Uelekeo wa TMJ Hospital

Uelekeo wa TMJ Hospital

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2011
Posts
303
Reaction score
154
Habari zenu ndugu!!

Ninaomba msaada wa kuelekezwa, kama ninatokea Mawasiliano nataka kwenda TMJ hospital, ninapanda magari ya wapi na ninashukia kituo gani?

Je, TMJ wanapokea Bima ya afya?

Tafadhali
 
Mwenge to posta via mwinyi rd, shuka morocco, kuna barabara inakwebda mikochen nenda kwa mguu, au pik2 sh500/1000. Ni km 1 hiv. Iko karib na US embassy, zantel, ila iko opposite na mafair plaza.
 
Kutokea mawasiliano panda gari ya kawe shukia mwenge, hapo panda gari inayoenda posta au hata kariakoo. Shuka morocco hapo utaziona daladala nyingi tu zinazoenda kawe shukia kituo cha chama utakuwa umefika TMJ wanapokea bima pia
 
Kutokea mawasiliano panda gari ya kawe shukia mwenge, hapo panda gari inayoenda posta au hata kariakoo. Shuka morocco hapo utaziona daladala nyingi tu zinazoenda kawe shukia kituo cha chama utakuwa umefika TMJ wanapokea bima pia

Ndg kituo cha mabasi ya posta/k koo kioo makumbusho.kama yupo mawasiliano apande magari yanayoenda makumbusho. Kutoka hapo ndio atapata magari yanayo kwenda posta/k koo. Ashuke moroco then apande hayo yanayo kwenda kawe
 
panda gari za Kawe,waambie msaada Tmj maana kituo ni darajani kiko nyuma kidogo.bima wanapokea.

angalia asije panda magari ya kawe yanayopitia mwenge....

panda gari mpaka Moroko, ukifika moroko panda gari za kawe halafu fata kama alivyosema huyu ndugu
 
Habari Mkuu,Kama upo Simu2000,Panda magari yaendayo msasani waambie wakushushe kituo kinaitwa UBALOZI,Ukishashuka utaona Pikipiki hapo kama mfuko upo vizuri ni Jero au Buku mpaka TMJ maana ni 400m tu,Kama unaweza kutembea muulize mtu yeyote hapo Shoppers Plaza au May Fair Plazer ipo wapi? Watakwambia Nyoosha hiyo barabara ya kwenda Kawe moja kwa moja utaona Shopping Malls ya upande wa kushoto ni Shoppers na ya kulia ni May Fair,ukishafika karibu na hizo Malls uliza Mtu yeyote hapo TMJ ipo wapi? Atakuonyesha Jengo hilo Hapo Mbele yako.
 
Nafunga mjadala.....panda kifodi kiendacho kwa Mromboo,teremka Ngarnaro upande cha Sembetini[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom