The Bliss
JF-Expert Member
- Oct 16, 2021
- 213
- 435
Yawezekana viongozi wetu wa kisiasa wanashindwa kutatua matatizo yanayowahusu wananchi kwa sababu mbili: Moja, hawana uwezo mzuri wa kufikiri na kutatua matatizo (Upeo wa akili zao ni mdogo).
Mbili, hawataki kutatua matatizo kwasababu matatizo ya wananchi ni fursa ya wao kuendelea kupata nafasi za uongozi ( Ulafi wa madaraka).
Kwa kuanza na sababu ya kwanza. Ni ukweli usiopingika kwamba viongozi wengi wa kiafrika hawako smart in problem solving. Wengi wao hawana uwezo mzuri wa kubuni mbinu za kuondoa tatizo badala yake huwa wanaondoa tatizo dogo kwa kuleta tatizo kubwa. Rejea ongezeko la tozo na mfumko wa bei Tanzania. Viongozi wengi hawana sifa za uongozi bali wanabebwa na historia za wazazi, ndugu , jamaa na marafiki ambao kipindi cha nyuma walibahatika kushika nafasi za uongozi katika nchi lakini kiuhalisia hawana sifa za uongozi na utendaji ambao unaweza kulitoa taifa hili sehemu ya chini na kwenda juu. Pia elimu za viongozi wengi wa kisiasa zimekuwa za kutiliwa mashaka na jamii kutokana na jinsi zilivyopatikana au kwasababu wanashindwa kutafsiri elimu zao katika mazingira halisi. Rejea baadhi ya PhD za viongozi wengi wa Tanzania.
Viongozi wengi hawana muda wa kujua matatizo halisi ya wananchi wao kwasababu ya historia za makuzi yao kwasababu wengi wamekulia kwenye maisha safi yasiyokuwa na shida kabisa. Kwahiyo kuonja maisha ya mtu anayekunywa maji katika bwawa moja na Ng'ombe inakuwa ngumu sana, kuonja maisha ya mtu anaesoma katika shule yenye walimu wawili au wanne haimuingii akilini, kuonja maisha ya watu wanaokosa huduma za afya hawezi kuelewa kwa uhalisia, kuonja maisha ya vitu kupanda bei hawezi kuonja uhalisia kwasababu hata vocha za mawasiliano wanapewa na serikali, gari za kutembelea pamoja na posho za kusinzia na kupiga makofi bado wanazipata. Hivyo basi inakuwa ngumu kukua kiakili na kupata mbinu na muamko wa kutatua matatizo ya wananchi. Rehejea maamuzi ya mawaziri na baadhi ya watendaji wa serikali.
Najaribu kufikiria pia katika mlengo wa nadharia ya pili kwamba endapo viongozi wetu hasa wa kisiasa wakitatua matatizo ya uhaba wa maji safi na salama, umeme wa uhakika, huduma za afya, miundombinu za barabara, elimu na usalama wa raia na mali zao, ajira hivi watajinadi kufanya nini wakati wa kampeni za kuomba nafasi za uongozi? Jibu ni kwamba hawatakuwa na chakuongea. Kwasababu wananchi watakuwa hawahitaji tena kutatuliwa shida za ugumu wa maisha bali wanahitaji kuambiwa kuhusu advanced economy, technology and world domination kitu ambacho viongozi wengi wa kiafrika hawawezi kukifanya. Rejea issue za PayPal, crypto currency, price za internet bundles.
Viongozi wetu wa kiafrika wamewekeza kwenye matatizo ya wananchi wao kama mitaji yao ya kisiasa hivyo basi kuondoa changamoto za wananchi katika jamii zao ni kujikosesha nafasi za uongozi kwasababu hawana cha kutoa katika jamii zaidi ya kuahidi kutatua matatizo yaleyale kila mwaka.
Hitimisho: Ukitaka kumtawala kwa urahisi binadamu basi mnyime elimu bora. Ukitaka binadamu akutii basi mfanye awe mnyonge kupitia njaa kisha mpe chakula kidogo kidogo.