BIN BOR
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 1,013
- 407
Anitha ni mkatoliki lakini alipata mchumba mlokole aitwae Marko. Wazazi wa Anitha wakasema hawatakubali Marko amwoe Anitha hadi kwanza abadili dhehebu. Anitha akaanza kumbembeleza Marko kwa taabu maana walokole nao wakakataa kijana wao kuwa mkatoliki. Lakini penzi likakolea na baada ya miezi 3 akakubali kuwa mkatoliki. Marko akaanza mafundisho na siku ya komunio wazazi wa Anitha wakamzawadia gari kama matayarisho ya mume wa binti yao.
Siku moja kama baada ya miezi 2 hivi, Anitha alirudi nyumbani na machozi tele akaanza kugala gala chini.
Wazazi : Anitha vipi tena, umepatwa na masaibu gani?
Anitha : Marko hatanioa tena!
Wazazi : Kwa nini asikuoe wakati anaendelea vizuri na ukatoliki? Amepata komunio na kipaimara kama tulivyotaka! Amekuwa mkatoliki kweli kweli siku hizi.
Anitha : Hilo sasa ndio tatizo wazazi wangu!
Wazazi : Tatizo kivipi wakati amebadili dhehebu ili akuoe wewe?
Anitha : Ameamua kuwa padre........