UDOM kitivo cha Elimu wapo mbioni kugoma

King junior

Member
Apr 8, 2011
63
12
Wanafunzi wanaosomea ualimu kitivo cha elimu Udom wapo mbioni kugoma.

Tukio limeanza jana baada ya kubandika matangazo ya mkasanyiko wa wanafunzi wote katika moja ya mabwalo ya wanafunzi (BLOCK F). Mnamo saa tatu usiku, wanafunzi zaidi ya elfu moja walikusanyika na kuanza kujadili hoja zenye mashiko na za msingi kuhusiana na kero mbali mbali zinazowakera wanafunzi hao, lakini moja lililopewa kipaumbele zaidi ni kucheleweshewa pesa za kujikimu (BOOM).

Kimsingi utaratibu huu mpya wa utoaji mkopo hadi wanafunzi wasaini umeonekana kuwa kero kwa kuwa uongozi wa chuo unatumia fursa hiyo kuchelewesha pesa hizo kwa wanafunzi.

Kwa taarifa za uhakika cheki ya malipo kutoka bodi ya mkopo ilifika tarehe 17/12/2011, ambapo malipo yalitakiwa kuanza tarehe 20/12/2011 lakini imekuwa tofauti.

Hadi leo nawasilisha mada, pesa haijaingia, huku kukiwa hakuna matumaini kuwa watawaingizia lini ingawa kwa taarifa ya waziri wa mkopo, ni kwamba kuanzia ijumaa ya tarehe 6/01/2012 ndio malipo yanaanza kufanyika.
 
Hahaha, niko hapa uwanjan, mambo yameiva, duh forward mpango mzma, mpaka kieleweke
 
Udom walaini sana hayo mambo hawawezi.biti kidogo tu mgomo kwisha

hii ndio udom ambayo inafuata sheria bwana. Tatizo ni kuwa sheria wanyofuata sijui imeandikwa wapi kwani wao sheria ni kutoona mfanyakazi anapata haki yake kwa wakati ama sawa na wengine walio nje ya chuo hiki ktk taasisi zingine.

Je hili nalo chadema wanahusika kuchelewesha fedha za wanafunzi? Huu uongozi wa udom unafanya kazi ipi hasa ambayo wengi wa wapenda maendeleo wanashangaa muda wote? Haki za wanafunzi zinafinyangwa na wafanyakazi ndo kabisaaaaaaaaaaaa
 
Duh, eti wanasema, wanaprocess majina, ,kwa msimamo huu, tamko limetolewa na kikula kuwa, kuwa wanaanza kuweka leo, ila wanaanza na colege ya afya, mpaka ijumaa wote tutakuwa tushapata, mcjal, najua UDSM mnatudai ,tutawalipa tu'
 
Back
Top Bottom