UDA tena hiyo imeibuka repoti ya CAG 2014/2015

mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
4,133
6,343
Bodi ya Wakurugenzi ya UDA iliuza hisa za Shirika bila kupata kibali cha Serikali. Hisa za Shirika la UDA zilithaminishwa kwa bei ya Shilingi 744.79 kwa kila hisa mwezi Oktoba, 2009, na mwezi Novemba, 2010 thamani ya kila hisa ikawa 656.15.

Hata hivyo, katika uuzaji huo, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA ilitoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa kwa mwekezaji huyo (kwa Tathmini ya bei ya hisa ya mwezi Oktoba, 2009), bila kuwepo na sababu za kufanya hivyo. Kwa mujibu wa majibu ya Mlipaji Mkuu wa Serikali, Serikali haitambui uuzwaji wa hisa hizo. Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa tarehe 11 Februari, 2011 mnunuzi (mwekezaji) atalipa jumla ya Shilingi bilioni 1.14 kama bei ya ununuzi wa hisa zote ambazo zilikuwa hazijagawiwa, ingawa mkataba haukuonyesha akaunti ya benki ambayo malipo yangefanyika. Mnunuzi (mwekezaji) alilipa kiasi cha Shilingi milioni 285 pekee

katika akaunti namba 0J1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA. Hakukuwa na malipo mengine ya ziada yaliyofanywa na mwekezaji kuhusiana na ununuzi wa hisa za UDA. Mwenyekiti wa Bodi alipokea kiasi cha Shilingi milioni 320 kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa Mwekezaji ambayo kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ilikuwa ni ada ya ushauri alioutoa kwa Mwekezaji. Malipo haya yalizua mgongano wa kimaslahi. Wakati Serikali haitambui uuzwaji wa
hisa za UDA, ninashauri Shirika la UDA lirudishwe chini ya usimamizi wa Serikali hadi hapo mgogoro huu utakapotatuliwa.

Suala hili lilihojiwa katika ripoti zangu za miaka iliyopita na Serikali imewasilisha majibu kwa Ofisi yangu kuwa inaandaa mapendekezo ya kuuza asilimia 49 ya hisa za UDA na kufikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, majibu hayo hayaonyeshi kama hisa ambazo ziliuzwa bila kufuata utaratibu zitarejeshwa Serikalini na hatua zilizochukuliwa dhidi ya Bodi ya Wakurugenzi wa UDA kutokana na kukiuka taratibu za uuzaji wa hisa zaShirika hilo.
 
Jamani Kisena ni muhuni kupitiliza yani hela ya kununua tani tano za dagaa wananunua UDA!!!
 
Yaani biashara ya UDA ni jipu sugu, haiingii akilini kabisa kwa jinsi Iddi Simba alivyochomoka Mahakamani.
 
Sio kila jipu ni la kutumbua by LUGUMI, hili la uda mmoja wa wanashea ni Khalfan mtoto wa mstaafu lazima hii ishu itasafishwa kama lugumi.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya UDA iliuza hisa za Shirika bila kupata kibali cha Serikali. Hisa za Shirika la UDA zilithaminishwa kwa bei ya Shilingi 744.79 kwa kila hisa mwezi Oktoba, 2009, na mwezi Novemba, 2010 thamani ya kila hisa ikawa 656.15.

Hata hivyo, katika uuzaji huo, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA ilitoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa kwa mwekezaji huyo (kwa Tathmini ya bei ya hisa ya mwezi Oktoba, 2009), bila kuwepo na sababu za kufanya hivyo. Kwa mujibu wa majibu ya Mlipaji Mkuu wa Serikali, Serikali haitambui uuzwaji wa hisa hizo. Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa tarehe 11 Februari, 2011 mnunuzi (mwekezaji) atalipa jumla ya Shilingi bilioni 1.14 kama bei ya ununuzi wa hisa zote ambazo zilikuwa hazijagawiwa, ingawa mkataba haukuonyesha akaunti ya benki ambayo malipo yangefanyika. Mnunuzi (mwekezaji) alilipa kiasi cha Shilingi milioni 285 pekee

katika akaunti namba 0J1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA. Hakukuwa na malipo mengine ya ziada yaliyofanywa na mwekezaji kuhusiana na ununuzi wa hisa za UDA. Mwenyekiti wa Bodi alipokea kiasi cha Shilingi milioni 320 kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa Mwekezaji ambayo kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ilikuwa ni ada ya ushauri alioutoa kwa Mwekezaji. Malipo haya yalizua mgongano wa kimaslahi. Wakati Serikali haitambui uuzwaji wa
hisa za UDA, ninashauri Shirika la UDA lirudishwe chini ya usimamizi wa Serikali hadi hapo mgogoro huu utakapotatuliwa.

Suala hili lilihojiwa katika ripoti zangu za miaka iliyopita na Serikali imewasilisha majibu kwa Ofisi yangu kuwa inaandaa mapendekezo ya kuuza asilimia 49 ya hisa za UDA na kufikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, majibu hayo hayaonyeshi kama hisa ambazo ziliuzwa bila kufuata utaratibu zitarejeshwa Serikalini na hatua zilizochukuliwa dhidi ya Bodi ya Wakurugenzi wa UDA kutokana na kukiuka taratibu za uuzaji wa hisa zaShirika hilo.
UDA ni lazima ife na Mtu .
 
Back
Top Bottom