Udanganyifu wa kampuni ya madini (WAANIKWA)

Nitaunganisha hizi dots za data mnazotoa, nikirudi nakuja na full data juu ya issue hii
 
hapa kinahijika kitendo wala sio maneno maana maneno kila siku tulishachoka tutaka utekelezaji wala sio uhuni uhuni wa kutundanganya mnafanya kazi kumbe ndio mianya ya kula kuku kupitia maliasili zetu
 
ni mwendelezo wa Sarakasi na Mazingaombwe aliyowahi kuyazungumzia Mzee Mwanakijiji.
Hao waliohusika wanatakiwa wakamatwe na kisha sheria zifuatwe na wakipatikana na hatia wafungwe.
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDANGANYIFU ULIOBAINIKA KUFANYWA NA KAMPUNI YAUCHIMBAJI IITWAYO AUREUS LIMITED AMBAYO ZAMANI ILIKUWA IKIJULIKANA KAMAMINEXTECH


Utangulizi

Kampuni ya Aureus Limited(zamani ilikuwa ikiitwa Mineral Extraction Technologies Ltd (Minextech)) nikampuni inayojishughulisha na uchenjuaji wa marudio ya dhahabu ya wachimbajiwadogo (gold tailings) kwa kutumia teknolojia ya kemikali ya sayanaidi (vatleaching).

Kampuni hiyo inamilikileseni ya uchimbaji madini ML 384/2009. Mitambo ya uchenjuaji ya kampuni hiyoipo katika maeneo mawili, mtambo wa kwanza upo katika Kijiji cha NyarugusuWilayani Geita na mtambo wa pili upo huko Nyakato Jijini Mwanza.

Mwezi Agosti hadiSeptemba 2011, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ulifanya ukaguzi wahesabu za fedha na kodi kwa kampuni ya Minextech (ambayo sasa inaitwa AureusLimited). Ukaguzi huo uligundua kasoro kadhaa zilizoikosesha Serikali mapato.Baadhi ya kasoro hizo ni:

1. Kampuni ya Minextech kuficha taarifa zake zamauzo ya dhahabu kiasi cha kilo 63.27 yenye thamani ya Shilingi 2,763,426,787katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010. Udanganyifu huo ulibainikabaada ya kulinganisha takwimu za uzalishaji zinazotunzwa na kampuni hiyo nakulinganisha na taarifa za mauzo ya dhahabu zilizowasilishwa Serikalini nakampuni hiyo katika kipindi husika.

2. Kampuni ya Minextech kutolipa kiasi cha Shilingi 9,085,031,656 kama VAT yamauzo ya dhahabu katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

3. Kampuni ya Minextech kutolipa kiasi cha Shilingi252,683,678 kama PAYE katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

4. Kampuni ya Minextech kutolipa kiasi cha Shilingi371,026,716 kama mrabaha katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.Hatuastahiki zinaendelea kuchukuliwa na Serikali ili kuhakikisha malipo hayoyanafanyika.

Tuhuma za UtoroshajiMadini ya Dhahabu

Kumekuwepo na tuhuma mbalimbali kuwa, Kampuni ya Aureus Limited imekuwaikizalisha dhahabu nyingi na kuitorosha nje ya nchi na hivyo kukwepa kulipakodi za Serikali. Kwa mfano, mwezi wa Juni, 2012 iliripotiwa katika Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba kampuni ya Aureus Limited imekuwaikizalisha wastani wa kilo 15 kwa wiki na kuzitorosha nje ya nchi bila kulipakodi za Serikali. Kufuatia tuhuma hizo, Wizara kupitia Wakala wa Ukaguzi waMadini Tanzania (TMAA) ilichukua hatua za haraka kwa kuweka usimamizi makini washughuli za uzalishaji za kampuni hiyo ili kubaini ukweli.

TMAA ilianza rasmi kukagua uzalishaji na mauzo ya dhahabu ya kampuni ya AureusLimited kuanzia tarehe 16 Juni, 2012 ambapo Wakala uliweka Mkaguzi katikamtambo wa kampuni hiyo uliopo katika Kijiji cha Nyarugusu. Pia, tarehe 27 Juni2012 Wakala uliweka Mkaguzi katika mtambo wa uchenjuaji wa kampuni hiyo uliopohuko Nyakato Jijini Mwanza. Ukaguzi unaofanywa na Wakala ulilenga kupatataarifa sahihi na za kina za uzalishaji wa kampuni hiyo na kuhakikisha kuwaSerikali inapata kodi na mrabaha stahiki.


