Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,578
- 7,281
Baada ya kufuta Central Admission System (CAS) na kuweka uombaji wa vyuo moja kwa moja chuoni (Direct Application to Institutions-DAI) naamini sasa tumepata uzoefu unaotuwezesha kufanya tathmini itakayo tuwezesha kuamua mfumo wa kutumia(CAS, DAI au mfumo mwingine). Tuliambiwa CAS inawafanya waombaji wapangiwe program wasizo omba (tukapewa mifano ya rushwa hata kama hakuna ushahidi uliowekwa wazi).
CAS ikaondolewa na sasa tuna hiyo DAI (siyo jina rasmi).Tumesguhudia tatizo kubwa la multiple selection ambalo matokeo yake ni pamoja na kutibua calendar ya udahili (mwaka wa jana na huu tumefika round ya nne), vyuo kabla ya kujua wana nafasi zipi raundi ifuatayo huanza, wenye multiple selection hushika nafasi zaidi ya moja na kila round wapo.
Jana TCU wameonyesha kuna kama vijana 5000+ hawaja confirm round ya 1-3. Dakika ya mwisho kutakuwa na nafasi wakati tuna vijana wana ufaulu wa kuweza kujaza hizo nafasi lakini watakosa. Bodi ya mikopo nayo hauwezi kutoa mkopo kwa mtu ambae hawajui amechaguliwa wapi na wao wana muda muafaka wa kutoa majina ya waliopata mkopo.
Hivyo wengi ambao wanakadhia ya multiple selection si ajabu itakula kwao. Na je kila mtu anaepata chuo anapata anachotaka?
Nafikiri ni wakati muafaka kuwe na tathmini ya mifumo hii na uwazi katika hili ili tujue tunakwenda wapi. Waizara ya Elimu , TCU, NACTE, na Vyuo ni baadhi ya wadau. Ni imani yangu zoezi kama hili likifanywa kwa uwazi litasaidia. Na hili liendane na vyuo kuna na uwazi mtu akikosa ajue amekosaje.
Naweka baadhi ya mijadala iliyopita kuhusu kuondolewa kwa CAS-mapovu yalitutoka lakini kuna historia ndani yake na labda njia za kutatua baadhi ya haya mapungufu.
Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli? - JamiiForums
Kuondolewa CAS ni chanzo udahili mbovu - JamiiForums
TCU mnaturudisha nyuma. Kwa mfumo wenu mpya wa udahili vyuoni, mnatuonea wananchi - JamiiForums