Uchaguzi 2020 Uchunguzi: Uchaguzi wa mwaka 2020 wagombea wa CCM watatumia rushwa kwa kiwango cha juu kuliko wakati wowote

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Katika uchunguzi huu inaonyesha wagombea wa CCM watatumia milungula, rushwa, ubabe na ulaghai ili wapate nafasi katika kugombea nafasi ndani ya CCM.

Viashiria vya rushwa katika chama hiki vimeanza kutapakaa katika maeneo mbalimbali ya nchi, wengine wakitumia mgongo wa shughuli za kijamii; wengine wakitumia nafasi ya uongozi walizonazo serikalini na wengine wakijificha huku wakitumia wafanyabiashara wa maeneo husika.

Baadhi ya wahamiaji (waliohama kutoka vyama vingine na kuhamia CCM) Wanasema "Ukiwa CCM kipindi kama hiki huwezi ukalala njaa maana pesa inatumika hasa kwa wasaka nafasi za kisiasa kwa kipindi hiki"

Baadhi ya wanaCCM wanahofia kwa kipindi hiki wagombea wakawa wa ovyo sana kuliko kipindi chochote maana dalili za kutumia rushwa mapema hivi ni kubwa sana.

Pia, wanahofia vijana walio na ndoto za kuwa viongozi katika chama hiki zikapotea kwa sababu ya rushwa maana vijana hawana uwezo wa kupambana na wazee katika kutoa rushwa, kwa hiyo tutakuwa na viongozi wabovu sana kutoka CCM.

WanaCCM wanahofia kutaibuka makundi makubwa ambayo yatawatafuna katika uchaguzi mkuu kwa sababu ya matumizi ya rushwa, hivyo kuwapa nafasi vyama vya upinzani kuchukua nafasi katika maeneo mbalimbali.

Mmoja wa wanaCCM mkoani Simiyu alikiri mchakato wa kuwapata wagombea CCM itakuwa kazi ngumu sana kwa sababu rushwa imeanza mapema, na unafikiri mtu ametumia mamilioni ya fedha akakosa nafasi unafikiri atamuunga mkono yule aliyeshinda, la hasha! lazima yeye na vibaraka wake watabadili msimamo na kuunga chama cha upinzani, hiyo ndo silika ya binadamu hakubali kirahisi kushindwa.

Anasema anahofia upinzani kuwa na nguvu baada ya kura za maoni CCM, wengine hawatakubali matokeo,wengine hawatakubali kukatwa na kamati kuu lazima upinzani upate nguvu tu"
 
cutelove,

Sasa rushwa imeanza kwa wagombea kugawa vifaa vya kujikinga na covid 19. Kwa mantiki hiyo Takukuru angalieni kwa umakini viongozi wanaogawa vifaa hivyo ndio rushwa mpya iliyoingia nchini.
 
Baada ya kura za maoni CCM, mtifuano utakuwa mkali sanna! Japo sioni sana rushwa lkn nategemea wizi mkubwa.
 
Back
Top Bottom