Uchungaji vs Ndoa!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Maisha yana vituko vyake na majamboz

Jambo lolote lile ukilichukulia kikasuku litakutokea puani,yaani unalichukua tu bila kulitafakari

Niliwahi kutoa kisa kimoja hapa cha Mchungaji mmoja kutomtimizia mkewe haki ya ndoa kwa ridhiko kwa sababu eti "kula sana" ni ulafi,nilidhani jambo lile ni dogo kwa kiasi hicholakini nimekutana tena na jambo hilo hilo tena

Hili la sasa ni kwa aina yake

Huyu Mchungaji yeye huwa anampa mkewe haki yake lakini ni mara chache sana

Iko hivi;Kwakuwa huyu mchungaji kanisa lake ni la "kiroho" huwa wana mifungo ya hapa na pale kwa wingi wa kutosha,yaani inawezekana kwa wiki wakafunga hata mara mbili au moja na kila mfungo huhusisha siku 2 hadi 3

Akiwa kwenye mfungo huwa kuna mambo huwa hafanyi na mojawapo ni hilo la kumpa mkewe haki ya ndoa hivyo kwa ratiba hiyo siku anazokuwa "free" ni ndogo sana kitendo ambacho klinamfanya mkewe kupata haki ya ndoa mara chache pia

Jambo hili Mama mchungaji limempa majaribu sana na imefikia kumuambia Dada mmoja ambae ni rafiki wa dada mmoja ambae tunafanya kazi eneo moja na yule dada kujaribu kuniuliza namna ambavyo anaweza kumshauri rafiki yake

Nilichomshauri nimesha mshauri,lakini nimeona kuna jambo la kujiuliza na hatimae kujifunza hapa

Najua umuhimu wa kufanya maombi haswa ya mfungo kwasababu najua faida zake,lakini ndoa nayo ina umuhimu wake mkubwa sana,sasa hii inakuwaje?Kipi kichukue nafasi ya kingine?

Sijui kama ukiwa mfungoni sio ruhusa ya kukutana kimwili na mkeo lakini najua pia kuwa "alone" hasa kwenye mfungo wa maombi kuna faida pia,sasa je si bora tu mtu ambae anajishughulisha na haya mambo ya kiroho kiasi hiki asioe tu?

Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa anaehudumu na kujihusisha na mambo ya kiroho kutokuwa na ndoa kabisa maana unaweza kumsababishia matatizo mwenzako

Au kama unaamua kuingia ndoani basi either upunguze kuwa na mifungo ya mara kwa mara au kubali "usumbufu" wa mwenzako wakati huu muhimu

Kama mtu anaona yote ni magumu huenda mambo ya kiroho yakawa magumu sana kuyachanganya na ndoa

Haya ndio masiha na changamoto zake

Wewe unaonaje?

Kipi ni kipi?

Mid week njema ........!!
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,491
2,000
Huyo mama mchungaji nae ana njaa kweli...sasa mtu yupo kwenye mfungo anapataje nguvu za kufanyia tendo la ndoa? Mimi naona hao watu wawe wanachunguzana interest zao ikibidi waulizane kabla ya kuingia kwenye ndoa ili asiwepo wa kukwazika na mwenendo wa mwenzake.....baba akiwa wa kufunga na mama nae awe hivyo hivyo ili waende sawa. Hapo kwenye kumridhisha mmmh....inawezekana mchungaji ana upungufu wa nguvu na hiyo ni defense mechanism
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,027
1,500
Tena mambo ya kiroho yakimwingia sana mtu, anakuwa hafiki. Haviki wapi vile? Wapendwa msiniue ila nilishawahi soma mahali sababu ya ile guilty konshazi kuwa 'ni dhambi'. Labda ikikomaa sana inaextend hata ndoani.
 
NGUVUMOJA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,350
1,195
Hili tatizo linaletwa na baadhi ya watu kuchukuwa mawazo ya hovyo ya binadam wenzao na kujifanya yanatoka kwa MWENYEZI MUNGU.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Huyo mama mchungaji nae ana njaa kweli...sasa mtu yupo kwenye mfungo anapataje nguvu za kufanyia tendo la ndoa? Mimi naona hao watu wawe wanachunguzana interest zao ikibidi waulizane kabla ya kuingia kwenye ndoa ili asiwepo wa kukwazika na mwenendo wa mwenzake.....baba akiwa wa kufunga na mama nae awe hivyo hivyo ili waende sawa. Hapo kwenye kumridhisha mmmh....inawezekana mchungaji ana upungufu wa nguvu na hiyo ni defense mechanism

Kutokuridhishwa kunatokana na mfungo wa mara kwa mara!
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Tena mambo ya kiroho yakimwingia sana mtu, anakuwa hafiki. Haviki wapi vile? Wapendwa msiniue ila nilishawahi soma mahali sababu ya ile guilty konshazi kuwa 'ni dhambi'. Labda ikikomaa sana inaextend hata ndoani.

Anakuwa hafiki kiaje?
 
ICHANA

JF-Expert Member
May 10, 2012
4,780
2,000
Ni kwel usemayo nini kisa cha mama mchungaji aliyechepuka kwa kuwa hapati huduma za tendo kutoka kwa mumewe

Mm naona kama mwanamke umeamua kuolewa na mchungaji uwe ushafanya maamuz sahih na kuwa mwaminifu kwa ndoa yako

Ni kweli tendo ni muhimu ila inabid aelewe mazingira ya kazi ya mumewe na pia wachungaji wajitahid kuoa wanawake wenye tabia kama zao ili kwenye mifungo wawepo wote.
 
Kweli .......!!
 
ICHANA

JF-Expert Member
May 10, 2012
4,780
2,000
Kweli .......!!

Yaaaa that's the true paroko

Kikubwa ni watu kuwa waaminifu kwenye ndoa zao na hii inatokana na kufanya good choice of hubby/wife tangia mwanzo wa mahusiano

Na tatizo sio uchungaji tuu Bali TABIA za mwanamke kutokuwa mvumilivu na kutofanya maamuz mazur before ndoa
Kuna mapadri hawaoi ili kufanya huduma ya kiroho ila wanachepuka hadi kuzaa wakati wameweka nadhiri za milele

Kuna wenye ndoa wanalala na kuamka na wake/ waume zao ila wanachepuka

Kuwa na mke / mume sio sababu kila mmoja anatakiwa kuwa mvumilivu kwenye ndoa yake kwa maana umetoa ahadi ya kuwa mwaminifu kwenye shida na raha.suala LA tabia ndo muhimu zaid
 
Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,561
1,500
Huyo mchungaji yuko kinyume, biblia inasema kwa habari ya kufunga na kuomba wanandoa wakubaliane na watengane kwa muda ili wasimpe shetani nafasi. Sasa hii habari ya kufunga X2 kwa wiki siku tatu tatu huwezi kuwa na performance nzuri kwenye tendo. Ikumbukwe mwanaume akifika nyumbani anavua koti la uchungaji anakuwa mme anakuwa baba.
 
Fixed Point

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
11,311
1,225
Ni kwel usemayo nini kisa cha mama mchungaji aliyechepuka kwa kuwa hapati huduma za tendo kutoka kwa mumewe

Mm naona kama mwanamke umeamua kuolewa na mchungaji uwe ushafanya maamuz sahih na kuwa mwaminifu kwa ndoa yako

Ni kweli tendo ni muhimu ila inabid aelewe mazingira ya kazi ya mumewe na pia wachungaji wajitahid kuoa wanawake wenye tabia kama zao ili kwenye mifungo wawepo wote.
mama Mchungaji si anatakiwa kuwa msaidizi wa mchungaji? anamsaidia nini?
nilidhani msaada anaohitaji sana ni kufunga na kuomba pamoja. sasa kama wote wanasaidia kwenye mifungo na maombi inakuwaje mwingine anakuna na uhitaji wakati mwingine hana?
Haya mambo haya.........:loco:
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Tatizo lako ni kuhoji hata kama umeelewa....
nasema hivi bora kupangiwa ratiba nje kuliko ndani ya ndoa labda mtu awe mgonjwa
kitanda, vyakula hata kwetu vipo over!!!
....jioni njema

Sio over .....

Hujui ni kwanini nauliza kuhusu "bora"

Ni bora kulinganisha na nini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom