Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Wakuu.
Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) wamekiri kupitia kwa aliyekuwa moderator wa mdahalo ambaye ni mhadhiri wa chuo hicho kuwa mdahalo walio uandaa kuhusu mchakato wa katiba ulihujumiwa na CCM kwa kukodi vijana kutoka mitaani kuja chuo kikuu kushangilia na kupiga makofi.
Mdahalo ule uliharibiwa na CCM ikiwa ni pamoja na kuwapendelea makada wa chama hicho kutoa michango yao kuliko hata wanataluma wabobezi walio hudhuria kongamano lile na hivyo nafasi ya UDASA kupokwa na CCM mpango ambao ulipangwa mahususi kujenga taswira kuwa jumuiya ya chuo kikuu iko pamoja na ccm na hivyo wanakubaliana nao kwenye mchakato wa katiba mpya.
Tafsiri ya makala hiyo...
Kwenye bandiko hapo chini jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDASA) kupitia kwa katibu wake Bwana Faraja Kristomus ameliambia gazeti la "The Citizen" kuwa makada wa CCM waliuhujumu mdahalo wao kwa kuwaingiza/kupenyeza vijana wa kukodi (waliolipwa) kutoka mtaani ili kuharibu michango ya baadhi ya washiriki.
Bwana Faraja amekiri kwa kusema ni kuwa "...Ni kweli mkutano ule wa mdahalo ulivamiwa na vijana ambao hawakualikwa ambao walilalamikiwa kuwa walikodiwa na wanasiasa..."
Ufafanuzi wa Bwana Faraja unakuja baada ya kusambaa kwa habari kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na kilicho gubika tukio la jumapili lililotawala na kuzomea, vurugu za kushangilia na hatimae kutoka nje.
UDASA ililalamikiwa kama chambo cha kukisaidia chama tawala kusonga na ajenda yake ya muundo wa muungano wa serikali mbili kinyume na matakwa ya umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA).
Bwana Faraja anasema kwamba "...jumuiya yao haikujua mipango ya CCM mapema na walikuja kujua kabla ya kuanza kwa mdahalo ulio jadili nini kifanyike ili nchi ipate katiba yake mpya...". Mawaziri Stephen Wassira, Prof Anna Tibaijuka na William Lukuvi pamoja na Mwigulu Nchemba walihudhuria na kuzungumza.
"...Tulishtushwa na kundi la vijana walioshushwa kwenye mabasi ya UDA kwenye eneo...waliingia ukumbi wa Nkurumah mapema saa nne asubuhi..." alidhibitisha pia kuwa, vijana walio shushwa walionekana wakigawana fedha walizopewa.
Mheshimiwa Lukuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi na miongoni mwa vigogo wa CCM walio hudhuria alipo ulizwa akasema "...hakujua kuwa watu walisombwa au kukodiwa ili wahudhurie.."
"...niikuwa Dodoma kuhudhuria vikao nilipo alikwa na wahadhiri kuhudhuria mdahalo, sikupokea mualiko wowote kutoka CCM na kwa kweli nilishangaa kukuta wanachama wa CCM wamehudhuria..." amesema.
Ripoti zina sema vijana waliokodiwa kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es salaam walilipwa kati ya shilingi elfu 50 na kada wa umoja wa vijana wa chama hicho tawala.
Kazi kubwa ilikuwa kuzomea yoyote aliyetoa mchango kuunga mkono UKAWA kuhusu katiba mpya, kikundi hicho kilipaswa kushangilia hoja za mjadala kutoka kwa viongozi wa CCM waliotoa maoni yao kwenye mdahalo huo.
--Nimejaribu kuitafsiri makala hiyo kwa kiswahili ili kuzidi kukazimia maarifa na kuonyesha obwe (vacuum) lililoko kwenye jumuiya iliyoheshimika na kuwa kitovu cha fikra mbadala enzi hizo tungali makinda.
Mtakumbuka siku ile ile mara tu baada ya mdahalo niliweka status hapahapa kulaani mdahalo ule ambao UDASA walitumika kama mhuri wa CCM huku wanazuoni kama Dr Lwaitama na Prof Sheriff uwepo wao ukionewa kinyaa.
Jisomee yaliyo andikwa kwenye makala hiyo hapo chini.