nashindwa elewa hivi direct cost ni 77,400 au 97,400??mana waliowahi kufika walilipa 97,400 juzi viongozi wakatangaza kua imeshuka tulipe 77,400 kama zamani.Nimelipa 77,400 napeleka risiti naambiwa bado elfu 20...eti hela ya tcu
tunakoelekea tutaambiwa tuchangie hadi hela ya loan board
SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TOZO YA TCU
Ndugu wanaUDSM
Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam inapenda kutoa taarifa kuhusu mkanganyiko uliopo juu ya tozo ya TCU SHILINGI 20,000 kwa lila mwanafunzi. Baada kupata taarifa kuhusu tozo hiyo, DARUSO ilipinga vikali kuhusu tozo hiyo kwa kumuandikia barua katibu mkuu mtendaji wa TCU na kueleza kinagaubaga kuwa hatupo tayari kulipa huku tukiweka sababu kuntu na zenye mashiko na za kisheria.
Katibu mkuu mtendaji wa TCU aliomba kukutana nasi ili tujadiliane juu ya hili na utawala ulitusaidia kutukutanisha na katibu mkuu mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya mnamo tarehe 9 novemba 2015, jumatatu saa sita mchana. Katika kikao hicho kilichokuwa kimehudhuriwa na Makam Mkuu wa Chuo pamoja na Naibu Makam Mkuu wa Chuo -Utawala,mshauri wa wanafunzi, na baadhi ya wanafunzi wasio viongozi. Viongozi wa DARUSO walihoji kuhusu tozo hiyo na kumfanya katibu mkuu mtendaji wa TCU kukubali kusitisha zoezi hilo la kuwatoza wanafunzi hiyo pesa huku tukikubaliana na utawala kuwa waandike tangazo la kusitisha zoezi hilo mara moja.
Katika hali ya kusikitisha, huku tukisubiri tamko la chuo tulilokubaliana litolewe, tarehe 10 novemba tulipata taarifa kuwa TCU wamebadilisha msimamo wao na wameagiza wanafunzi walipe hiyo pesa na ni lazima. Katibu mtendaji yuleyule, aliyekubali kusitisha zoezi zima la hiyo tozo, ndiye aliyetoa maelekezo kwa chuo kiendelee kukusanya hata kwa installment hiyo tozo akidai amepata maelekezo kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya Elimu na mshauri wa Rais, kitu ambacho ni kinyume na makubaliano yetu. Tukumbuke kuwa, chuo kinapokea maelekezo kutoka TCU, hivyo sisi hatuna mgogoro na chuo ila tuna mgogoro na TCU.
DARUSO hatukuunga mkono na hatuwezi kuunga mkono maagizo hayo yenye kila aina ya ukandamizaji na tayari tumechukua hatua madhubuti. Kwanza tunafurahi kuwa wanafunzi wa mwaka wa pili, wa tatu na wa nne mnaweza kujisajili kwa kulipa direct cost ileile, yaani 77,400 kwani baada ya mazungumzo yetu na utawala wa chuo ya tarehe 10 novemba saa 5 asubuhi, tozo ya TCU imetolewa kwenye direct cost na mwanafunzi asiyekuwa nayo atasajiliwa vema huku akidaiwa hiyo ya TCU. Kusema hivi kunamaanisha kuwa, bado msimamo wa TCU ni kuwa twapaswa kulipa hiyo tozo wakati wowote tukiwa nayo na haulazimiki kulipa sasa pamoja na direct cost.
Pia, leo tarehe 11 novemba 2015, uongozi wa DARUSO ulibisha katika ofisi ya katibu mkuu wa wizara ya Elimu ili kuwasilisha malalamiko yetu moja kwa moja na tumefanya mazungumzo na mkuregenzi msaidizi wa Elimu ya juu ambaye ametuelewa vema na kuwasilisha taarifa zetu kwa maandishi. Ni imani yetu kuwa tutafanikiwa kupinga tozo hili ya kidhalimu na kuokoa mabilioni yanayotarajiwa kukusanywa bila kujua matumizi yake na uhalali wake.
Tunawasihi wanafunzi wanaoendelea (continuing students) warudi chuo na kulipa 77,400 kama direct cost pasipo kukwamishwa na 20,000 ya TCU msiyokuwa nayo. Pia, wanafunzi wa mwaka wa kwanza wataendelea kulipa 97,400 kama walivyoanza. Lakini, kwa wote waliolipa pesa hiyo, itarudishwa haraka pindi tutakapomaliza mgogoro wetu na TCU.
IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS DARUSO
KITAPONDA AHADI
RAIS-DARUSO