UDSM na mashinado ya ZAIN imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM na mashinado ya ZAIN imekaaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kandambilimbili, May 13, 2009.

 1. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kusikia maongezi ya watu kuhusiana na mashindano yanayoondeshwa na ZAIN kwa vyuo vikuu.

  Nilisikia kuwa UDSM inatia aibu kweli kweli na ini dalili mbaya sana kwa elimu ya Tanzania, vijana wanashindwa kujibu maswali rahisi rahisi, wakati mwingine wanachagua maswali kwenye field amabazo hawana ujuzi mfano mtu wa B. Com anachagua maswali ya Medicine utaweza kweli????

  Hata hivyo nasikia uchaguzi wa nani aende kwenye mashindano hayo umegubikwa na UFISADI wakati vyuo vingine wanaochagua ni walimu ambao uangalia wanafunzi VICHWA nasiki UDSM wanajichagua wanafunzi na uongozi wa wanafunzi, ili uchaguliwe inabidi ugawane zawadi utakazopewa na hao FISADI waliokunominate.

  Jee hii ina ukweli wowote na imekaaje? Wana UDAM mnasemaje? mimi sijui ni TETESI nimezipata mahali.
   
 2. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi hawana general knowledge na elimu tunayopata pia inachangia kuwa na mawazo myembaba tunaweka msisitizo kwenye ujuzi wa taaluma zetu tu. Wakenya na waganda kwa upande mwingine hata kwenye maongezi ya kawaida unaona wanajua mambo mengi. Utamaduni wa kujisomea ndio unazidi kutokomeza. Ubingwa wa masomo ya darasani haimaanishi ujuzi wa mambo ya dunia pia...
   
 3. Miwani

  Miwani Senior Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 182
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  UFISADI sio serinalini tu, hata kwenye vyuo vya elimu. unafikiri mwanafunzi atawezaje kulipa 40% ya ada kama asipofanya mbinu za KIFISADI kama hizo
   
 4. Isimilo

  Isimilo JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shindano la zain ni la kishenzi haliendai na hadhi ya mwanafunzi wa chuo kikuu. maswali yanayoulizwa kwa mtindo ule yanafaa shule za msingi tena darasa la nne. huwezi kumuuliza interllectual kwa staili ile. watu wanatakiwa kujifunza ubunifu sio kukalili au kutakiwa kujibu kwa pupa. ni ujinga. ni udhalilishaji wa taaluma kwa bara la Africa
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Jamani ni balaa mbona naona kama tunaburuzwaa......duu hadi najisikiaga aibu..sijui ni english ndio tatizo au hatuna conf sijui...ila duu ni soooo
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...fafanua hoja yako mkuu. Nilidhani kuwa shindano hilo lilikuwa kipimo kizuri cha ufahamu na wepesi wa kusolve problems wa hao intellectual unaowasema? Unataka katika dunia hii inayokwenda mbele kwa kasi ya kutisha kila unapopewa swali basi upewe na muda wa kulifikiri kii-intellectual??:rolleyes:
   
 7. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mawazo kama haya ndio yanachangia kubaki kwetu nyuma, ingekua hivyo mbona wanayashindwa? Ni changamoto nzuri kabisa halina ushenzi kama unavyodai
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  .. Na juzi ndio ilikuwa aibu zaidi! Kile chuo gani sijui cha uganga cha Daressalaam, tena kina neno International, ilikuwa ni aibu tupu! yaani walikuwa wanaonyesha kuwa hawana general knowledge ya mambo mengi yanayoendelea duniani!!!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Its just a game guys..relax..
   
 10. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #10
  May 14, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  NOPE, this is more than a game, hata kama HOJA IKO PALE PALE, tunatia AIBU alafu sie hao hao ndio tunajiita CHUO BORA TANZANIA.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ubora wa ilmu inayotolewa na chuo X haihusiani moja kwa moja na perfomance ya mwanafunzi Y ktk dubious 'challenges' at time t and location XYZ.

  Huwezi kupima ubora wa mwanafunzi X kwa kutumia lisaa limoja au swali moja au vyote 2, let alone ubora wa chuo anachotoka.

  Tunachofanya ni kusema UDSM imetolewa lakini thats by convention tu(maybe we don't have a better word) kwa sababu it is debatable, as UDSM sio individual au groups of random people bali ni entire wadau.
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280


  Hamna cha ufisadi wala nini, tatizo ni kama alivyosema mkubwa Nkamagi kwamba general knowledge kwa wabongo ni zero! Mtu akienda UDSM kusoma Engineering tayari keshajiona Engineer na anakushangaa kwanini unamwambia aende kwenye kipindi cha General Studies! Mtoto wa A-Level nae anayesoma PCB tayari anajiona keshakuwa MD na wala haoni umuhimu wa Develpment Studies!! Heri tukwepe DS na GS wakati tunapenda kusoma vitabu lakini nalo ni kama kumwambia Osama asome Agano Jipya!!
   
 13. D

  Dandaj Member

  #13
  May 14, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kumbukumbu zangu, vyuo viliingia kwenye mashindano hayo kutoka TZ ni vinne tu navyo ni Muhimbili, IMTU, Mzumbe na SAUT. Je hiyo UDSM ilikuwepo lini kwenye mashindano hayo? Nimeshindwa kuchangia hiyo mada ya UDSM na mashindano ya ZAIN imekaaje baada ya kukumbuka UDSM haikuwepo katika mashindano hayo.
   
 14. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kweli kabisa kile chuo cha IMTU kilitia aibu sana, ilifika hatua walikaa kimya kabisa...japo mwenzao mmoja alikuja kuwaokoa mwishoni kidogo...ule mchenzo sio mbaya kama wengine wanavyosema...kwanamna fulani unareflect mfumo wetu wa elimu...Tanzania tunakamua sana taaluma ya darasani kuliko real situation duniani, elimu yetu ni ya kufikirika mno na mitaala yetu bado ni ya zamani haiendani ni technological changes...most of the best students from Engineering are now either good accountants or finance managers kwa kuwa walipopewa kazi za taaluma waliyosomea walichemka...

  the challenge is good...nadhani tu vyuo vijaribu kupeleka wawakilishi bora zaidi...
   
 15. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2009
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 487
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  tatizo ni general knowledge coz wanafunzi hawapati muda wa kusoma vitabu na other journals wanaconcetrate katika notes za darasani sana coz maprofesa wa pale wanakomoa wanadhani mwanafunzi anakuwa mzuri kwa vitu vigumu. Sema ndio the best university Tanzania kwa sasa
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mnaweza kutupa mfano wa maswali yanayoulizwa?
   
 17. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  You are wrong siyo kwamba mtu kubadili kutoka engineer na kuwa good accountant au good manager maana yake ameshindwa kazi za engineering!! TOO WRONG!! Maana yake huyo ni mtu safi katika mambo yote ndiyo maana ameweza ku switch from one field to another na anaziweza!! Fuatilia vizuri utakuta engineers wengi wanasoma MBA ili iwasaidie katika management na wanakuwa the best managers duniani kote.
   
Loading...