Udhaifu, Maoni na Mapendekezo kwa Tume ya Ajira "PSRS"

Mshale_OG

Member
Sep 21, 2022
8
5
Kwa vijana wengi, hii kitu / tume ya ajira imekua kichefu chefu sana na yanayoendelea yanakatisha tamaa mno.

1. Udhaifu

Tume inafanya kazi manual, yaani chaguzi za watahiniwa / wasahili unafanyawa na unaamuliwa na watu. Hii husababisha / huweza sababisha kuwepo kwa upendeleo, kuacha mtu mwenye vigezo stahiki, kuchagua mtu asiye na vigezo n.k

Tume hii haina namba ya simu ya uhakika yani ni wababaishaji, ukiingia portal.ajira.go.tz kuna namba za simu 4 yani 2 za "helpdesk", 2 nyingine za "malalamiko" ila inayopokelewa ni 1 ambayo ni "+255784398259 Helpdesk" na mpokeaji hajui kujibu hoja, na hana msaada kwa kifupi na hajielewi.

Barua pepe kwa kawaida pia hua hazijibiwi kabisaaaa

Interview nyingi hua hazifuati ratiba na muda uliopangwa, unaweza kufika asubuhi mfano saa 12.30 asb na usahili ulipangwa kufanyika saa 1.00 asb na mtihani ukafanyika saa 5 au 6 Mchana.

Wasimamizi wengi wapo kama "robot", hawawezi kujiongeza kabisaa. Mtahiniwa kuitwa kwaajili ya usahili inamaanisha tayari amekidhi vigezo kadha wa kadha ktk kada husika hivyo kuja kushindanishwa na wengine, changamoto nyingi zipo kwa wale wenye dual degrees i.e Electrical & Electronics , Electronics & Telecommunications n.k. Hawa mara nyingi huwekwa pembeni kusubiri maamuzi ya Msimamizi mkuu! Tena kwa kuandikwa majina pembeni kama wamebaguliwa / wamelazimishwa kuwakubali.

Kupachikia majibu / marks za watu wengine kwa kigezo cha undugu, urafiki au connection. Mara nyingi hawa huwa hawatoboi kwenye Oral interview. Ila kama alijipanga au alipendekezwa na wakubwa basiiii anapitishwa !


2. Maoni na Mapendekezo

Matumizi ya tehama ktk mchakato wote wa uchaguzi na uteuzi wa watahiniwa. Hii itasaidia kupata watu wengi sahihi kwa muda mfupi. Hii itapunguza gharama kubwa "pesa na muda" hili linawezekana ila ni rahisi sana kuhujumiwa kwasababu sio rafiki sanaa kwenu na inawezekana ikawa tishio kwasababu hutopata unayemtaka wewe.

Wekeni call center yenye watu makini wenye uweledi na busara!

Kuwepo na standard katika mitihani ya Utumishi. Maswali 4 hayatoshi ku-justify mtahiniwa, hio ni kubahatisha! angalau maswali 50 hadi 100 katika kada husika.

Kuwepo na option ya kufuta Account (Delete Account) kwenye ajira portal profile.

Kuwepo na option au dirisha dogo la Taasisi kufanya Headhunting kupitia PSRS na kuvuta wanaojitolea ktk taasisi mbali mbali.

Nawasilisha.
 
Mkuu endelea kuapply usikate tamaa ipo siku Mungu atabariki juhudi zako.
Shukran, ingawa mimi ni mstaafu (PhD) na PSRS ina upuuzi mwingi mno, hawaambiliki hopefully vijana wataamka ingawa wengi ni waoga but message sent!
 
Back
Top Bottom