Hiyo ndo hali ya aibu inayolikumba taifa, watalaam wazuri wasema ukweli wanasumbuliwa sana na siasa za matumbo za watalawa; LAKINI MPIGANAJI hawi mpiganaji mzuri na mkubwa bila kupigana, Dr A. atadhihirisha hilo.
Ah, we unamdhania Kikwetu au? Yule mwenye PhD ya kuchongwa?yule phd muuza sura kwenye tv kila wik1i?
Hivi kwa nini wataalam ambao si wanafki wanaondolewa udsm? Tunajua labda mkataba wake umeisha lakini umri wake bado unaruhusu sana. Kwa siasa za Tanzania usishangae yakamkuta ya Profesa Baregu!, lakini naamini chuo kinachokuja juu sana Kwa sasa St Agustino hawatamwacha mtaalamu huyu kama udsm watamwacha bingwa huyu wa siasa.
Nakumbuka usemi wake mmoja aliowahi kuusema pengine ulikuwa shubiri kwa ccm, alisema hivi (MIMI NI CCM MFU! Mwanachama asiyelipia kadi!) tafakari maneno haya kabla ya kuchangia.
Umri wa kustaafu ukifika lazima mtu astaafu! kanuni ya utumishi wa umma unaruhusu kwa wahadhiri kupewa mkataba anapostaafu kwa masharti sio lazima kila anayestaafu apewe mkataba. Baadhi ya masharti ni kuwepo na upungufu wa wahadhiri, kutokuwepo kwa mhadhiri mwenye ujuzi alionao mstaafu na mengine. Vilevile, kanuni haziruhusu mtu kundelea kupewa mkataba akishafikisha umri wa zaidi ya miaka 70. Kwa iyo kabla hamjatoa lawama lukuki mngeuliza idara aliyokuwa anaifanyia je walikuwa wanamuhutaji wakanyimwa kupeleka maombi?
hayo maneno kawaeleze magamba wenzio huko,ile phd ya kusoma siyo ya kupewa kama wengineyule phd muuza sura kwenye tv kila wiki?