Ndiyo sisi tuna migodi lakini tumewagawia wazungu. Wanatuachia 3% na mashimo. Tuna ardhi nzuri lakini pia tumeamua kuwakodishia wageni wajilimie na kupeleka chakula kwao. Wenzetu Carribea watoto karibu wote wanavaa viatu, sisi watoto wetu kwa idadi kubwa bado wanasoma kwenye mavumbi. We should be ashamed.
Kasi gani hiyo unayozungumzia? Tanzania ya Kikwete iko nyuma na pale alipotuacha Mkapa. Hospitali zetu hoi, shule zetu hoi, elimu hoi, wakulima hoi, vijana hawana kazi hata baada ya kumaliza vyuo vikuu. Tulikuwa na haraka gani ya kuchimba madini kama uwezo hatuna? Tungesubiri Watanzania waweze kuchimba. Mbona Uganda imeweza? It is a shame!Roma haikujengwa siku moja. Wewe unataka kesho ukiamka ukute kila Mtanzania ana maisha ya juu? Hiyo haiwezekani. Sisi tunaenda na kasi yetu lakini tunaenda. Na maendeleo yanaonekana. Kama wewe ungekuwa na uwezo wa kuchimba ungechimba uchukue hiyo 97%. Kama ulishindwa basi usilalamike wenzao wakifaidika. Si ndiyo uchumi wa kileo huo?
Kasi gani hiyo unayozungumzia? Tanzania ya Kikwete iko nyuma na pale alipotuacha Mkapa. Hospitali zetu hoi, shule zetu hoi, elimu hoi, wakulima hoi, vijana hawana kazi hata baada ya kumaliza vyuo vikuu. Tulikuwa na haraka gani ya kuchimba madini kama uwezo hatuna? Tungesubiri Watanzania waweze kuchimba. Mbona Uganda imeweza? It is a shame!
Kwa shule hizo, kazi utazopata ni za chini kidogo. Yaani hata dola 2000 kwa mwezi unaweza usipate. Upo? Labda urudi mwenyewe ufungue biashara yako kama mjasirimali.
lazima wataporomoka kiuchumi, ni kwasababu wameacha misingi ya waanzilishi wa taifa hili. walimtanguliza Mungu mbele, sasa wanakumbatia sera za,(kishetani shetani) kama ushoga,utoaji mimba, uonevu na ubababe kwa mataifa madogo ambazo ni chukizo kwa Mungu, hawana jinsi mungu ndo anawaadhibu hivyo
Kama vipi visivyotangazwa? Toa mfano.
Siku hizi American dream imegeuka kuwa American nightmare. Wana kazi kweli hawa Waamerika.
Uchumi wa Tanzania unaweza ukawa "unakuwa" kwa kasi kuliko wa America,lakini hiyo kasi kuwafikia kuwafikia America hata kama ingekuwa kasi ya mwanga kwa utaratibu wetu sisi bado sana...Uchumi haujengwi kwa porojo za simba na yanga.Uchumi wa bongo unakuwa kwa kasi kuliko wa America. Marekani iko hoi karibu wataanza kuomba misaada.