Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,720
- 21,778
UDA kutumia Sh 24 bilioni kuagiza mabasi ya abiria
Elizabeth Ernest
KAMPUNI ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), imesema itatumia Sh 24 bilioni kununua mabasi 150 ya abiria yatakayotumia gesi asilia kwa ajili ya kusafirisha abiria jijiji Dar es Salaam.
Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni ya usafiri Dar es Salaam (UDA), Victor Milanzi alisema mabasi hayo, yataletwa mwezi Juni kutoka nchini Korea.
"Mabasi hayo yatatolewa kwa mkopo wa serikali ya Korea na mambo yakienda vizuri kabla ya Juni, mwaka huu yatakuwa yamewasili na kuanza kazi.
"Mabasi hayo, yatatumia gesi asilia ambayo itazalishwa na kiwanda cha Tanzania Petrolium Development Cooparation (TPDC) na yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 100, hivyo mradi huo, utasaidia kupunguza tatizo la usafiri jijini Dar es Salaam,"alisema Milanzi.
Alisema ili mradi huo, uwe endelevu kutakuwa na wakala wa vipuri ambaye ataletwa nchini na serikali ya Korea ili kurahisisha utengenezaji wa mabasi hayo, mara mradi huo, utakapoanza nchini.
Alisema mradi huo, utaongeza tija na ufanisi katika sekta ya usafirishaji kwa kuwa uendeshaji wa mradi huo, ni rahisi kwa asilimia 46 kuliko mabasi yanayotumia mafuta ya dizeli na petroli.
Milanzi alifafanua kwamba lita moja ya gesi ni Sh600 wakati lita ya dizeli ni Sh1,500 na pia mradi huo, utasaidia kupunguza wizi wa mafuta ya magari ulioshamiri jijini.
Alisema UDA itakapofanikiwa kuingiza mabasi hayo, pia itatoa ajira kwa madereva na kondakta watakaofanya shughuli katika mabasi hayo ambayo yatafanya ruti katika maeneo ya Dar es Salaam.
"Tayari tumefanya mazungumzo na serikali ya Korea kuhusu mradi huo, tumeandika mapendekezo na kufanya upembuzi yakinifu na tumeshawapelekea ubalozini kwao na tayari vimetumwa nchini Korea," alisema Milanzi