UDSM acheni kujisifia mimi nimemaliza udsm miaka michache iliyopi wakati huo kweli kulikua na migomo ya kueleweka ikiongoza na akina waitara mwita, mwita magesa, mtatiro na wengine. Lakini baada ya hapo UDSM wamenywea hasa chini ya uongozi wa prof. Mukandara ambaye amewaweka kiganjani. UDSM hawana ujasiri tena na hata hiyo DARUSO haina sauti tena imeshapunguziwa madaraka. Ndio maana sasa hivi wanafunzi wote wanasajili upya kila semister na kupewa vitambulisho vipya kila semester tofauti na ilivyokua miaka 3 iliyopita ambapo wanafunzi walisajiliwa walipofika mwaka wa kwanza tu na kupewa vitambulisho walivyotakiwa kuvitumia hadi watakapohitimu chuo. Tunajua pia hakuna mwanafunzi wa UDSM anayesajiliwa bila kulipa asilimia anayotakiwa kulipia kwenye tuition fee. Kwa mambo yote haya mbona wana UDSM hawajagoma? Jibu ni simple tu, mkandala amewadhibiti. Hivyo sisi wana udsm tusibaki kujisifia bali tuwaunge mkono wana udom kwa move nzuri waliyoifanya hasa ikizingatiwa kua chuo chao ni kipya na hakikua na uzoefu wa mambo ya migomo. Tuache kufuata mkumbo na kuwalaumu eti wao ni wana ccm, mara tuseme walimchangia JK mil. 1, mara walilaani walkout ya wabunge wa chadema.... Hizi zote ni propaganda za kisiasa zinazoendesha na ccm kusababisha "divide and rule"