Udhaifu wa mapendekezo ya CHADEMA kuhusu Katiba Mpya

MenukaJr

Member
Apr 24, 2021
50
128
Katika chapisho la kwanza nilieleza namna mapendekezo ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA yasivyoweza kutupatia Katiba mpya, bora na shirikishi kama alivyosema. Kwa ajili ya kumbukumbu, Freeman Mbowe alisema kuwa Rais aunde Tume huru ya Katiba. Tukamwambia haiwezekani, swala la Tume ya Katiba na muundo wake tayari limeelezwa katika sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83 ya mwaka 2012. Kwa hiyo, muundo ni uleule. Wembe ni uleule kwa mujibu wa sheria.

Freeman akasema tena kuwa mchakato wa Katiba mpya uanzie katika hatua ya rasimu ya Jaji wa Warioba kisha rasimu hiyo ilinganishwe na Katiba inayopendekezwa halafu katika kupunguza tofauti, iundwe rasimu mpya itakayopelekwa katika Bunge la Katiba. Tukamwambia tena hilo haliwezekani, mchakato wa Katiba una sheria yake ambayo imeweka hatua za kupitia. Tukamwambia katika hatua zote, hakuna hatua hiyo anayotaka. Sheria inataka baada ya rasimu kutoka katika mabaraza ya Katiba (hiyo ya Warioba) hatua inayofuata ni Bunge Maalum la Katiba, no more. Tukamshauri Freeman asome sheria ya mabadiliko ya Katiba aache kubwabwaja mambo yasiyokuwepo katika jambo kubwa hili. Ni aibu Mwenyekiti wa Chama Taifa kufikiriwa haijui sheria ya madai anayodai.

Baada ya kuonesha udhaifu wa mapendekezo ya Freeman Mbowe, leo nitaonesha udhaifu wa John Mnyika-Katibu Mkuu wake. Ni kama Chama chote kinaongozwa na watu wasiofahamu lolote kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba halafu wanawadanganya Watanzania kuwa watawapatia Katiba bora. Kwa kifupi, Katiba mpya bora haiwezi kupatikana na watu wasioifahamu Katiba iloyopo. Naomba nisizungumzie elimu zao maana wote zina utata, mmoja mwaka wa kwanza UDSM mwingine form six Ihungo. Wote hawakufika mwisho mzuri!!

John Mnyika amesema sheria ya mabadiliko ya Katiba ifanyiwe marekebisho ili kukidhi mahitaji ya kutoa Katiba mpya iliyo bora. Kwa sababu John Mnyika haijui sheria ya mabadiliko ya Katiba, akazigawa sheria hizo katika makundi mawili. Akasema sheria moja ni ya mwaka 2012 yenye kusema kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi halafu nyingine ni sheria ya mwaka 2013 inayosema kuwa Katiba inayopendekezwa isipopigiwa kura za NDIYO za kutosha, Katiba iliyopo itaendelea. Rejea hotuba yake wakati akifunga kongamano la BAVICHA juu ya madai ya Katiba mpya. John Mnyika hajui lolote kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba kama alivyo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe. Mwambieni Mnyika akasome sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83 ya mwaka 2012 vifungu vya 31-36. Siyo sheria ya mwaka 2013 kama alivyosema yeye, hatuna sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Vilaza wakubwa hawa!!

Kwa kujibu hoja zake;
1. Ushauri wake ukichukuliwa kama ulivyo kwamba tubadilishe sheria ya mabadiliko ya Katiba ili TUME ya uchaguzi isisimamie kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa, bado hatuwezi kupata Katiba anayotaka kwa sababu wenye kubadilisha sheria ni Bunge la JMT ambalo ndilo lenye Katiba inayopendekezwa wanayoikataa. Kwa sasa lote ni Bunge la CCM tusiotaka Katiba mpya hadi kwanza watu wamejifunza kuitii iliyopo. Kwa hiyo tukiamua kuchukua ushauri wake wa kubadilisha sheria, tunaweza kubadilisha sheria tukatengeneza Tume ya CCM kusimamia kura ya maoni na hakuna wa kutuzuia wala cha kutufanya tukairudisha hii hii katika jalada jipya. Udhaifu wa pendekezo hili ni kwamba, linatoka CCM lilikoharibiwa na kurudishwa CCM kusahihishwa.

Ushauri: Tuwafundishe watu KUTII Katiba iloyopo kisha tufikirie Katiba nyingine ama watu watavunja Katiba iliyopo kupata nyingine. Hatari zaidi inaweza kuvunjwa Katiba mbovu ikatengenezwa Katiba mbovu zaidi.

2. Kura ya NDIYO au HAPANA. Mnyika anasema tubadilishe sheria ya mabadiliko ya uchaguzi ili kuondoa sharti la Katiba inayopendekezwa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana na kwamba isipopigiwa kura ya ndiyo iloyopo itaendelea kutumika. Anataka utaratibu uwe, wananchi wapige kura za ndiyo katika mambo wanayokubaliana nayo na hapana katika mambo yasiyokubalika kisha yasiyokubalika yarekebishwe hadi yakubalike kwa kura ya ndiyo. Mnyika haelewi dhana ya wengi wape wachache wasikilizwe. Wanataka demokrasia wakati hawaijui demokrasia, vilaza hawa.

Hata kama tukichukua ushauri wake, Je, ni nani wa kutengeneza sheria hiyo ya mzunguko wa nenda rudi nenda rudi? Je, ni hili Bunge la JMT la CCM kwa asilimia 99 lenye Katiba inayopendekezwa na kukataliwa? Bila shaka pendekezo hili nalo haliwezekani. Mapendekezo ya CHADEMA yote ni mfu, hayapo, hayawezekani kwa usahihi kwa sababu hayakuandaliwa kwa makini na utulivu. Ni upotevu wa muda, ni sufuri.

Ushauri: Tuwafundishe kwanza watu UTII wa Katiba ili wakipelekewa marekebisho ya sheria watende sawa na Katiba. Bila kufanya hivyo watu watavunja sheria kurekebisha sheria halafu tutakosa sheria yenye kutupatia Katiba bora. Watanzania hawana mahitaji na Katiba mpya kwa sasa bali UTII wa Katiba iliyopo.Tuishi humo!

MenukaJr,
#FikraHuru.
 
Katiba ya 1977 ilitokana na mapendekezo ya Wana CCM. Nchi inahitaji katiba mpya.
 
Katiba Mpya sio agenda ya CHADEMA wala Mbowe tu, ni takwa la WANANCHI wote, wala sio hisani ya Rais.
 
Mbona tulipokuwa na katiba ya kwanza miaka ya 1960's hatukuanza na kuwafundisha watu utii wa katiba?
Hoja yako haina mashiko.
Hawa jamaa ubongo wao uko sehemu nyingine kabisa siyo kichwani. Mtu anaandika maneno meeeengi mantiki hakuna. Ni kama Evarist Chahali kule you tube alikuwa anasema eti kama watu wanashindwa kuwa waaminifu kwenye ndoa, hata katiba mpya ikija haitasaidia 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Anza kuwafundisha viongozi wako kwenye chama kuitii Katiba iliyopo, wajue haki za raia ni wajibu wao, wakati wengine tukiwaamsha wananchi waujue umuhimu wa Katiba Mpya.
 
Katika chapisho la kwanza nilieleza namna mapendekezo ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA yasivyoweza kutupatia Katiba mpya, bora na shirikishi kama alivyosema. Kwa ajili ya kumbukumbu, Freeman Mbowe alisema kuwa Rais aunde Tume huru ya Katiba. Tukamwambia haiwezekani, swala la Tume ya Katiba na muundo wake tayari limeelezwa katika sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83 ya mwaka 2012. Kwa hiyo, muundo ni uleule. Wembe ni uleule kwa mujibu wa sheria.

Freeman akasema tena kuwa mchakato wa Katiba mpya uanzie katika hatua ya rasimu ya Jaji wa Warioba kisha rasimu hiyo ilinganishwe na Katiba inayopendekezwa halafu katika kupunguza tofauti, iundwe rasimu mpya itakayopelekwa katika Bunge la Katiba. Tukamwambia tena hilo haliwezekani, mchakato wa Katiba una sheria yake ambayo imeweka hatua za kupitia. Tukamwambia katika hatua zote, hakuna hatua hiyo anayotaka. Sheria inataka baada ya rasimu kutoka katika mabaraza ya Katiba (hiyo ya Warioba) hatua inayofuata ni Bunge Maalum la Katiba, no more. Tukamshauri Freeman asome sheria ya mabadiliko ya Katiba aache kubwabwaja mambo yasiyokuwepo katika jambo kubwa hili. Ni aibu Mwenyekiti wa Chama Taifa kufikiriwa haijui sheria ya madai anayodai.

Baada ya kuonesha udhaifu wa mapendekezo ya Freeman Mbowe, leo nitaonesha udhaifu wa John Mnyika-Katibu Mkuu wake. Ni kama Chama chote kinaongozwa na watu wasiofahamu lolote kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba halafu wanawadanganya Watanzania kuwa watawapatia Katiba bora. Kwa kifupi, Katiba mpya bora haiwezi kupatikana na watu wasioifahamu Katiba iloyopo. Naomba nisizungumzie elimu zao maana wote zina utata, mmoja mwaka wa kwanza UDSM mwingine form six Ihungo. Wote hawakufika mwisho mzuri!!

