VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Baada tu ya Zitto,Kitila na Mwigamba kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya CHADEMA,kumekuwa na msururu wa Matamko kutoka kwa wanaojipambanua kama 'Wanaolaani Maamuzi ya Kamati Kuu'. Matamko yametokea sehemu mbalimbali za nchi. Kwa udadisi wangu binafsi,naona kuwa Matamko yote kama si kuandaliwa na CCM basi yanawahusisha CCM moja kwa moja. Nina sababu za udadisi huu:
Kwanza, Matamko yote yametolewa na watu waliojichanganya sana. Wapo waliojipa vyeo visivyokuwepo mfano Chitanda wa Mtwara na yule wa Mwanza. Haraka CHADEMA inaingia na kuumbua. Kutokana na kujisingizia vyeo na hadhi chamani, si ngumu kuona hizi ni porojo na propaganda. Udadisi unanielekeza kuwa CCM yahusika.
Pili, Matamko yote:lile la Mtwara,Dar Es Salaam na Mwnza,yamejaa kashfa mpya,tuhuma mbichi na vitisho. Hayajajielekeza kwenye uamuzi hasa wa Kamati Kuu. Yametaka kuvuruga tu amani ya kwenye chama. Hizi ni njia zitumiwazo hasa na CCM dhidi ya CHADEMA. Kumbebasi, matamko haya ni ya CCM.
Tatu, mara baada ya kutolewa matamko hayo,wa kwanza kuweka mitandaoni ni wana-CCM. Baada ya kuweka hujaa kujadili kwa kusifu matamko na kukandia tu CHADEMA.Ni kukandia tu bila ya kujenga mantiki yoyote. Udadisi wangu unanieleza kuwa Matamko haya ni ya CCM!
Nne,Matamko hayo ya 'watu wa CHADEMA' yamepokelewa kwa bashasha sana na magazeti ya Serikali ya CCM na magazeti ya chama,yaani CCM.Yamepata kurasa za mbele haraka na kupambwa kiuandishi. Udadisi wangu unanilazimisha kuamini kuwa CCM wanahusika na Matamko haya.
Kwahiyo, CCM inahusika na Matamko haya.Udadisi wangu unasema kwa sauti kuu kuwa watoa Matamko waliandaliwa kwa ustadi mkubwa ingawa wameangukia pua. Watoa Matamko wameumbuka haraka hata kabla. Ni aibu iliyoje. CCM inahusika na Matamko haya.Ni udadisi tu waungwana!