VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Chuo Kikuu ni sehemu ya ukomavu wa kifikra. Fikra za kubuni,kuendeleza,kuhoji,kupongeza na hata ikibidi kuponda hupatikana chuo kikuu. Nasema,chuo kikuu ni tanuru au kisima cha fikra pevu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM hadi leo kilipobadilishwa.
UDSM,leo,imepandishwa meli ya kusifu bila kuhoji;kutenda bila kufikiri na kuahidiwa ili kupendelewa. Leo,Rais na timu yake wametumia mbinu ya kumwaga sifa. Kuanzia viongozi wa chuo hicho,wahadhiri,waendeshaji na hata wanachuo wote wamesifiwa tu.
Wanachuo wameitwa vipanga;wahadhiri wameitwa wabobezi na waendeshaji wameonekana mahiri. Kila mmoja kwa nafasi yake akajazwa sifa. Halafu,wa vyuo vingine wakapondwa na kuachwa nyuma. Wana-UDSM wakashangilia bila kulia. Wakasahau au kujisahaulisha kuwa wahadhiri wa UDSM huadhiri na kwenye vyuo vingine.
Rais Magufuli na Mkuu wa UDSM Kikwete wakafanikiwa kuiteka UDSM na kuifanya jukwaa la kisiasa. CCM ikatajwa na kutamalaki. Mambo yakapangwa na kupangika. Kila mzungumzaji hakuhoji,alisifu tu. Wana-UDSM nao wakacheka na kushangilia hata ilipotumika lugha kali,ya kejeli za kweli.
UDSM imepatikana. Imekamatika. Si ile tena. Siri yao iko wazi. Ponda wale utapendwa; wasifu watakusifu!
Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam