UDA yaivua nguo serikali

Danpol

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
5,747
Reaction score
9,012
SAKATA la umiliki wa Shirika la Usafiri jijini Dar es Salaam (UDA), limeiingiza serikali katika aibu ya mwaka, huku mawaziri na wabunge ‘wakivuana nguo' bungeni.

Hali hiyo iliyosababisha baadhi ya wabunge kuishambulia serikali, ilitokea juzi wakati wa mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Waliohitimisha mnyukano huo kwa kauli za kuumbuana ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu Spika Job Ndugai.

Dk. Mwakyembe, akihitimisha mjadala huo, alisema suala la umiliki wa UDA halina uhusiano na wizara yake, hivyo alimlaumu Naibu Spika Ndugai, kuruhusu mjadala huo kwenye wizara yake, huku Naibu Spika huyo akifoka na kusisitiza wizara hiyo inahusika.

Awali kabla ya mzozo wa UDA haujaanza juzi, Waziri Mwakyembe, wakati akijibu hoja za Waziri Kivuli na Msemaji Rasmi wa Kambi ya Upinzani wa wizara hiyo, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), aliyehoji sakata la UDA, aliweka bayana kwamba suala la umiliki wa shirika hilo halihusu wizara yake.

Hata hivyo, pamoja na kuweka angalizo hilo mapema na wakati Bunge likiendelea, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kingwangala (CCM), aliliibua sakata hilo na kusema kuwa mmiliki wa UDA, Robert Kisena, alinunua kihalali.

Dk. Kingwangala, alitoa kauli hiyo akijua fika kwamba siku chache zilizopita, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alilipeleka suala la UDA mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kumhoji Kisena kwa kauli yake kwamba wabunge waliopinga umiliki wa UDA, wamehongwa na mwekezaji wa nje anayetaka kuinunua.

Sambamba na hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, amepata kuliambia Bunge wiki iliyopita kuwa sakata la umiliki wa UDA limepelekwa tena mbele ya Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa hatua zaidi za kisheria.

Mbali na viongozi hao, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Adam Malima, wiki iliyopita wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alisema UDA inamilikiwa na serikali kwa asilimia 49 ya hisa na Jiji la Dar es Salaam asilimia 51, na kwamba mmiliki wa sasa, Kampuni ya Simon Group chini ya Kisena hana umiliki wa hisa.

Akijenga hoja yake juzi bungeni, Dk. Kingwangala, alisema mmiliki wa UDA, Kisena amekuwa akinyanyaswa kutokana na kauli tata za serikali.

Huku akisoma nyaraka za kuhalalisha umiliki wa UDA kwa Kisena, mbunge huyo alitaka serikali itoe kauli juu ya sakata hilo na kama asingepata majibu ya kuridhisha, angekwamisha Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wengi, akiwemo Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola (CCM), aliyemshangaa Waziri Mwakyembe kwamba suala la UDA halihusiani na wizara yake.

Lugola, alisoma moja ya barua ya Wizara ya Uchukuzi wakati huo ikiitwa Wizara ya Miundombinu, ikitoa maelekezo kuhusu suala la UDA, hivyo alisisitiza kuwa wizara hiyo inahusika na kumtaka waziri atoe kauli juu ya mzozo huo.

Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge, Lugola alisema mwekezaji huyo amekuwa akizungushwa kama mchezo wa ‘Joyce Wowowo' huku wizara husika zikitupiana mpira.

Alisema wenye hisa, yaani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameamua kuuza hisa zao kwa Kisena, lakini aliishangaa serikali imekuwa ikitoa maelezo aliyoyaita ya kukengeuka.

Wakati mzozo ukiendelea, Waziri Malima alisimama kutoa ufafanuzi wa kauli yake ya awali ya umiliki wa hisa za UDA ambapo alisisitiza kuwa serikali haimtambui Kisena kwani alilinunua shirika hilo kiujanja.

Mpira wa hoja hiyo ulimrukia Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Multazar Magungu (CCM), aliyesema kama mnunuzi alikosea, serikali imlipe fidia na kulirudisha shirika hilo mikononi mwake na kisha kuliuza upya.

Alisema kwa sasa wanaomtetea Kisena, wana maslahi yao na wanaopinga pia wana maslahi yao, hivyo serikali ikae chini kupata ufumbuzi wa tatizo hili.

Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema kama Kisena alinunua UDA kwa bei ya kutupwa, wa kulaumiwa ni serikali na sio mmiliki wake.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alisema kama kuna jambo limeivua nguo serikali, hili la umiliki wa UDA ni aibu ya mwaka.

Mbowe, alisisitiza kuwa jambo hili limeivua nguo serikali kwani kauli za viongozi wake zinagongana na kamati tano za Bunge zilizoshughulika na suala hilo, kila moja inasema lake.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, sijawahi kuona serikali imenywea kama leo kwenye hoja hii. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwekezaji wa UDA ameingiza magari 300, serikali inamwona, kauli za viongozi wa serikali zinagongana, kamati tano kila moja inasema lake, leo mnakuja kuvuana nguo hadharani, hii ni aibu kwa serikali hii sikivu ya CCM.

"Ushauri wangu, kaeni chini mmalize utata huu badala ya kuvuana nguo bila sababu maana wananchi wa Dar es Salaam wanahitaji usafiri," alisema Mbowe.

Kuona mzozo unazidi kuwa mkubwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema serikali haijajivua nguo katika suala hilo kwani maelezo yake yako wazi.

Alisema Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), ipo na imesema wazi kwamba kuna utata wa umiliki wa UDA.

"Lakini pia si mnajua suala hili lipo Takukuru na kwa DPP. Pili Mnyika alilitolea mwongozo na jambo hili lipo mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kwa hatua zaidi," alisema Lukuvi.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), hakuridhika na majibu ya serikali ambaye katika mchango wake aliishangaa kusema haimjui mwekezaji Kisena wakati imetoa msamaha wa magari 300 aliyoyaingiza nchini bure bila kodi.

"Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja ya Kingwangala kuhusu mmiliki wa UDA. Mwekezaji huyo ameingiza magari 300, yakatolewa bure bila kodi, leo serikali hii hii inasema haimjui. Mmeenda mahakamani, ameshinda kesi, mahakama imewaachia huru. Hili suala liangaliwe upya, huyo mwekezaji ni mwenzetu, ngozi nyeusi (Mzawa), tumwache," alisema Serukamba.

Sakata la UDA lilihitimishwa kwa malumbano makali kati ya Naibu Spika Ndugai na Waziri Mwakyembe.

Ndugai, alipompa nafasi Mwakyembe kujibu hoja za wabunge kuhusu UDA, waziri huyo aling'aka huku akikunja sura kwamba wizara yake haihusiki na UDA.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nieleze masikitiko yangu kwa kuruhusu mjadala wa UDA ambao hauhusiani kabisa na hoja yangu. Mimi sijawahi kuliona faili la UDA likija mezani pangu, unataka nijibu nini hapa? Hatuhusiki ndio maana tangu awali nilisema hili halituhusu."

Kuona hivyo, Ndugai alisimama kwenye kiti chake na kufoka: "Suala hili linahusu Wizara ya Uchukuzi na mada iliyopo inahusu uchukuzi ndiyo maana leo wamekuja madereva wa malori, kwa hiyo linawahusu. Lakini jambo hili linatuhusu sote, kwa hiyo serikali ikae ije na majibu kumaliza utata huu," alisema Ndugai na kufunga mjadala wa UDA.

Mjadala nje ya Bunge


Baada ya mjadala wa UDA kumalizwa bungeni kwa kufuata ushauri wa Mbowe aliyeitaka serikali ikae chini kumaliza utata huo, nje ya ukumbi wa Bunge kulikuwa na vituko vyake.

Baadhi ya wabunge na mawaziri walisimama kwenye vikundi kujadili kilichojiri bungeni kuhusu suala la UDA.

Mshangao wa kwanza ulielekezwa kwa Naibu Spika kuruhusu mjadala huo huku akijua fika kwamba Spika Makinda, alishalitolea maamuzi na serikali kupitia kwa AG Werema ilieleza kwamba jambo hili lipo Takukuru.

Source: Tanzania Daima
 
Taarifa hii ina harufu ya Utanzania Daima
 
Sana jamvi tumeshuhudia Sakata la Uda likiteka binge,huku viongozi WA serikali wakijichanganya kwa kuonyesha kutokujua nini kinaendelea ktk shirika Hilo.Ni aibu kubwa Sana kwa viongozi wetu kuliuza Uda kama vile ni wachuuzi.
 
Wana jamvi tumeshuhudia Sakata la Uda likiteka binge,huku viongozi WA serikali wakijichanganya kwa kuonyesha kutokujua nini kinaendelea ktk shirika Hilo.Ni aibu kubwa Sana kwa viongozi wetu kuliuza Uda kama vile ni wachuuzi.
 
Taarifa hii ina harufu ya Utanzania Daima

Kwa hiyo Naibu spika aliyetaka Mwakyembe akibu hoja zinazohusiana na UDA ana uharufu wa Tanzania Daima?

Bisha vitu kwa logic, siyo unabisha kwa mahaba na uzezeta wa mapenzi yaliyojaa kopofu.
 
Yote haya yanatokea kwasababu ya kuwa na viongozi wa nchi ambao ni mafisadi!!!Mwakyembe analikwepa sakata la UDA kwavile anajua kuwa lina uvundo kama ule wa deni la ATCL kutokana na ukodishaji wa kihuni wa ile ndege aina ya AIRBUS!!!
 
Hiyo si familia Kikwete wamejiuzia tu.
 
Nikiona source: Tanzania Daima huwa napiti tu, bye!
 
Wawaulize Idd Simba na Didas Ma------ wanalijua sakata hili lililopelekea watu kuambiwa wanafikiria kwa kutumia maka...
 
Kwa hiyo Naibu spika aliyetaka Mwakyembe akibu hoja zinazohusiana na UDA ana uharufu wa Tanzania Daima?

Bisha vitu kwa logic, siyo unabisha kwa mahaba na uzezeta wa mapenzi yaliyojaa kopofu.

ndio shida ya kukaririshwa mambo ya kusema hapa ame-edit jibu alopewa wiki iliyopita
 
Jamani UDA ni ya kisena na riz1 hili liko wazi jamani
 
H Kigwangallah na Robert Kisena ni marafiki wakubwa na ni matapeli wakubwa kwenye sekta ya Pamba. Kigwangallah anamiliki MSK Solutions wakati Robert Kisena anamiliki Simon Agency ikiwa na ginnery pale Malampaka Maswa. Kigwangallah alipiganiwa na mama Salma Kikwete kupata ubunge wakati Robert Kisena alipiganiwa na Riziwani Kikwete kupata ubunge lakini wananchi wa Maswa wana akili kuliko wa Nzega na kugoma kumchagua tapeli kuwa mbunge licha ya kwamba Kisena alimchapa vibao OCD wa Maswa kituoni na RPC akasema ni masuala binafsi na watajuana wenyewe. Kisena hakuchukuliwa hatua wakati OCD alihamishwa.

Riziwani mmiliki wa UDA yuko bungeni, Mwakyembe kachaguliwa na Baba Riziwani na anatetea tumbo lake sio wananchi, mwisho wa siku kesi ya tumbili tumemkabidhi nyani aihukumu, watanzania tutaacha lini ujinga. Dawa sio kuitafuta UDA saizi maana hadi Jaji mkuu kateuliwa na Kikwete, dawa ni kuhakikisha tunapiga chini MaCCM 2015, au ikishindikana basi mtu wa Kikwete joka la mdimu asipokee kijiti 2015.
 
Nikiona source: Tanzania Daima huwa napiti tu, bye!

Kweli jina lako jidodo...

Jitu maskini kama wewe unaishi kwa fadhila za matapeli kama Riziwani ambao wamebakiza mwaka na nusu tu kuendelea kutamba, unasafiri kwa daladala kila siku badala ya kutetea UDA ili 2016 ikuokoe na kutembea kwa miguu unajifanya kuponda gazeti ili kutetea ufisadi wa bwana wako. Jionee huruma, Baba yako alikuwa maskini, wewe ni maskini na obvious mwanao atakuwa maskini, hujishangai wala kujionea huruma unatetea majizi.
 
Tanzania bwana! Nu ujanja ujanja tuuuuu kwa kila kitu. Sasa kwa nini suala la umiliki wa UDA liwe mjadala bungeni kama ni shirika halali?
 
Taarifa hii ina harufu ya Utanzania Daima

Wewe shangilia wanaume wanavyokula maisha na kujimilikisha UDA tu, yatakutokea puani 2016. Hivi vihela anavyokuhonga Riziwani vina kikomo, baada ya hapo utalazimika kuishi kihalali kama sisi na moto utakuwakia kwenye madaladala utaikumbuka UDA hautaipata.

We mbulumundu huoni hata uchungu UDA wanaingiza mabasi 300 bila kulipa ushuru wakati watanzania wengine wameshindwa kukomboa mabasi yao bandarini kwa sababu za ushuru mkubwa. Ubinafsi wa ajabu sana huu hata kama unamtetea mumeo.
 

Ngoja makuwadi wa mafisadi na maroboti ya Lumumba yaje na mapovu yenye shombo"!
 
Yote haya yanatokea kwasababu ya kuwa na viongozi wa nchi ambao ni mafisadi!!!Mwakyembe analikwepa sakata la UDA kwavile anajua kuwa lina uvundo kama ule wa deni la ATCL kutokana na ukodishaji wa kihuni wa ile ndege aina ya AIRBUS!!!

Mwakyembe ni mbinafsi mno. Anajua fika ukweli ukoje kuwa UDA ni ya Riziwani Kikwete, ila kwa kulinda kibarua inabidi akae kimya. Kumbuka Mwakyembe aliikana Tanganyika aliyoitetea kwenye research yake ya PhD. Kuna mijinga huwa unawaza Mwakyembe ana sifa za urais wakati mi naona hata za ubunge hana. Hawezi kutetea nchi Mwakyembe maana alikuwa anachangia huku anaangalia upande wa Riziwani kwa woga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…