Mi ni mgeni katika mjadala huu wa hii topic ya udini, lakini haraka haraka naweza sema mtenda akitendewa huhisi kaonewa. Kama ni kweli JK ana udini, basi nenda kaangalie Muhimbili, TRA, na taasisi zingine. Mi nadhani ni bora tuweze kuwa wakweli, watanzania hatutaki kukubali suala la udini kama lipo au halipo. Waingereza wanasema dont give a problem another face if you need to solve it. Angalia Nigeria, wameweza kuona suala la udini lipo na wakaweza kuwa na utaratibu wa migawanyo ya ajira, elimu na kadhalika kwa kufuata uwiano wa kidini. Hii sio kuwa na udini, ni kuwa mkweli na wala si mnafiki, tuache unafiki, udini upo lakini hatukubali, JK alipohutubia bunge wakati fulani alisema uchaguzi umetuachia mpasuko wa udini. Watu wakainuka na kusema ni muongo wengine wakesma atuonyeshe huo uduini na kadhalika. Nilimshangaa sana yule mama Ananelea Nkya, ni msomi lakini hajaelimika, kwani faida ya elimu ni kuweza kutumia katika kutambua masuala hata ya kimazingira, lakini yeye alikurupuka na kusema tofauti na JK. Udini upo na tuingize kwenye katiba jinsi ya kuishi katika hali hii ya dini mbalimbali, ikiwezekana tuweke mgawanyo wa vitu kama ajira, elimu na kadhalika kufuatana na uwiano wa kidini. Ndipo hapa sasa tutataka sensa ya ukweli, ili kuweza kujua idadi za kweli ili migawnyo iende sawa. Hii ndio kisayansi na kibinadamu, hakuna jinsi nyingine ya kutibu udini zaidi ya kuutambua upo, na kuweka utaratibu wa kuishi nao.