UDSM-haya magazeti mnapewa bure?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Hivi hakuna magazeti zaidi ya Mzalendo, uhuru na habari leo? Haya ndiyo magazeti wanayoyajaza pale library.
 
Nashanga!
Ina maana UDSM ni taasisi ya Chama Cha Magamba-CCM?Aise ni aibu ati kukuta msomi mzima anasoma Uhuru na Mzalendo vijigazeti vilivojaa umbeya wa kina Nnape na Riz1.Aibu!!!

Someni pia Mwananchi na gazeti dada la The Citizen. Mtazidi kuelimika badala ya kusoma umbeya wa CCM.
 
Kazi ya Mukandara,hamwelewi huyu jamaa?yote yaliyoko pale ni ya ccm,ukilikuta lingine km vile mwananchi ujue mtu kalisoma then kalitupia tu pale kwenye meza,then watu wanaligombania maana mengine yote ni craps
 
Mara ya mwisho kuyasoma hayo magazeti pale library ni enzi zile namaliza chuo nilikuwa natafuta kazi! saizi nilishasahau! Niko na mwananchi, Tanzania daima, mwanahalisi na Raia mwema! Mengine ni ya kenya ndo nasoma soma!
 
Bidhaa nzuri na bora haibaki dukani,magazeti hayo yanaonekana kwa sababu hakuna aliye na time nayo ndiyo maana yanabaki hayo mengine ambayo makini yanagombaniwa.Kwa hali ilivyo hivi sasa chuki ya walalahoi kwa chama tawala yataaza kugomewa hata kwa akina Mamantilie kufungia mandazi.
 
Nashanga!
Ina maana UDSM ni taasisi ya Chama Cha Magamba-CCM?Aise ni aibu ati kukuta msomi mzima anasoma Uhuru na Mzalendo vijigazeti vilivojaa umbeya wa kina Nnape na Riz1.Aibu!!!

Someni pia Mwananchi na gazeti dada la The Citizen. Mtazidi kuelimika badala ya kusoma umbeya wa CCM.

mwananchi?nalo silielewielewi siku hizi!kama limenunuliwa flani hivi,ila inaonekana aliyennua waandishi machangudoa hajatoa dau la kueleweka ndo maana wanauma na kupuliza,..au sababu ya lile karipio kali??ila bado nina kaimani nao kidogo but time will tell
 
Hebu ondoeni expenses za kijinga na makaratasi yenu huko udsm. Nani anashindwa kununua gazeti mwenyewe na kufikiria na akili zake? Wakati wa kumsikiliza mtukufu au mweshimiwa raisi sio generation yetu.
 
Chuo kilishachakachuliwa. Ukiangalia kwenye shelf ya magazeti ya zamani kule east afrikana utakuta magazeti critical kama rai (la ulimwengu), mwananchi na mengine mengi. Bora habari leo na daily news tunaweza kusema ni ya serikali lakini uhuru!!? Gazeti la chama sielewi linafuata nini pale.
 
pale library nlikua nasoma the guardian na daily news but nlishawahi kuuliza mbona mengine kama mwananchi hayapo wakanijibyaliyopo yanatolewa free kwa taasis ya chuo kikuu hence inawezekana haya mengine hayatolowi kama free copy ndo sabab hayapo pale.
 
Enzi zetu walikuwa wanatuletea hata UHURU,sijui wameacha kuleta kwa sasa,kwa maana akina Mkandara ni wanachama wa Gazeti hilo
 
Back
Top Bottom