Udom sasa kufundisha kwa mtandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udom sasa kufundisha kwa mtandao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Amon, Mar 30, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  MFUMO wa ufundishaji kwa kutumia Mtandao wa Teknohama, umeingia rasmi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) na kwa sasa, uongozi wa chuo umeanza mchakato wa kuhakikisha kuwa kila mhadhiri, anafundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.

  Hayo yalisemwa juzi na Balozi Juma Mwapachu, alipokuwa akizungumza na wahadhiri wa Udom katika ufunguzi wa mafunzo ya ufundishaji kwa njia ya teknolojia hiyo.

  Balozi Mwapachu ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, alisema dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia na kwamba vyuo vikubwa kama Udom, lazima vibadili mitaala yake na kufundisha kwa njia ya kisasa.

  "Chuo hiki kimebaini kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kutokuwa na uwiano wa kuridhisha katiya walimu na wanafunzi kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi na changamoto hizi azima zifanyiwe kazi ili zisiathiri utoaji wa taaluma,''alisema Balozi Mwapachu.

  Alisema wingi wa wanafunzi katika chuo hicho kikubwa kwa sasa hauendani na idadi ya wahadhiri waliopo na kwamba bila ya kuwa na mbinu mbadala za kuwafundisha, wanafunzi wataachwa nyuma.
  "Udom siyo chuo cha kawaida katika nchi za Afrika Mashariki, lakini pia niseme kuwa siyo vyuo vingi hapa duniani vimeweza kupata bahati ya kukua kwa kasi kubwa ndani ya miaka minne kama Udom, kwa hiyo ukuaji wa chuo hiki lazima uwe wa kisasa na unaokwenda na sayansi na teknolijia," alisema

  Balozi Mwapachu pia aliitaka Serikali kuongeza nguvu katika kukisaidia chuo hasa wa kukipatia vitendea kazi na miundombinu bora.Kwa mujibu wa Balozi Mwapachu, mfumo wa Teknohama unawezesha pia hata wahadhiri kutoka nje ya nchi, kufundisha wakiwa katika nchi zao.Kuhusu miundombinu ya maji, umeme na barabara, alisema lazima iangaliwe vizuri na kutengewa bajeti ya kutosha.

  Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Udom, Prof Idris Kikula, alisema chuo kilikuwa kinakabiliwa na tatizo katika ufundishaji, hatua iliyoulazimisha uongozi kubuni mkakati huo.Kikula alisema hatua ya sasa ni ya kuwajengea uwezo wahadhiri, ili waweze kufanyakazi zao kwa ufanisi mkubwa zaidi.


  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mambo ya JMK na swahiba yake Bill Gates.

  Ahsante Kikwete, tutakukumbuka daima kwa haya mambo adhimu na adimu.
   
 3. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  maneno meeengi.si waliahidi kuwa kila mwanafunzi atakuwa na laptop yake?
   
 4. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Hiyo ahadi imetoka lini mkuu? Mbona mimi sijawahi kuisikia?
   
 5. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Waache siasa na ujeuri wa CCM, chuo hicho kijiendeshe bla maslah ya kisiasa/wanasiasa wahuni!
   
 6. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo Tanzania hii hii? Unless upo abroad, na hata waliopo huko wanafahamu hii ahadi na nyingine nyiiiiiingi uchwara..!
   
 7. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  ... kompyuta ziko wapi?
   
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  mambo mengine huna hata haja ya kujiuliza mkuu cuz hata kwa mtu asiye na akili anajua kabisa kuwa kumpa kila mwanafunzi laptop haiwezekani.
   
 9. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  ..Sina maana ya kompyuta kwa kila mwanafunzi, namaaninsha kwa kila mhadhiri na lab ya ku-accomodate at least 150 students kwa wakati mmoja. Hivi vipo? Hii ni muhimu kabla ya kufikiria ku-broadcast lectures, kitu ambacho ni expensive kuliko hata kununua kompyuta.
  <br/>
  <br/>
  UDSM (UDBS) waliwahi kuwa na degree yenye kolabo na chuo cha nje, ikawalazimu kuifuta baada ya kushindwa gharama za uendeshaji (download rate ilikuwa ndogo sana kiasi kwamba ilikuwa ngumu kupata lectures live). Bongo mipango sio matumizi.
   
Loading...