John Mnyika amesema sheria ya mabadiliko ya Katiba ifanyiwe marekebisho ili kukidhi mahitaji ya kutoa Katiba mpya iliyo bora. Kwa sababu John Mnyika haijui sheria ya mabadiliko ya Katiba, akazigawa sheria hizo katika makundi mawili. Akasema sheria moja ni ya mwaka 2012 yenye kusema kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi halafu nyingine ni sheria ya mwaka 2013 inayosema kuwa Katiba inayopendekezwa isipopigiwa kura za NDIYO za kutosha, Katiba iliyopo itaendelea. Rejea hotuba yake wakati akifunga kongamano la BAVICHA juu ya madai ya Katiba mpya. John Mnyika hajui lolote kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba kama alivyo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe. Mwambieni Mnyika akasome sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83 ya mwaka 2012 vifungu vya 31-36. Siyo sheria ya mwaka 2013 kama alivyosema yeye, hatuna sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Vilaza wakubwa hawa!!

Kwa kujibu hoja zake;
1. Ushauri wake ukichukuliwa kama ulivyo kwamba tubadilishe sheria ya mabadiliko ya Katiba ili TUME ya uchaguzi isisimamie kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa, bado hatuwezi kupata Katiba anayotaka kwa sababu wenye kubadilisha sheria ni Bunge la JMT ambalo ndilo lenye Katiba inayopendekezwa wanayoikataa. Kwa sasa lote ni Bunge la CCM tusiotaka Katiba mpya hadi kwanza watu wamejifunza kuitii iliyopo. Kwa hiyo tukiamua kuchukua ushauri wake wa kubadilisha sheria, tunaweza kubadilisha sheria tukatengeneza Tume ya CCM kusimamia kura ya maoni na hakuna wa kutuzuia wala cha kutufanya tukairudisha hii hii katika jalada jipya. Udhaifu wa pendekezo hili ni kwamba, linatoka CCM lilikoharibiwa na kurudishwa CCM kusahihishwa.

Ushauri: Tuwafundishe watu KUTII Katiba iloyopo kisha tufikirie Katiba nyingine ama watu watavunja Katiba iliyopo kupata nyingine. Hatari zaidi inaweza kuvunjwa Katiba mbovu ikatengenezwa Katiba mbovu zaidi.

2. Kura ya NDIYO au HAPANA. Mnyika anasema tubadilishe sheria ya mabadiliko ya uchaguzi ili kuondoa sharti la Katiba inayopendekezwa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana na kwamba isipopigiwa kura ya ndiyo iloyopo itaendelea kutumika. Anataka utaratibu uwe, wananchi wapige kura za ndiyo katika mambo wanayokubaliana nayo na hapana katika mambo yasiyokubalika kisha yasiyokubalika yarekebishwe hadi yakubalike kwa kura ya ndiyo. Mnyika haelewi dhana ya wengi wape wachache wasikilizwe. Wanataka demokrasia wakati hawaijui demokrasia, vilaza hawa.

Hata kama tukichukua ushauri wake, Je, ni nani wa kutengeneza sheria hiyo ya mzunguko wa nenda rudi nenda rudi? Je, ni hili Bunge la JMT la CCM kwa asilimia 99 lenye Katiba inayopendekezwa na kukataliwa? Bila shaka pendekezo hili nalo haliwezekani. Mapendekezo ya CHADEMA yote ni mfu, hayapo, hayawezekani kwa usahihi kwa sababu hayakuandaliwa kwa makini na utulivu. Ni upotevu wa muda, ni sufuri.

Ushauri: Tuwafundishe kwanza watu UTII wa Katiba ili wakipelekewa marekebisho ya sheria watende sawa na Katiba. Bila kufanya hivyo watu watavunja sheria kurekebisha sheria halafu tutakosa sheria yenye kutupatia Katiba bora. Watanzania hawana mahitaji na Katiba mpya kwa sasa bali UTII wa Katiba iliyopo.Tuishi humo!

MenukaJr,
#FikraHuru.
Kwanza ni wazi kuwa sio CDM pekee wanaotaka katiba mpya.
Pili ni kweli mabadiliko ya katiba huongozwa na sheria. Swali ni sheria ipi? Tunajua kuna sheria nzuri na sheria mbaya. Kama sheria ni mbaya inaweza kubadilishwa hata kuitupilia mbali na kuandika mpya. Na hapa ndipo maridhiano yanapoingia. Kama kuna nia yote yawezekana. Kama ni ujanja ujanja hatufiki mbali tutaingia kwenye mkwamo mwingine. Hivyo mawazo ya Mbowe na Mnyika sijaona kama yanaonyesha kutokujua sheria.
 
Back
Top Bottom