Udini wainyemelea CCM?

Tatizo ni kwamba CCM wenyewe ndiyo waanzilishi wa siasa za kupakana matope ya udini na undugu. Walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuichafua CUF eti kwakuwa viongozi wengi ni Waislamu wakakiita chama cha Kiislamu. Wakaja kwa CHADEMA wakadai ni chama cha kikabila na Kikristo. Hawakujua kuwa wanafanya siasa chafu, isiyo na msingi tena inayoweza kuwageukia. Sasa yanayotokea ndiyo haya, ni haki kulisema hili ili wajue ubaya wa siasa za uzushi na ubaguzi.
 

Asante na Mungu akubariki
 

hakika wewe ni mgonjwa wa akili kama si juha basi ni maamuma kweli kweli, ilimu imekuozesha akili
 
'Dhambi ya kubaguana(ubaguzi wa rangi,dini,kabila n.k ni mbaya sana)'..........Mwl.Nyerere
 
Mi nadhani badala ya kubishana nani mkristo,nani muislamu,nani Mu hindu n.k katika chama au serikali tujiulize tu je hao wanaoshika nafasi za uongozi wana sifa za kiuongozi na wana nia njema na watanzania wote???.

Kama mtu alieteuliwa kushika nafasi ya uongozi sehemu fulani ni mchapa kazi,anaejituma kwa dhati kwa ajili ya maendeleo yetu kama wa Tanzania, sidhani kama swala la yeye ni kabila gani au dini gani lina nguvu yeyote hapo...tunataka viongozi bora!!!viongozi wanaoguswa na mateso ya njaa,ujinga,maradhi na matatizo ya msingi yanayoathiri jamii yetu...hivyo kama tunataka kuwahukumu viongozi wetu na tuwahukumu kwa kiwango chao cha utendaji na wala si kwa rangi,urefu,uzuri,jinsia,kabila,au dini...
 

Ni vema ungetoa Orodha ya Viongozi wote badala ya kutumia mfano wa wachache hawa kisha kutoa tuhuma za Udini ndani ya CCM......Hivi watu kama Pius Msekwa,John Chiligati,Amos Makalla,Bernard Membe(Wajumbe wa Skretariat ambayo ndo safu ya uongozi wa juu wa CCM ni waislamu??),au watu kama Martin Shigella,Beno Malissa(UVCCM) n.k ni Waislamu???????.........
 

"Kaburu si lazima awe mtu mweupe au atoke Afrika kusini, mtu yoyote mwenye dhana ya ubaguzi ya rangi, ya udini ,ukabila ni KABURU TU!" Mwl JK Nyerere RIP.
 
hakika wewe ni mgonjwa wa akili kama si juha basi ni maamuma kweli kweli, ilimu imekuozesha akili


Nikawaida yenu mkiishiwa na hoja kuleta mitusi, Ukweli unabaki palepale Historia ya CCM haitobadilika na waanzilishi wanajulikana na nyie msimamo wenu unajulikana.

Mliwatetea wakolono mkaikataa CCM kwakua ilipinga ukoloni, kinachowashangaza ninini waislam kuawa wengi CCM? Jibu hoja wacha matusi!! au unatamani hii historia ifutike?
 

hoja nyingine bana! nachoka kabisa.

kwa hiyo unamaana hao unaosema walianzisha chama kupambana na ukoloni
walifika mahali wakaona bila uongozi wa "yesu" hawawezi fika wanakokwenda
hivyo wakaamua waongozwe na jkn? lol
 
.........

Mliwatetea wakolono mkaikataa CCM kwakua ilipinga ukoloni, kinachowashangaza ninini waislam kuawa wengi CCM? Jibu hoja wacha matusi!! au unatamani hii historia ifutike?

Mimi sipo kwenye ugomvi wenu, wala sitatizwi na idadi ya Waislam au Wakristo katika CCM, CHADEMA wala CUF. Isipokuwa nataka ninyi CCM mjue wazi ubaya wa siasa zenu. CCM ndiyo walioichafua CUF kuwa ni chama cha Waislam, pia wakafanya hivyohivyo kwa CHADEMA. Sasa ndo linawageukia ninyi! Tena maneno yako yanadai CCM ni chama cha Waislam na ikiwa vinginevyo historia itafutika sasa unachukizwa na nini? si ukubaliane na siasa zenu za kibaguzi?
 
Hebu tupe majina ya Kamati ya kuchangisha ya CC M iliyotangazwa juzi!
 


Mimi si mzungumzaji wala si member wa ccm, ninachoongelea hapa ni historia ya ccm/tanu na chanzo cha waislam kuwa wengi ccm, ni historia ambayo haitafutika kirahisi kama wengine hapa jf wanavyoomba kwani ilikuwa fedheha kwa upande ule wa dini fulani.

Na wala ccm sio kuwa wako right kwa kila jambo lakini historia inabaki palepale kwamba waanzilishi ni waislam wakati ule wakiristo wakiwaback up wakoloni, waislam wala ccm hawakuvunjika moyo waliendelea kuwa-encourage wanzao wakiristo wajiunge na kweli walifanikiwa kiasi fulani kwa hiyo isiwemshangao wakiwa wengi kwenye ccm.

Kuhusu CUF, CHADEMA kuwa na udini kama wanavyo dai ccm na watanzania wengine, wanaoelewa historia ya vyama hivyo kuhusisha na udini watatueleza, lakini kwa ccm historia inajieleza kwa nini waislam ni wengi.

View people hapa jf wanatumia idadi ya waislam kama kigezo kuwa ccm kuna udini wanasahau historia ya ccm
 

Tupe majina ya viongozi wote wa CCM. Vinginevyo anaedai udini ndiyo mdini. Kwa kuona hizo nafasi tatu tu unatangaza kuna udini. Msituhabirie nchi kwa tamaa zisizo maana.
 

Nchi imeingiliwa sasa. Ama kweli makaburu ni wengi ulimwenguni. Kuona jina tu linafanana na upande fulani nongwa. Leta orodha mzima ya Uongozi wa CCM na Serikali yake tuijadili.
 
Huwa wanafarijika wanapo ona idadi kubwa ni kutoka upande wa dini wanao iyamini wao, bila kuangalia utendaji kazi wa mteuliwa wa nafasi ya uongozi... Wacheni chuki za kidini zitawaangamiza.
 
Nashangaa sana kuona bado kuna watu wanaotumia dini za wazungu na waarabu kama vigezo vyao vya kufanyia maamuzi na kuzungumzia upendeleo nk.

Hivi kwa mfano hata ingekuwa kweli kuwa mtu kateuliwa kwa sababu ya dini yake, unadhani angeathiri vipi uendeshaji wa nchi? Kwa sababu bado atalazimika kufuata katiba iliyopo ambayo si ya kidini. Uturuki wana karibu asilimia 100% ya raia wao ni waislamu, lakini katiba yao si ya kidini. Brazil karibu 100% ni wakristo tena wakatoliki, lakini katiba yao si ya kidini. Hapo namaanisha kuwa hata ikitokea viongozi wote wa serikali ni waislamu peke yao au wakristo peke yao, nina uhakika hakuna atakayependa nchi iendeshwe kidini maana athari zake zingekuwa mbaya kuliko faida, na hakuna anayeweza kukubali kukata tawi alilokalia, labda awe mwendawazimu.

Kuteua mtu wa dini fulani kushika madaraka si udini, maana rais habanwi na masharti ya dini katika uteuzi. Huyu aliyeleta hii hoja ni mwenye fikra finyu na potofu kabisa.
 


Na hao mababu zako weye waliojiunga na TANU - ikawaje baada ya hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…