Udanganyifu wa kampuni ya madini (WAANIKWA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udanganyifu wa kampuni ya madini (WAANIKWA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by QUALITY, Sep 13, 2012.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDANGANYIFU ULIOBAINIKA KUFANYWA NA KAMPUNI YAUCHIMBAJI IITWAYO AUREUS LIMITED AMBAYO ZAMANI ILIKUWA IKIJULIKANA KAMAMINEXTECH


  Utangulizi

  Kampuni ya Aureus Limited(zamani ilikuwa ikiitwa Mineral Extraction Technologies Ltd (Minextech)) nikampuni inayojishughulisha na uchenjuaji wa marudio ya dhahabu ya wachimbajiwadogo (gold tailings) kwa kutumia teknolojia ya kemikali ya sayanaidi (vatleaching).

  Kampuni hiyo inamilikileseni ya uchimbaji madini ML 384/2009. Mitambo ya uchenjuaji ya kampuni hiyoipo katika maeneo mawili, mtambo wa kwanza upo katika Kijiji cha NyarugusuWilayani Geita na mtambo wa pili upo huko Nyakato Jijini Mwanza.

  Mwezi Agosti hadiSeptemba 2011, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ulifanya ukaguzi wahesabu za fedha na kodi kwa kampuni ya Minextech (ambayo sasa inaitwa AureusLimited). Ukaguzi huo uligundua kasoro kadhaa zilizoikosesha Serikali mapato.Baadhi ya kasoro hizo ni:

  1. Kampuni ya Minextech kuficha taarifa zake zamauzo ya dhahabu kiasi cha kilo 63.27 yenye thamani ya Shilingi 2,763,426,787katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010. Udanganyifu huo ulibainikabaada ya kulinganisha takwimu za uzalishaji zinazotunzwa na kampuni hiyo nakulinganisha na taarifa za mauzo ya dhahabu zilizowasilishwa Serikalini nakampuni hiyo katika kipindi husika.

  2. Kampuni ya Minextech kutolipa kiasi cha Shilingi 9,085,031,656 kama VAT yamauzo ya dhahabu katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

  3. Kampuni ya Minextech kutolipa kiasi cha Shilingi252,683,678 kama PAYE katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

  4. Kampuni ya Minextech kutolipa kiasi cha Shilingi371,026,716 kama mrabaha katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.Hatuastahiki zinaendelea kuchukuliwa na Serikali ili kuhakikisha malipo hayoyanafanyika.

  Tuhuma za UtoroshajiMadini ya Dhahabu

  Kumekuwepo na tuhuma mbalimbali kuwa, Kampuni ya Aureus Limited imekuwaikizalisha dhahabu nyingi na kuitorosha nje ya nchi na hivyo kukwepa kulipakodi za Serikali. Kwa mfano, mwezi wa Juni, 2012 iliripotiwa katika Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba kampuni ya Aureus Limited imekuwaikizalisha wastani wa kilo 15 kwa wiki na kuzitorosha nje ya nchi bila kulipakodi za Serikali. Kufuatia tuhuma hizo, Wizara kupitia Wakala wa Ukaguzi waMadini Tanzania (TMAA) ilichukua hatua za haraka kwa kuweka usimamizi makini washughuli za uzalishaji za kampuni hiyo ili kubaini ukweli.

  TMAA ilianza rasmi kukagua uzalishaji na mauzo ya dhahabu ya kampuni ya AureusLimited kuanzia tarehe 16 Juni, 2012 ambapo Wakala uliweka Mkaguzi katikamtambo wa kampuni hiyo uliopo katika Kijiji cha Nyarugusu. Pia, tarehe 27 Juni2012 Wakala uliweka Mkaguzi katika mtambo wa uchenjuaji wa kampuni hiyo uliopohuko Nyakato Jijini Mwanza. Ukaguzi unaofanywa na Wakala ulilenga kupatataarifa sahihi na za kina za uzalishaji wa kampuni hiyo na kuhakikisha kuwaSerikali inapata kodi na mrabaha stahiki.


  Matokeo ya Uchunguzi wa Awali


  Mapitio ya taarifa za uzalishaji wa kampuni hiyo zilizowasilishwa Serikalinikuanzia mwaka 2006 hadi 2011 zilionesha kwamba kwa wastani, kampuni hiyoilikuwa ikitoa taarifa ya kuzalisha kilo 4 za dhahabu kila mwezi.


  Tathmini ya awaliiliyofanywa na TMAA kuangalia uwezo halisi wa kuzalisha dhahabu katika mitamboya kampuni hiyo ulionesha kuwa, mtambo una uwezo wa kuchenjua tani za marudio3,500 kila mwezi. Matokeo ya uchunguzi wa sampuli za kimaabara kwa marudio(gold tailings) yalikuwa na wastani wa kiasi cha gramu 4 ya dhahabu kwa tanimoja, na makapi yalikuwa na wastani wa gramu 1 ya dhahabu kwa tani moja, hivyokuwepo kwa uwezo wa kuzalisha kilo 10 za dhahabu kwa mwezi.


