Udhaifu Mahakama zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhaifu Mahakama zetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Aug 24, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wadau, nimekutana habari kutoka The Guardian 22nd August:

  Nimeona mambo matatu yanayonifanya niwe na wasiwasi na utendaji wa mahakama zetu:
  Kuna ulazima gani wa kutembelea magerezani kesi? Kesi ziko magerazani au mahakamani? Au hakuna kumbukumbu za kesi zote kwenye mahakama husika? Huu ama ni utendaji mbovu au matumizi yasiyo lazima ya fedha za walipa kodi, au kumepatika ufadhili kwa hivyo panatafutwa sababu ya kutumia esa hizo.

  Katika hilo hilo, inaonesha kuna mrundikano wa kesi za waiba kuku na kipande cha muhogo, bila ya kujali kuwa kuwaweka ndani watu hao sio tu kunawanyima uhuru wao na familia zao, bali kuitia hasara serikali.

  Hii ni kusema kuwa katika nchi yetu "mtu yeyote ni mkosa mpaka atakao thibitisha vyenginevyo. Mimi nikienda polisi na kusema tu kuwa fulani kaniibia, ninasekwa ndani kwanza ndio baadaye kunafanywa uchunguzi.

  Ina maana kama pesa hazjapatikana pesa, kesi zitaendelea kusota mahakamani.
   
Loading...