Matokeo ya Uchunguzi wa Awali


Mapitio ya taarifa za uzalishaji wa kampuni hiyo zilizowasilishwa Serikalinikuanzia mwaka 2006 hadi 2011 zilionesha kwamba kwa wastani, kampuni hiyoilikuwa ikitoa taarifa ya kuzalisha kilo 4 za dhahabu kila mwezi.


Tathmini ya awaliiliyofanywa na TMAA kuangalia uwezo halisi wa kuzalisha dhahabu katika mitamboya kampuni hiyo ulionesha kuwa, mtambo una uwezo wa kuchenjua tani za marudio3,500 kila mwezi. Matokeo ya uchunguzi wa sampuli za kimaabara kwa marudio(gold tailings) yalikuwa na wastani wa kiasi cha gramu 4 ya dhahabu kwa tanimoja, na makapi yalikuwa na wastani wa gramu 1 ya dhahabu kwa tani moja, hivyokuwepo kwa uwezo wa kuzalisha kilo 10 za dhahabu kwa mwezi.


Ukaguzi wa Uzalishaji wa Dhahabu Mgodini


Ukaguzi uliofanywa na TMAA kuanzia tarehe 26 Juni, 2012 hadi tarehe 3 Septemba,2012 unaonesha kuwa, uzalishaji wa dhahabu katika kipindi ambacho Wakalaumekagua shughuli za uzalishaji wa kampuni hiyo ni mkubwa kuliko uliokuwepokatika kipindi kabla ya kuanza kwa ukaguzi. Kwa mfano, jumla ya kilo 8.72 za dhahabuzilizalishwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012.


Ikumbukwe kuwa, marudio(gold tailings) yanayopembuliwa hivi sasa na kampuni hiyo yana dhahabu kidogoukilinganisha na marudio yaliyokuwa yanapembuliwa miaka iliyopita (kuanziamwaka 2006 hadi 2010). Hivyo, huu ni ushahidi wa wazi kuwa kampuni hiyo ilikuwahaitoi taarifa sahihi Serikalini za uzalishaji na mauzo ya dhahabu.

TMAA ilikubaliana na kampuni ya Aureus Limited kuwa, wakati kazi katika mtambowa elution zinapofanyika, Mkaguzi wa Wakala atakuwa na ruhusa ya kuingia katikaeneo la mtambo na kuchukua taarifa za uzalishaji wa dhahabu bila kizuizichochote. Pia, lakiri zitakazotumika kudhibiti uzalishaji kwenye mtambo huo haziwezikuondolewa bila kuwepo kwa Mkaguzi wa Wakala. Baada ya kuafikiana kuhusuutaratibu wa ukaguzi na udhibiti wa uzalishaji, Wakala umeendelea na kazi yaukaguzi kama kawaida.



TUKIO LA KUKIUKA MAKUBALIANO NA KUKATA LAKIRI ZA SERIKALI


Mnamo tarehe 9/9/2012 Mkaguzi wa TMAA alipangiwa kufanya ukaguzi katika mtambo wa kuchenjulia dhahabu (elution) wa kampuni ya Aureus Limited uliopo huko Nyakato - Mwanza.


Ratiba ya kazi iliyopangwa awali na uongozi wa kampuni hiyo ilikuwa, Mkaguzi afike katika eneola mtambo saa moja asubuhi. Mkaguzi huyo alifika mahali hapo muda wa saa 12 nadakika 55 asubuhi. Hata hivyo, Walinzi wa kampuni hiyo hawakumruhusu kuingiandani ya jengo la uzalishaji na walimfahamisha kuwa uzalishaji wa dhahabu usingekuwepo siku hiyo, na badala yake ungefanyika siku inayofuata, yaaniJumatatu ya tarehe 10 Septemba 2012.


Kufuatia maelekezo hayo,Mkaguzi aliondoka na kurejea ofisini kuendelea na kazi nyingine.Tarehe10/9/2012 siku ya Jumatatu saa moja kamili asubuhi, Mkaguzi alifika tena kwenyemtambo wa kampuni hiyo huko Nyakato – Mwanza. Alipowasili katika eneo hilo,alijulishwa na Wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa, walifanya kazi tarehe9/9/2012.

