ufisadi mtupu, kwanza watanunua used buses, pili wataleta pungufu ya idadi wanayosema wameagiza kwa kisingizio cha kuyaleta kwa awamu, huyo wakala wa kuleta spare atapewa kigogo mmoja akishirikiana na hao wakorea na atauza bei ya kufa mtu si vya serikali, mwisho mwaka tu mabasi yote chali huku yakiacha madeni makubwa ya hiyo gesi ya sh 600 hii ndo bongo
Mkuu uko sahihi kuwa cynical. Ni kweli kuwa sekta ya umma TZ haijawa na rekodi nzuri kwenye biashara ya usafiri wa abiria barabarani. Lakini kwa upande wa usafiri wa mijini (urban transport), kuna tatizo la msingi kwamba mara nyingi si biashara inayolipa kutokana na kutofautiana kwa idadi ya wasafiri kwa nyakati (peak and non-peak times). UDA wanalijua hilo. Ni moja ya mambo yaliyowaathiri huko nyuma.
Katika nchi zilizoendelea inabidi wakati mwingine serikali za mtaa zitoe ruzuku ili kuhakikisha huduma ya uhakika nyakati zote (zenye abiria wengi na zisizo) kwa nauli isiyobadilika. Lakini wenzetu hao wana mahesabu ya uhakika ya biashara nzima; hivyo wanajua ni wapi, wakati gani na kiasi gani cha ruzuku kinahitajika.
Tatizo hapa kwetu, uswahili mwingi. Ukichanganya na wizi, udokozi, uzembe na ufisadi, si rahisi kutengeneza kampuni ya uhakika (credible) ya usafiri mjini. Wajanja wengine walituchezea hivihivi na mradi wa mabasi ya wanafunzi. Hii si biashara ya ubabaishaji. Inahitaji umakini mkubwa sana.
Kinachotakiwa ni UDA kutueleza kama wamefanya tathmini ya kitaaluma (feasibility study) kujihakikishia na kutuhakikishia (walipa kodi) kama kilichowadumaza huko nyuma wamekipatia ufumbuzi na kwamba wana mkakati mpya wa kibiashara (business strategy) unaowapa confidence ya kuingia kwenye uwekezaji huo ambao, bila shaka, umegubikwa na deni zaidi kuliko mtaji.

Hivi washafanya a dry run kabla ya kuingia kichwa kichwa? Isije kuwa mambo ya economic hitmen.
Hiyo natural gas wata refill wapi? au wataweka vituo vya kujazia natural gas all over Dar?
Hii move ni muhimu sana kimazingira katika juhudi za kupunguza uchafuzi wa mazingira, hususan uchafuzi wa hewa, lakini bila kupiga marufuku magari yanayotoa moshi mchafu tutakuwa hatujafanya kitu.
Halafu tumeuza bandari (TCTIS) Reli mabenki na pretty much everything lakini tumebakisha UDA iwe kwa serikali, yaani priorities zetu ziko wapi?
UDA kutumia Sh 24 bilioni kuagiza mabasi ya abiria
Elizabeth Ernest
KAMPUNI ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), imesema itatumia Sh 24 bilioni kununua mabasi 150 ya abiria yatakayotumia gesi asilia kwa ajili ya kusafirisha abiria jijiji Dar es Salaam.
Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni ya usafiri Dar es Salaam (UDA), Victor Milanzi alisema mabasi hayo, yataletwa mwezi Juni kutoka nchini Korea.
"Mabasi hayo yatatolewa kwa mkopo wa serikali ya Korea na mambo yakienda vizuri kabla ya Juni, mwaka huu yatakuwa yamewasili na kuanza kazi.
"Mabasi hayo, yatatumia gesi asilia ambayo itazalishwa na kiwanda cha Tanzania Petrolium Development Cooparation (TPDC) na yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 100, hivyo mradi huo, utasaidia kupunguza tatizo la usafiri jijini Dar es Salaam,"alisema Milanzi.
Alisema ili mradi huo, uwe endelevu kutakuwa na wakala wa vipuri ambaye ataletwa nchini na serikali ya Korea ili kurahisisha utengenezaji wa mabasi hayo, mara mradi huo, utakapoanza nchini.
Alisema mradi huo, utaongeza tija na ufanisi katika sekta ya usafirishaji kwa kuwa uendeshaji wa mradi huo, ni rahisi kwa asilimia 46 kuliko mabasi yanayotumia mafuta ya dizeli na petroli.
Milanzi alifafanua kwamba lita moja ya gesi ni Sh600 wakati lita ya dizeli ni Sh1,500 na pia mradi huo, utasaidia kupunguza wizi wa mafuta ya magari ulioshamiri jijini.
Alisema UDA itakapofanikiwa kuingiza mabasi hayo, pia itatoa ajira kwa madereva na kondakta watakaofanya shughuli katika mabasi hayo ambayo yatafanya ruti katika maeneo ya Dar es Salaam.
"Tayari tumefanya mazungumzo na serikali ya Korea kuhusu mradi huo, tumeandika mapendekezo na kufanya upembuzi yakinifu na tumeshawapelekea ubalozini kwao na tayari vimetumwa nchini Korea," alisema Milanzi