UDOM na pesa za wanafunzi

UDOM na pesa za wanafunzi

prooo

Member
Joined
Jun 1, 2017
Posts
39
Reaction score
11
Huwa sielewi ni kwanini uongozi wa chuo UDOM, uko hivi huu ni ukatili mkubwa chuo hiki kinao ufanya ilikuwa ni tarehe 24 ya mwezi wa sita ambapo, wanafunzi ambao, pesa zao zilichelewa toka bodi ya mikopo, zilifika chuo na hivyo kupewa wazisaini, mchakato huo ukamilika bila matatizo.

Wanafunzi wakiwa na matumaini ya kuingiziwa hela zao ndani mfupi, inashangaza sana kuskia kwamba mpaka sasa miezi miwili inakamilika bila fedha kuingiziwa kwenye akaunti zao huu ni wizi mkubwa.

Wakiulizwa lini hizo fedha wataingiziwa hujibiwa '' tunashughurikia hivyo subirini ndani ya wiki''.looh! Yaani wiki zimezaa mawiki huu ni urasimu, sharti upingwe kwa nguvu zote wamefanya hivi fika wakijua kuwa, wanafunzi hawawezi fanya chochote, si wapo nyumbani.

Huyu yuko Mbeya yule Arusha watawezaje unganisha kelele zao, ''wacha tuzitumie tunavyotaka, tujizolea mafaida tutawaingizia, wata tufanya nini?"dah! Kwa hili wamewaweza, ni kweli wapo nyumbani kuandamana itakuwa vigumu kwao, lakini ifahamike ipo siku fedha hizi zitawatokea puani, waache waendelelee na kamchezo haka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
UDOM ni sawa na chama cha walimu ujipendekeza na kujiita wasomi chuo kikuu na kumsifia rais aongeze muda kumbe ni mazuzu tu yanafaidi wiki moja ya uchaguzi na kisha miaka 5 ya mateso na hizo kanga wanazopewa.mazuzu tu.


Swissme
 
Back
Top Bottom