Mkaguzi aliambiwa kwamba,lakiri zilikatwa na uzalishaji ulifanyika. Lakiri zilizoondolewa kwenye mapipa yanayohifadhi loaded carbon ni zenye namba MEM-TMAA 133570-81 na zile zilizotolewa kwenye mitungi ya kuchenjulia dhahabu ni zenye namba MEM-TMAA132691-4. Kitendo cha kampuni hiyo kufanya kazi ya uchenjuaji wa dhahabu bila kuwepo Mkaguzi wa Serikali ni kukiuka makubaliano kati yake na Serikali na nidharau kwa Serikali. Hivyo, Mkaguzi wa TMAA alitoa taarifa kwa Uongozi wa Wakala ambao nao ulizifikisha taarifa hizo Wizarani kwa hatua zaidi. Kufuatia tukio hilo, Serikali imechukua hatua zaawali za kuhakikisha kuwa wahusika wote wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka. Tayari viongozi wawili wakuu wa kampuni hiyo wapo mikononi mwa Jeshi la Polisi na uchunguzi zaidi unaendelea kabla ya Serikali kuchukua hatua zaidi zinazostahili.

Tukio hili linadhihirisha wazi kuwa, kampuni yaAureus Limited ilikuwa imekusudia kuficha kiasi halisi cha uzalishaji wake kwa lengo la kukwepa kulipa mrabaha na kodi stahi



Mhe. Stephen J. Masele

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI(MADINI)

Source: matukio-michuzi

My take: Chini ya serikali dhaifu tusitegemee mabwa katika kuinua uchumi!!!


Uu

Ukifuatilia sana utakuta kuna mtu kanyimwa mgao wake kaamua kumwaga mboga
 
Nilishagawahi kusema hapa siku nyingi kuwa hawa jamaa wakiotea ka issue kadogo kama haka kanapewa coverage kuuuubwa utadhani ni kitu cha ajabu sana kwenye nchi hii. Tangu 2006 mtu anapiga leo ndio mnatoa trailer? Huyu naye sijui kakosea wapi maana hakuna mzungu katika nchi hii naomba nirudie tena, nasema hivi hakuna mzungu ndani ya ardhi ya Tanzania anayeweza kuthubutu kuiba bila kusaidiwa na mtanzania! Swali ni je nyuma ya huyu mzungu wapo kina nani? Tushukuru mabadiliko ya baraza la mawaziri maana haya yote tusinge ya fahamu na hakika nawaambieni tukibadili na chama wenye roho ndogo watazimia kwa madudu yaliyopo chini ya capet!
N.B Ikumbukwe kuwa jamaa alikuwa anaosha masalio ya udongo yaliyochimbwa na kusafishwa na wachimbaji wadogo wadogo na alikuwa anapiga pesa kiasi hiki hao wengine wanaosaga mawe pure usiku na mchana tangu 1999 itakuwaje?
 
naomba wachunguze na kampuni hizi Petra diamond ltd (Williamson diamond ltd),ELHILAH na Hilah soud kama wanalipa mirahaba na kodi za selikali.Kila siku ndege zinatorosha almas kwenda nje ya nchi .
 
Hivi na sisi tunaochangia humu tumepigwa na changa la macho na huu uhuni wa magamba. Eti wanatamba kukamata mwizi leo 2012 wakati wizi umeanza 2006? Walikuwa wapi na hili limefumuliwa na wapinzani bungeni! Wasingefumua ingekuwaje? Hawa TMAA wamekuwa takukuru kwamba wanaenda kukagua tu pale kunapokuwa na taarifa za wizi au ni wajibu wao kukagua kila siku? Hivi waandishi wa habari waliuliza haya maswali au walipewa tu hili karatasi wakakimbilia kuandika magazetini?

Wasitake kutuchanganya na wajinga huu wizi wanahusika kwa asilimia 100 huku nikuwafool wadaganyika ila mie na wenye akili wengine hatumo!
 
Wakuu,

Inawezekana hesabu zinanipiga chenga lakini sielewi mtu atafanyaje mauzo ya Tshs. 2,763,426,787 na atakiwe kulipa VAT ya Tshs. 9,085,031,656? Yaani VAT ni kubwa zaidi ya mauzo yenyewe? Huyo aliyetoa hiyo taarifa ameziangalia kwa makini hizo tarakimu?

Tiba
 
VAT inazidi mauzo au nimeona vibaya!!???

Mkuu na mimi nimeliona hilo ngoja tusubiri wataalamu wamahesabu waje watwambie!!! Hii inaonyesha ni jinsi gani watu wanafanya kazi kwa kukurupuka. Huyo Naibu Waziri amewezaje kusaini/kuruhusu hiyo taarifa nyenye makosa kimahesabu itoke na jina lake?

Tiba
 
Hii ndio sababu moja wapo ya kuichukia CCM, 2015 nitamalizia hasira zangu zote na kuhakikisha Magamba wanatokomezwa na Kikwete, Mkapa pamoja na mafisadi wengine wanakwenda jela na kufia huko
 
Back
Top Bottom