UDOM: Utumiaji wa Smartphone kwenye mitihani unaharibu elimu

1. Hicho chuo hamna examination regulations??!!
2. External examiners wanafanya nini wakati mwalimu anapo standardize matokea kwa matakwa yake??!!
3. Nyie wanafunzi wa siku hizi ndio hovyo kabisa mnaumia kama hivyo lakini hata department kuitaja unashindwa, ok basi somo tu unashindwa kutaja, hata school inayofanya hayo madudu achilia mbali jina la mwalimu??!!!

Elimu inawakomboaje??!!!
 
Hili swala lipo katika mfumo wrote wa elimu kuanzia secondary sasa. Ni wajibu wa vyombo husika hasa TCU na wizara husika kwenda mbali kutumia technolojia kama kufunga camera.Shida inakuja hatawasimamizi wa mfumo watoto wao vilaza hivyo litaachwa tu!
 
Ufanyaji wa mitihani kwa kutumia smartphone sasa ndio imekuwa fasheni ambapo hata wale wanafunzi wachache ambao walikuwa hawaamini katika cheating za mitihani sasa wamekata tamaa katika kutumia akili zao. Maana wenzao wanaotumia smartphone wanapata course work kubwa na GPA kubwa hivyo inawakatisha tamaa.
Tatizo la smartphone hapa UDOM ni kubwa kiasi kwamba limekuwa likisumbua hata utawala wa chuo na walimu hasa wakati wa kutoa matokeo. Imefikia mahali matokea ya UE hapa Udom hayawezi kutoka mpaka yafanyiwe Standardization. Sababu kubwa ni mbili. Ama wanafunzi wamefaulu kupita kiasi yaani wote wamepata A au wamefeli kupita kiasi.
Kufaulu kupita kiasi.
Kunatokea pale ambapo mwalimu anayefundisha somo hasimamii vizuri wakati wa test hivyo kuwafanya wanafunzi wote kufaulu kupita kiasi na kuwa na course work kubwa. Hii ikienda hadi kwenye mitihani ya mwisho UE usimamiaji ukawa mbovu basi tegemea mwisho wa siku matokea yawe standardized kwa vigezo wanavyo tumia wao, either watakata marks kadhaa kwa kila mwanafunzi au worse ni mwalimu mwenyewe wa somo kupeleka marks za UE alizostandardize kwa kutumia vigezo vyake ambavyo mara nyingi vinaleta manung’uniko kwa wanafunzi ambao havijawa-favor.
Kufeli kupita kiasi.
Kunatokea pale ambapo kwenye mitihani ya UE, kunakuwa na usimamizi mkali kiasi kwamba hata mwanafunzi akiomba kwenda chooni anasindikizwa. Hili likitokea tegemea wanafunzi kufeli sana hata kama walikuwa na course work kubwa.
Scientific Proof: Njoo UDOM si ajabu, ni kawaida sana kumkuta mwanafunzi aliepata Course work ya kati ya 30 hadi 35 ya 40, akirudi September kufanya supplementary ya somo. Haiingii akilini katika rational thinking ya kawaida kwamba mwanafunzi kafanya test 2 na assignment 2 kwa uwezo wake kafikisha marks 35, halafu eti aje kufanya UE ambayo most of the time ni dublicate ya maswali yaleyale ya test, ashindwe kupata marks hata 10 kati ya 100. Hii inaonyesha kuwa kuna uwezekano wakati wa UE mwalimu aliesimamia alibana sana ikashindikana kutumia smartphone.
Kinachonishangaza zaidi ni kuwa huko kwenye cabinet ya kupitisha matokea ambako uongozi wa chuo uliojaa ma-proffesor, hakuna anayeona hili ‘GAP’. Ndio maana nasema matatizo ya Elimu UDOM ni makubwa zaidi ya yanavyoonekana.
Ukweli ni kwamba matatizo mengi ya kielimu yanayoonekana kwa wanafunzi UDOM yana-reflect nature na aina ya walimu wengi tulionao ingawa sio wote(ila ni wengi). System ya kuajili walimu UDOM ina tuhuma nyingi sana, kuna tuhuma kuwa ili uajiriwe UDOM lazima kuwepo na memo unless iwe ni field ambayo haijawa ‘saturated’. Yaani screening ya waombaji wa nafasi za ualimu UDOM imebase kwenye nepotism sana badala ya professionalism, sana sana kwenye baadhi ya college. Hili linasemwa sana.
Evaluation system za walimu hazifanyiwi kazi. Matatizo mengi ya walimu tumeyaandika kwenye zile fomu za evaluation ambazo zinajazwa kila mwaka lakini hakuna hata anaye-bother kuangalia nini wanafunzi wameandika na kufanyia hata uchunguzi wa ukweli wa kile kinachoandikwa. Kuna walimu wako extremely incompetent kwenye baadhi ya masomo kiasi kwamba kila anachoulizwa na wanafunzi darasani anatengeneza defence kwa kuwaambia kuwa “ hilo swali nawaachia kama assignment, mtakuja ku-present wiki ijayo”. Haiwezekani kila swali wanafunzi wanalokuuliza useme ni assignment. On top of that kuna topiki kibao kawaachia mjisomee wenyewe kwa kichaka cha “SELF STUDY”. Yaani akiingia kwenye kipindi mpaka anatoka assignment ziko si chini ya 4. Halafu huyo mwalimu anatoa maswali hay ohayo kwenye test, assignment, tutorial hadi UE unalikuta. Sasa hapo mwanafunzi unam-examine nini? Uelewa? Uwezo wa kumeza?au!!!! Pathetic!
Ni hatari sana kwa maendeleo ya elimu kusipokuwa na effective mechanism in place ya kucheki nini kinaendelea huko madarasani. Kuna walimu ili ufeli mwanafunzi inabidi uondoke chuo usifanye mitihani, kwa kuwa kwenye test anaruhusu smartphone wanafunzi wanatumia mbele yake anawaona. Nafikiri hawa ni wale walimu waliofika hapo walipo kwa staili hiyohiyo.
Kama Uongozi wa chuo ungekuwa serious kufuatilia issue wanafunzi wanazo-raise kwenye zile fomu za evaluation, ungeweza kupata sehemu ya kuanzia kwa baadhi ya issue. Kuna wanafunzi wanarisk kupata favor za kielimu kutoka kwa walimu kwa kuamua kuwa honest na kuandika matatizo ya walimu wao, pamoja na kuwepo kwa risk ya kuweza kuwa disclosed kwa sababu wanaokusanya hizo fomu ni walimu haohao.
Hii tabia ya walimu kufundisha with 100% impunity lazima ifike mwisho ili walimu wanao-underperform na ku-misbehave wawe accountable.

