Shikamoo mkuu Nakapanya, nashangaa sana hii hoja. Ukitazama uchezaji wa MCC unagundua kuwa tatizo lao ni la kiufundi zaidi na sio kisiasa wala bla blah. MCC ni tofauti na timu zingine zote za VPL, hawakurupuki katika utendaji wao na ndio maana ni timu pekee yenye mikataba mikubwa ya biashara mitatu hadi sasa. Kama washabiki hamtalitazama hili kwa jicho kubwa mtajikuta mnafarakanishwa na timu yenu iliyoonesha njia kwa maneno mbofumbofu kama haya.
Bado washabiki wana moyo na timu yao, na bado wachezaji na dawati la ufundi wako vyema!
Amavubi unaweza kuwa sahihi kabisa kwani baada ya yule mama sijui anaitwa mama mwanjelwa wa ccm kusema mbeya city ni timu ya ccm kwani inahudumiwa na manispaa imewakera sana watu wengi waliokuwa wanaitakia mema na michango mbeya city. Ni ukweli usiopingika kuwa ccm haina mashiko kwa baadhi ya watu wengi pale mbeya hasasa wafanya biashara wakubwa wakubwa ambao walikua bega kwa bega kutoa msaada wa wao wa hali na mali ila kilichowakasirisha ni maneno ya kuwa timu ni ya ccm.
Ndio kwanza mechi saba za ligi.nashukuru mkuu,wengi wanatamani sana MCC FC iporomoke,ligi ya msimu huu ina ushindani mkubwa,mkiteleza kidogo tu wenzenu wanatumia nafasi hiyohiyo kuwapiga bao.Mbeya city bado ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri na sisi mashabiki bado tuna imani nayo.
Nakapanya umehama Ndanda?
Ukweli msimu huu Mbeya City imeshindwa kufurukuta, ila bado ina nafasi ligi bado inaendelea, kwako Amavubi sijaona ukieleza ni namna gani UDINI na SIASA zilivyo athiri timu ya Mbeya City.
Nikweli kuwa na taasisi Imara ni muhimu lkn pia wajue hata hiyo Mikataba waliyopata imetokana na Matokeo mazuri ya uwanjani so pamoja na Mipango mingi ya baadae lkn ushindi wa uwanjani ni muhimu piaNdio kwanza mechi saba za ligi.
Ukitazama takwimu za mechi zao kiufundi utagundua kwamba sio wabovu kama ambavyo matokeo ya mwisho yanaweza kukufanya uamini. Nadhani kusuasua kwao kunaweza kuwa kunatokana na uongozi kuweka mkazo mwingi katika kutengeneza mustakabali wa timu zaidi, nasikia wana eneo kwa ajili ya uwanja tayari na mpango wa kiuchumi una sapoti toka kwa wadhamini kadhaa.
Haiwezekani timu iingie mikataba kadhaa ya mamilioni mia kadhaa halafu mtu aje aseme inasuasua, ni kichekesho. MCC wanajenga taasisi imara kwanza, ambayo ni zaidi ya ushindi wa uwanjani.
utakua na imani ya Tomaso wewe
nenda
LAANA YA 'WATUMISHI WA MUNGU' YAITAFUNA MBEYA CITY, - BIN ZUBEIRY
Kuyapeleka haya mambo bega kwa bega sio rahisi sana mkuu, nawarai washabiki wasiupe presha uongozi. MCC wanachohitaji kwa sasa ni kujilinda wasishuke daraja, kisha mengine yatajipanga taratibu timu ikishakuwa ma msingi imara.Nikweli kuwa na taasisi Imara ni muhimu lkn pia wajue hata hiyo Mikataba waliyopata imetokana na Matokeo mazuri ya uwanjani so pamoja na Mipango mingi ya baadae lkn ushindi wa uwanjani ni muhimu pia
Tatizo la Mbeya City ni la kiufundi zaidi labda pamoja na saikolojia. Mtaalamu wa ufundi wa ile timu allikuwa ni yule kocha msaidizi Maka, yeye ni mjuzi sana wa kuibua vipaji, kuwapa hamasa wachezaji na kuwasikiliza shida zao. Kwa mpira wa kibongo yule Maka anajua kufundisha soka lakini pia anajua vyema saikolojia ya wachezaji.
Mwambusi Juma, yeye kafanikiwa kujenga jina zaidi lakini sio fundi kivile, mafanikio yake yamekuwa yakija kwa kushirikiana na Maka...yeye na Maka waliunda benchi nzuri la Ufundi
Wakati Mbeya City inapanda ligi kuu maamuzi ya wadau wengi wa MCC walitaka Maka ndie awe kocha mkuu kutoka na ujuzi, ufundi na shule pia. Lakini mkurugenzi wa jiji wakati huo Idd alimtaka Juma Mwambusi ndio awe kocha mkuu na ikawa hivyo
Bahati nzuri timu ikafanya vyema msimu uliopita, hivyo hakuna aliyekumbuka kuwaza mapungufu ya Juma Mwambusi. Baada ya Juma kupata tuzo ya ukocha bora, ile fungu lote akamgawia Maka <200,000, hapo ndipo Maka akawapa choice MCC, aidha awe kocha mkuu yeye au aondoke. Ngoma ikawa namna ya kumuondoa Mwambusi, wakati wakiwa wanatafakari yule Maka akachukuliwa na timu moja inaitwa Panoni? ya huko Moshi.
Tatizo la Mbeya City kiufupi ni kuondoka kwa Mtaalamu Maka na kubaki kwa Juma Mwambusi peke yake
6.Financially mbeya city wapo vizuri na kila siku wanaingia mikataba minono na makampuni mbalimbali,juzi kati wameingia mkataba na cocacola,wakaingia mkataba na benki ya posta,wanadhaminiwa na Binslum tena kwa pesa ndefu kupitia RB battery sasa hiyo ya kusema financialy hawako fit unaitoa wapi?leta hoja nyingine siyo hii mufilisi.
MKuu pale mtakapo kuja kungundua kuwa mmoja wa mchawi wenu ni huyu jamaa hakika mtakuwa mmechekewa, kama hamjuhi kawaulizeni Coastal union.
Huyu jamaa ni nuksi.