Udikteta Wa Magufuli uko hata kwenye kauli

Udikteta Wa Magufuli uko hata kwenye kauli

Hewa mkaa

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2012
Posts
748
Reaction score
386
Nimejaribu kufuatilia mikutano ya Dr. JPM. Kauli zake zinachonganisha watu na serikali yao. Haiwezekani kwamba mambo ya serikali iliyopita yote ni hovyo. Uhadimu wa madawa, elimu mbovu, watendaji wabovu serikalini, uchumi mbovu usio na viwanda, kodi kubwa n.k yamekuwa mambo anayonadi kila kukucha. MTU kama huyu akiingia ikulu ataburuza watu ili kujaribu kama anayotaka yatatimia kwa gharama yoyote. Huo ndo udikteta. Hata kauli zake anazotoa ni za ubabe na udikteta
 
Haupendi ukweli unataka kudanganywa na kupepewa haipo hiyo kama tunataka kutajirika
 
Keshasema ataendesha nchi kidikteta...
Unataka nn mkuu?
 
Fools are wise until they speak-Randle Cotgrave

Ulitaka afanye nini ili asionekane dikteta?
 
suala la udikteta kwa maghufuli linaonekana dhahiri kabisa. nina wasiwasi kama maghufuli atashinda tutegemee nchi kuandamwa na migono mingi sana.
 
suala la udikteta kwa maghufuli linaonekana dhahiri kabisa. nina wasiwasi kama maghufuli atashinda tutegemee nchi kuandamwa na migono mingi sana.
Kumbe unafahamu kama kuna uwezekano wa Magufuli kushinda!

Kwa hiyo unapingana na kauli ya mgombea wako anayesema ushindi ni saa nne za asubuhi?

Kumbe unafahamu kama kauli zake niza kilaghai.
 
awe hasiwe sisi ni lowassa, kwanza hana hayo mabavu ya kufurukuta kweny mfumo
Unafahamu maana ya mfumo au ndiyo yaleyale ya bendera fuata upepo.

Wewe unachagua ambaye yuko kwenye mfumo gani? Mfumo wa Lowassa na kundi lake?
 
Hampendi udictatator mnapenda mahaba tu! Uvivu na upopobawa! Hapa kazi tu hizo itikadi za lowassa ni za kivivu
 
suala la udikteta kwa maghufuli linaonekana dhahiri kabisa. nina wasiwasi kama maghufuli atashinda tutegemee nchi kuandamwa na migono mingi sana.
Si nyie ndio mlisema eti Kikwete dhaifu anachekacheka tu. Sasa mnalialia nini. Kwani mlijipangaje? Tulieni mnyolewe.
 
Back
Top Bottom