Udini ni mtaji wa CCM kuendelea kushika dola...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini ni mtaji wa CCM kuendelea kushika dola...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanzaniaist, May 31, 2012.

 1. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanaJF..!

  Kumezuka Suala la UDINI Tanzania...,ambalo liliasisiwa na Mh.Jakaya M.Kikwete alipofungua bunge baada ya uchaguzi mwaka 2010..! ambako sasa hv Watanzania wamekuwa na hofu juu ya mustakabali wa Taifa hili..,huku wengi wakiwa hawajui UDINI umeanzia na kutokea wapi..? ambako CCM wameamua kumtoa kafara Hayati Julius K.Nyerere kama chambo na vugu vugu la kuanzisha udini Tanzania huku wakiwatumia makada wao chini ya mwamvuli wa Waislamu kueneza chuki,propaganda,uwongo na siasa majitaka dhidi ya wakristo..,huku ni na madhumuni yao ni

  1.Kuwagawa Watanzania, na kuwawezesha watanzania kuacha kufuatilia mijadala muhimu kama Katiba mpya, na pia kuwafanya wasifuatilia mijadala inayohusu ufisadi,wizi,rushwa na ubadhirifu wa mali za umma unaotokea serikalini chini ya chama cha CCM..!

  2.kuvunja nguvu ya upinzani...,baada ya kuona CHADEMA inakuja kwa kasi hasa baada ya CCM kujeruhiwa vibaya kwenye uchaguzi 2010 na CHADEMA..,wameamua kueneza Mada kwamba CHADEMA ni chama cha wakristo na hata tumeona kwenye uchaguzi igunga mambo yalivyofanyika..,baada ya CCM kufanikiwa kukipaka CUF matope kwamba ni chama cha kiislamu kwa sera yao ya UDINI sasa wameamua kuhamishia majeshi yao CHADEMA..,baada ya sera yao ya UDINi kufanikiwa kukisarambatisha CUF

  3.Udini unatumiwa na CCM kama kielelezo kwamba serikali inasemwa na kusimangwa sana kuhusu Ufisadi kisa Raisi ni Muislamu..,hata sasa hv kuna watu wanzusha eti Mkulo alihujumiwa kisa eti ni Muislamu...,kwakuwa CCM wameshindwa kutimiza ahadi zao kama Maisha bora kwa kila Mtanzania wameamua kutumia Udini kama sera ya kulinda Uzembe,Ufisadi na Maovu yao...!

  Mwisho..,CCM imeamua sasa kuwatumia Waislamu kwakuwa wengi hawajasoma, wanaishi kwenye umaskini mkubwa, na wengi hawana ajira ili kutimiza matakwa yao..,huku wakiwapa sumu za chuki dhidi ya wakristo na hata juzi makanisa yalichomwa moto ili kuwapa ari waislamu kuingia mitaani na kufanya fujo..! Huku wengi ya waislamu wamesahau CCM waliwapiga waislamu risasi karibia 100 na wengi kufa baada ya udanganyifu wa kura uchaguzi Zanzibar mwaka 2000.., huku pia wamesahau chanzo cha umaskini wao ni serikali ya CCM ambayo imeongoza nchi kwa miaka 51 leo..,ambayo imewatenga na kuwaacha kwenye lindi ya umaskini...,ambako hasa mikoa ya lindi,mtwara na pwani wanapotoka waislamu wengi CCM imewatenga,.kuanzia suala zima la korosho,gesi na hata pia elimu..,leo hii hao hao CCM wanatumia kujenga chuki dhidi ya wakristo na wale waopinga serikali kama adhma yao ya kuendelea kubaki CCM..!

  Jana charles Taylor amehukumia miaka zaidi ya 50 jela,, Nape Nnauye watch out..,siasa na propaganda chafu hazifai
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Well said Mkuu. Hoja imekamilika 100%.
   
 3. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Haya tumekusoma
   
 4. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,314
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Sio ntaji bali ni changamoto ya rais ajaye ndani ya ccm na nje ya ccm kwani aliyepo ni .........mu
  anyway only god can judge the beuty tanzania.
   
 5. m

  makkeys Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said mkuu, hii kitu itakuja kuleta shida sana mbele ya safari
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama kweli wanatumia dini kama mtaji, basi wajitambue kua wamefilisika. Wamefilisika kimawazo na kimantiki. Na kutokana na kufilisika huko ndio maana nchi inaonekana kuwa imekwama. Hakuna kinachoonekana kwenda vema, si kwenye elimu, si kwenye kilimo, si kwenye madini, si kwenye michezo... kila sehemu tumekweama kama nchi
   
Loading...