bichwa lako nmeamn lina kazi ya kubeba maskio na ubongo tu ila tayr huna maan yyt hata hapo UDOM. Yaani unaongea rubish mwanzo mwisho,,,
lione lilivyo
 
Huyu mleta mada sijajua kama ni
Mwanafunzi au mfanyakazi ila inaonesha ni wewe mwanafunzi

Kuna vitu vyaweza ikawa kweli na vingine umechukua story za hostel ukaleta hapa, binafs nimemaliza Udom miaka mitatu iliopita.

Nnachojua unapozungumzia lecturer kufanya standardization kwa aonavyo yeye si kweli, maana chuo kina mifumo ya external examiners kupitia mitihani na usahihishaji.

Pili mi nilitoka Udom ( na mwaka wetu ndio tulikiwa wengi haijapata tokea tena mpka leo) lkn usimamizi ulikuwa juu sana na enzi izi tukiwa na wafanyakazi wachache sana, japo enzi izo smartphone zilikuwa bado kuenea lakn tulikuwa na nokia express music, simu iliokuwa kwenye hit ilikiwa inaweza ku Google, lkn kuingia nayo kwenye exam hall/room ilikuwa ngumu

Baadhi ya college, infomatics social sciences na Humanities zilikuwa na miundombinu ya Camera, nilitegemea miaka michache baada ya sisi zile hall kubwa za mitihani zitakuwa zote na Camera, ebu tuambie ukweli hata izo chache kweli hazipo? Mbona hujazizungumzia?

Mada inaweza kuwa na mashiko lakn isiwe valid na ukweli kama ulivotaka kuaminisha japo najua Udom yapo matatizo, but mostly enzi izo zetu tuliokuwa pioneer sio wewe

Sisi tulioitwa caterpillars tukiwaandalia ninyi barabara mpite kiulaini.... So dogo jipange kiasi kiuchunguzi ndio uje
 
mkuu nilikuwepo udom cive baadhi ya mambo ni kweli hasa uwezo mdogo wa walimu kujibu maswali kila ukiuliza wanasema hiyo itakuwa assignment kwa cive walimu hao ni kama mt..o, ley..a, gh.i mpaka unajiuliza walipataje kazi hawa mambo mengine umezungumzia ni ya zamani sasa hayapo.
 
Kuna ukweli,mdogo wangu alikua na supp ya accounts,akamhonga ticha elfu 50,supp ikafutwa,nkashangaa hicho chuo au uozo tu!

Hayo ni maajabu kwani supplementary huwa approved na senate hivyo sioni lecturer ataifutaje baada ya kupitishwa.
 
huyo jamaa anachokiandika ana uhakika? cozwork na UE ni vitu viwil tofauti. System ya pale ni kwamba hata uwe na cozwork ya 40, UEunatakiwa upate kuanzia marks 40 kati ya 100 tofauti na hapo inakuwa technical suplementary
 
Endeleeni kubishana lkn mengi nayaamini kwa kupitia hawa graduates wa udom walio ktk soko la ajira! Ni wepesi mno na hamna kitu
 
Thread imekaa kiushabikizaidi, Udom pana examination regulation iPo very clear smartphone haziruhusiwi NA wapo waliofukuzwa kwa kukiuka taratibu, PIA pana quality assurance unit Na Ina kamati kila college issue Ya evaluation form inakuwa handled Kwa umakini na ripoti zake zinabadiliwa katika board zote kuanzia school, college Hadi senate...wanafunzi wawakilishi wanakuwemo katika vikao hivyo pia, kikaja college kama CIVE kuwa haina wataalam ni kichekesho kwa quality Ya CIVE NI Ya hali ya juu na pana wataalam wazuri sana wakiongozwa professors wakali Kabisa....
 
kuongezea...UDOM Katika mambo Ya mitihani hakuna mzaha mwanafunzi anaanza kufeli toka KWENYE course work...mchujo huo nadhani ni UDOM pekee ,wanafunzi ambaye hajapata 40% Ya course work hafanyi mtihani Hata akifanya hautasahihishwa....na inabidi hiyo Kazi alsome upyaaa mwaka unaofuatia. UDOM SR huenda unachuki na UDOM AU pengine ni mwanafunzi muathirika wa sheria Kali ZA mtihani za UDOM
 
huyo jamaa anachokiandika ana uhakika? cozwork na UE ni vitu viwil tofauti. System ya pale ni kwamba hata uwe na cozwork ya 40, UEunatakiwa upate kuanzia marks 40 kati ya 100 tofauti na hapo inakuwa technical suplementary
Mtu anaongelea UE na analalamika eti mwanafunzi kakosa hata maksi 10 kati ya 100. . . . !!!
 
Hayo ni maajabu kwani supplementary huwa approved na senate hivyo sioni lecturer ataifutaje baada ya kupitishwa.

lecture anaweza kuitoa supp,Kuna Chuo Kuna Chuo Kuna mwalimu amefukuzwa kwa ajili hiyo tens kipo dodoma na Ni cha serikali CB)
 
Back
Top Bottom