  Ukaguzi wa Uzalishaji wa Dhahabu Mgodini


  Ukaguzi uliofanywa na TMAA kuanzia tarehe 26 Juni, 2012 hadi tarehe 3 Septemba,2012 unaonesha kuwa, uzalishaji wa dhahabu katika kipindi ambacho Wakalaumekagua shughuli za uzalishaji wa kampuni hiyo ni mkubwa kuliko uliokuwepokatika kipindi kabla ya kuanza kwa ukaguzi. Kwa mfano, jumla ya kilo 8.72 za dhahabuzilizalishwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012.


  Ikumbukwe kuwa, marudio(gold tailings) yanayopembuliwa hivi sasa na kampuni hiyo yana dhahabu kidogoukilinganisha na marudio yaliyokuwa yanapembuliwa miaka iliyopita (kuanziamwaka 2006 hadi 2010). Hivyo, huu ni ushahidi wa wazi kuwa kampuni hiyo ilikuwahaitoi taarifa sahihi Serikalini za uzalishaji na mauzo ya dhahabu.

  TMAA ilikubaliana na kampuni ya Aureus Limited kuwa, wakati kazi katika mtambowa elution zinapofanyika, Mkaguzi wa Wakala atakuwa na ruhusa ya kuingia katikaeneo la mtambo na kuchukua taarifa za uzalishaji wa dhahabu bila kizuizichochote. Pia, lakiri zitakazotumika kudhibiti uzalishaji kwenye mtambo huo haziwezikuondolewa bila kuwepo kwa Mkaguzi wa Wakala. Baada ya kuafikiana kuhusuutaratibu wa ukaguzi na udhibiti wa uzalishaji, Wakala umeendelea na kazi yaukaguzi kama kawaida.  TUKIO LA KUKIUKA MAKUBALIANO NA KUKATA LAKIRI ZA SERIKALI


  Mnamo tarehe 9/9/2012 Mkaguzi wa TMAA alipangiwa kufanya ukaguzi katika mtambo wa kuchenjulia dhahabu (elution) wa kampuni ya Aureus Limited uliopo huko Nyakato - Mwanza.


  Ratiba ya kazi iliyopangwa awali na uongozi wa kampuni hiyo ilikuwa, Mkaguzi afike katika eneola mtambo saa moja asubuhi. Mkaguzi huyo alifika mahali hapo muda wa saa 12 nadakika 55 asubuhi. Hata hivyo, Walinzi wa kampuni hiyo hawakumruhusu kuingiandani ya jengo la uzalishaji na walimfahamisha kuwa uzalishaji wa dhahabu usingekuwepo siku hiyo, na badala yake ungefanyika siku inayofuata, yaaniJumatatu ya tarehe 10 Septemba 2012.


  Kufuatia maelekezo hayo,Mkaguzi aliondoka na kurejea ofisini kuendelea na kazi nyingine.Tarehe10/9/2012 siku ya Jumatatu saa moja kamili asubuhi, Mkaguzi alifika tena kwenyemtambo wa kampuni hiyo huko Nyakato – Mwanza. Alipowasili katika eneo hilo,alijulishwa na Wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa, walifanya kazi tarehe9/9/2012.

  Mkaguzi aliambiwa kwamba,lakiri zilikatwa na uzalishaji ulifanyika. Lakiri zilizoondolewa kwenye mapipa yanayohifadhi loaded carbon ni zenye namba MEM-TMAA 133570-81 na zile zilizotolewa kwenye mitungi ya kuchenjulia dhahabu ni zenye namba MEM-TMAA132691-4. Kitendo cha kampuni hiyo kufanya kazi ya uchenjuaji wa dhahabu bila kuwepo Mkaguzi wa Serikali ni kukiuka makubaliano kati yake na Serikali na nidharau kwa Serikali. Hivyo, Mkaguzi wa TMAA alitoa taarifa kwa Uongozi wa Wakala ambao nao ulizifikisha taarifa hizo Wizarani kwa hatua zaidi. Kufuatia tukio hilo, Serikali imechukua hatua zaawali za kuhakikisha kuwa wahusika wote wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka. Tayari viongozi wawili wakuu wa kampuni hiyo wapo mikononi mwa Jeshi la Polisi na uchunguzi zaidi unaendelea kabla ya Serikali kuchukua hatua zaidi zinazostahili.

  Tukio hili linadhihirisha wazi kuwa, kampuni yaAureus Limited ilikuwa imekusudia kuficha kiasi halisi cha uzalishaji wake kwa lengo la kukwepa kulipa mrabaha na kodi stahi  Mhe. Stephen J. Masele

  NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI(MADINI)

  Source: matukio-michuzi

  My take: Chini ya serikali dhaifu tusitegemee makubwa katika kuinua uchumi!!!


