaswa kupewa Uhuru wa kufanya kazi yake na Sapoti ya walioko juu yake.

Sioni idara ya uenezi yenye sifa hizo ndani ya chama changu Chadema.

Mbona hujajibu swali?! Msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Abas umemsikia lini akiusemea serikali ya JMT tangu Corona ianze?! Hana ushawishi au hana cha kuongea?!
 
Kwa miaka mingi nimekuwa nikifuatilia namna Chadema inavyo jitangaza na kutafuta ufuasi. Katika jambo linalonipa maswali ni kutosikika kwa idara yake ya uenezi.

Sijafahamu vizuri kitengo cha uenezi kama kipo kwa jina jingine au hakipo na shughuli zake zimeelekezwa kwenye ngazi ipi. Ukifuatilia CCM kitengo cha uenezi miaka yote kinapewa nguvu na penda usipende, mwenezi wa CCM anafahamika katika ngazi ya taifa na MIKOA mikubwa.

Sijafahamu kama tatizo la Chadema ni muundo, mfumo wa utendaji au kumekuwa na waenezi dhaifu miaka yote.

Kuna baadhi ya majina kama Mtelemwa, Mushi, Makene sifahamu hawa ni maafisa habari au waenezi.

Kama kweli Chadema hawana hiyo ngazi ya uenezi basi muundo wao unawapunguzia nguvu ya kujiuza kwa wananchi. Ni vizuri Chadema wakatathmini muundo na nguvu wanayopaswa kuzipa idara zake .

Waenezi ni muhimu ngazi zote kuanzia taifa, Kanda, Mikoa , Wilaya, Tarafa na Kata. Si nafasi ya kupuuza.
Achana na chadema wewe vaa barakoa
 
Mbona hujajibu swali?! Msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Abas umemsikia lini akiusemea serikali ya JMT tangu Corona ianze?! Hana ushawishi au hana cha kuongea?!
Msemaji wa serekali anasema sana tu fuatilia na anafahamika. Msemaji wa CCM anafahamika na anaeneza kwa uwazi na chini kwa chini.

Polepole ameidhuru sana Chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tunaposema Chadema imekufa inashindwa kuelewa ?

Hao wamepoteza mwelekeo Tusubiri October tuzike
Chadema wamekufa sasa Mbona bado watu wanahangaika nao sana..!? ya nini kuhangaika na mfu. Hata maandiko yanasema kitu kikifa na kumbukumbu lake linafutika.Mfano kuna gazeti moja la kila wiki, yani chadema tu na viongozi wake utazani hamna habari zingine za kuandika. Hii CDM ishakufa sasa ya nini kuizungumzia tuiache tu hiyo octoba
 
mbowe ndo kila kitu pale, mwenezi, head and assitant, mkusanyaji ruzuku yaani kila kitu anafanya yeye
 
mm hua naomba NCCR wapate wanachama wapya ili wawe chama kikuu cha upinzani
Kutokukasimu madaraka kunamfanya mbowe ajikute katika mashambulizi mengi.

Ni jambo zuri Mbowe asigombee Hai ili apate fursa ya kuwakampenia wabunge madiwani na mgombea u rais vinginevyo atajipigania mwenyewe atakosa ubunge na kupoteza viti vingi vya ubunge udiwani na mgombea urais kuambulia kipigo

mwenzako anawaza ruzuku
 
Hio ni katiba ya chadema
Screenshot_20200518-205247.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom