KERO Wanafunzi Mwatulole Sekondari (Geita) wakifanya makosa wanatozwa Sh 1,000

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hivi karibuni niliona kuna andiko lipo JamiiForum kuhusu Shule ya Jakaya Kikwete kuwa Wanafunzi wanalazimishwa kununua karanga utoka kwa Walimu wao, nami nikaona nishee hii kero ninayoiona.

Huku kwetu, Kuna Shule ya Sekondari ya Mwatulole, Wanafunzi kuwanaofanya mitihani kile wikiendi wamekuwa wakilazimishwa kutoa Shilingi 200 kwa ajili ya kuchangua kufanya mitihani hiyo.

Mbali na hapo ikitokea Mwanafunzi amekuwa mtoro, anaambiwa atoe kiasi cha Shilingi 1000 ama achague apewe adhabu

Shule hii ambayo ipo Wilaya na Mkoa wa Geita inawezekana wahusika wana lengo zuri la kuwafanya Wanafunzi watimize majukumu yao lakini njia wanayotumia sio nzuri na jambo hilo limekuwa likiwakwaza wazazi wengi.
 
Mimi kuna kipindi nilikuwa Simiyu miaka ya nyuma, mtoto wa shule ya msingi kama asipoenda shule siku moja analipa Sh 100, mwanafunzi wa sekondari kama hajaenda siku moja analipa 500.
 
Ufikage kwenye vikao vya shule uhoji huko

Wawez kuta nimaazimio , huku utaleta Taharuk
 
Mkuu huenda kwenye kikao cha wazazi ndivyo walivyokubaliana.

Hii elimu bure imefanya baadhi ya wazazi walio wengi kijisahau na kutofuatilia mahudhurio ya watoto wao shuleni.

Sasa kama mtoto kaanza utoro mzazi akianza kudaiwa hizo bukubuku na yeye atakaza huko nyumbani.

Walimu kweli wana njaa ila sasa msichukulie kiivyo.
 
Hio nzuri, mzazi lazima utoe pesa, ama ufuatilie nidhamu ya mtoto wako,
Naunga mkono tabia hio, iendelee,
 
Yaani unaufungulia nyuzi shillingi 200 kweli
Elimu mnapewa bure bila hata thumni, kweli ujamaa umeilemaza hii nchi
 
Kama hutaki kulipa hiyo hela zingatia taratibu za Shule.
Mimi nadhani changamoto ingekuwa endapo mtoto hajahudhuria shuleni na mzazi alishatoa taarifa kisha akalazimishwa kutoa hicho kiasi cha pesa, hoja yako ingekuwa na mashiko.
 
Back
Top Bottom