   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  NGELEJA ANYONGWE!alikataa kabisa madini hayaibiwi eti yanapita JNIA,sasa aitwe aeleze wameiba kiasi gani migodi yote
   
 3. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ndege zinazo tua na kuelekea nje ya nchi vipi? Hili shamba la bibi
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  serikali ya mkoloni hii,tumekwisha
   
 5. K

  KINUKAMORI Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila siku tz tunapigwa changa la macho tu
   
 6. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngeleja na pinda wanataarifa maana jana pinda kamsifia kuwa ngeleja ni mchapakazi!!!Kweli magamba ni magamba alafu hata huyu waziri anayeitwa simbachawene ni gamba hana anachokijua zaidi ya kufunga tairi za magari
   
 7. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Just a Tip of an Iceberg.....
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  vitu kama hivi vinanipaga hasira sana bora nisiwe nafungua such topics
   
 9. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tz ni shamba la bibi yao
   
 10. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha haaaa hichi kichekesho tu.. mchezo wa kuigiza! waanze na Barrick, GGM na tanzanite one kwanza.. Nchi hii tunaibiwa kila siku mabilioni wanakuja kutudanganya na huu mchezo wa kuigiza ili kupata credit? hiyo waliyoitoa ni ndogo sana kimsingi kila siku huo ndio mchezo na ndio maana ngeleja akawekwa na Rosti tamu pale nishati na madini..

  Ngeleja si aliwabishia Hamad Rashid na Wenje kuhusu huu wizi? sasa aitwe atuambie ukweli
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huu uzembe ni sababu ya CDM serikali ichukiwe na wananchi wake!
   
 12. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kama kisai hicho cha pesa kinapotea kwenye kampuni ndogo hivyo ambayo haichimbi inachambuwa dhahabu kwenye mabaki ya udongo ulio kwisha chambuliwa dhahabu mwanzoni je ni vipi zile zinazo chimba gold yaani kampun kubwa?
  ngeleja na wengineo lazima ni matrilionea ukijumlisha na nguzo za mgololo zilisemwa zinatoka south
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwani huo mchezo umeanza leo, hawa ccm na watendaji wao ni legelege , eti hako kajamaa kameona na kenyewe kamepata deal la kutuambia, TUNAHITAJI KUJUA TUMEPATA HASARA KIASI GANI NA NAMNA GANI TUTARUDISHA HASARA TULIYOPATA.
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kuna haja kubwa sana ndani ya katiba mpya iwekwe sheria ya viongozi wawe wananyongwa mapema sana mara wabainikapo wana kosa.
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  nimejaribu kutafuta habari hii sijaipata lakini nimesikia asubuhi leo kuwa Mh. Pinda kamsifia sana Ngeleja na hata kwenda mbele na kumfananisha na mzee Mwinyi.
  Hawa watawala wanasahau kitu kimoja kuwa this is a 'century of light', wamejaribu kutuangalia wachache kati yetu kama wajinga na kuamini kuwa watatupumbaza daima lakini hawajui kuwa wao ndio wajinga zaidi. Pesa hizi wangeridhika na plosho pamoja na mishahara yao na kuzibakisha hapa tungefaidi sote lakini sasa zimeondoka na wenyewe wako 'matajiri' katikati ya umasikini waliousababisha au masikini waliowaibia. Mambo yatafanyika gizani lakini mwishoni yatajulikana tu!

   
 16. N

  NKANOELI JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yaani hata mm nimeshangaa,kusikia Pinda anamsifia Ngeleja,wanalao jambo.FYUUUUUUUUUUUUUUUU! nasikia hasira sana,ningekuwa na amri hawa ni risasi hadharani pumbafffffffffffffffff
   
 17. controler

  controler JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nikchangia hapa NAWEZAPIGWA na FLYING OBJECT YENYE NCHA KALI iENDAYO KASI
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  wanajifanya wamestuka leo wakati wanajua wanapochimba dhahabu kuna na madini mengine kama silver na mengine, lakini wamesaini mkataba wa dhahabu au almasi pekee na hayo mengine mchanga unapelekwa ulaya kila mwezi,..ridhiwan ana tender ya kupeleka malori yake buzwagi kusafirisha huo mchanga hadi bandari,..mzindakaya ana tender ya kusambaza nyama kutoka kwenye shamba lake la ng'ombe analolimiliki na mkapa..nchi imeshauzwa hii
   
 19. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Kuhusu BARICK (kahama, buzwagi na north mara) or ANGROGOLD ASHANTI( GGM)? Tunataka report ya ukaguzi ya hizo kampuni.
   
 20. g

  godliving Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kabila ya kuwakamata hao wahusika walitakiwa kukamatwa mawaziri waliopigwa chini CNGELEJA).Halafu uongozi wa hiyo kampuni ubanwe waseme nani anayewapa kiburi kiasi hicho. MWISHO HIYO KAMPUNI IFILISIWE KABISA KWA KUHUJUMU UCHUMI WA NCHI
   
Loading...