kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,870
- 7,752
Umma wa wananchi wanafahamu kwamba Shirika la Usafiri Dar-es-Salaam- UDA halikubinafsishwa kihalali kwa Simon Group ila limeporwa kifisadi. Thamani ya mali za UDA ilikua kubwa sana kulinganisha na hela kiduchu waliyolipa Simon Group ambayo hata hivyo kiasi cha shilingi milioni mia tatu ziliishia mfuko binafsi wa mwenyekiti wa iliyokua bodi ya shirika hilo Idi Simba.
CAG mstaafu ametoa masikitiko yake hivi karibuni jinsi kesi ya Idi Simba ilivyofutwa huku ikiacha maswali mengi kama hela ya umma aliyotia mfukoni sasa inakuaje! Kwa hali halisi na msingi wa haki UDA sio mali ya Simon Group na kampuni ya UDA-RT iliyoundwa kuendesha huduma ya usafiri kwenye DART sio halali.
Inafaa serikali kua makini na hawa matapeli kwani sio wawekezaji ila ni wababaishaji. Wawekezaji gani hawawezi hata kulipia ushuru wa forodha wa mabasi. .Watakwamisha mradi kwani ukweli hawana hela wala uzoefu na utaalam. Serikali itajikuta inawekeza fedha za umma kawanufaifa wezi wa mali ya umma.
Kinachostahili kufanyika na serikali kwa sasa ni kuanzisha kampuni yake kuendesha usafiri kwenye DART. Wataweza kubinafsisha kwa kuuza baadhi ya hisa baadaye kuliko kuwategemea hawa Simon Group wenye nia ya kupora mali za umma. Habari za kuaminika wameshauza kiujanja depot ya UDA kurasini yenye thamani kubwa kwa kupakana na bandari.