Udoso ya udom ni ufisadi mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udoso ya udom ni ufisadi mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by LWAKAPISI, Apr 23, 2011.

 1. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chuo kikuu cha Dodoma kitivo cha elimu kuanzia jtano ijayo kinaweza ingia kwenye mgomo mkubwa iwapo uongozi wa chuo utaleta mzaa kama kawaida yake.Mpaka jana kitivo hicho kilikuwa hakijavunja bunge ili kupisha uchaguzi mpya.Bunge la kitivo hicho kilikaa jana saa 10.30jioni ili kupokea ripoti ya fedha.Mara spika alipomkaribisha waziri wa fedha ripoti ilikuwa fupi ikiwa na maneno kuwa "orditors watakamilisha kazi tarehe 15.6.2011".hivyo wabunge wakaanza kuchangia mjadala ambapo walikubaliana kuwa bunge lisivunjwe ili wajue hatma ya milioni 16.8 za "students union"ambazo kwa ushaidi ulio wazi wamekula rais wa kitivo Ruta,spika wa bunge na rais wa shirikisho Baisi.Mwisho wabunge walikubaliana kuwa wao kama wabunge wanakiri kushindwa kazi kwahiyo suala lirudi kwa "wananchi" ili waamue wenyewe.Katika hali ya kushangaza ghafla aliingia rais wa kitivo Ruta ili atoe taarifa ya serikali bungeni,kazi ambayo kikatiba ya UDOSO ni ya waziri mkuu.Wabunge walihoji hilo lakini spika aliendelea kusisitiza kuwa ripoti hiyo lazima aitoe rais na si vingine.Ruta kama kawaida yake alifika mbele na kutoa pumba zake na baadaye akatamka kuvunja bunge.Lakini wakati anatoa tamko hilo wabunge wote walikuwa wameshatoka nje,kavunja mbele ya spika,katibu na mawaziri aliowateua wakiwa sio wabunge.Baada ya pale uliitisha mkutano wa ghafla wa wanachuo wote kuanzia saa 3 usiku na wakakubaliana kuwa jumatano iitishwe college baraza,ili waamue yafuatayo;
  1.kupinga bunge kuvunjwa kihuni
  2.kupinga ada ya kuchukua fomu za urais wa chuo ambayo ni elfu75
  3.kupinga mkurugenzi wa tume ambaye ni mwaka wa3,na katiba inasema awepo kwa mwaka mzima
  4.kutaka kujua muafaka wa hiyo hela iliyopotea pasipo maelezo
  Iwapo utawala utachukulia poa basi mgomo endelevu utaanza mpaka kieleweke.HIYO NDO UDOM CCM WANAYOIMBA KUWA CHUO BORA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
   
Loading...