Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer

Wachina wanamdanganya Magufuri na ma project yao ya kujenga jenga hovyo ili kuliport ukuaji wa uchumi, yeye anadhani wanajenga Taifa letu,

hawa wachina haya mapesa wanakopeshwa na mabank yao serikali yao ikiwadhamini, mabank yao yanapotangaza ukuaji wa faida na kiwango cha mikopo yao, ndio unasikia wanatishia kuipiku Marekani kiuchumi.

Data hizo hizo, IMF na WB wanazitumia kusema na Tanzania uchumi unakua sababu ya investment kwenye properties na infrastructure.

Hakuna pesa inabaki hapa kuzunguka na kuboost uchumi,

Yeye anafurahia kuona miundo mbinu na ma growth rates

vyote uongo uongo tu
 
Uzuri kila mtu atakula kibano kwa wakati wake.Paskali,Hili mimi niliona wakati mzee wangu Magufuli alipoanza kugusa kila mahali,kila sekta,kila idara.Alipoanza kusimamia kwa nguvu kubwa sheria ambazo zilitungwa kwa ajili ya kusimamiwa taratibu.Alipoanza kuwabania wafanyakazi wapiga dili wakati walikuwa hawalipwi mshahara wa kutosha kuishi.Alipoanza kuwasumbua wahindi kama manji wakati walikuwa wanamiliki zaidi ya nusu ya uchumi ghafi.Alipoanza kutamani matajiri waishi kama mashetani na kusahau kwamba hawamashetani ndo wanafanya wananchi wengi wanaishi angalau kama watu,so wakiwa mashitani ina maana wananchi wanakuwa majini.

Ninachokiona hapa ni serikali kuanzakushindwa kujiendesha kutokana na kushuka kwa mapato ya kodi ambayo itapelekea hata hivi vimishahara vidogo vinaolipwa serikalini visiwepo.Baada ya hapo atashindwa kuwalipa wanajeshi watanza kufanyia raia uharamia,Wanajeshi wakimaliza kufanyia raia uharamia wataona hapana ngoja tumfate huko huko.

Itakapofika hatua hio wale jamaa wanaokaa na kombati pale feri kutishia wananchi wasishangae tausi wa ikulu watageuka na kuingia ndani kukinukisha.ikifika hatua hiyo basi KIAMA CHA TANZANIA KITAKUWA KIMEFIKA NA MASIHI ATAKUJA KUWACHUKUA WATEULE WAKE
 
Wanabodi
Kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania ya Magufuli, ambayo umekuwa ukikua kwa asilimia zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, sasa kasi hiyo imeanza kuporomoka ambapo sekta binafsi ndio mhanga mkuu kwa Ku suffer.

Ku suffer huko kulianzia kufungwa kwa maduka makubwa ya bidhaa na supermarkets.

Yakafuata baadhi ya mashirika na makampuni kufilisika hivyo kupunguza wafanyakazi, sasa kibano hicho kimeigusa sekta ya Media ambapo media kubwa kabisa nchini zimeanza kutikisika.

Kwenye media ilianza Star TV, kati ya wafanyakazi 400, ililazimika kupunguza wafanyakazi 200!.

Leo kumepatikana taarifa ya wafanyakazi wa gazeti kubwa la the Guardian, hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, hivyo kitakachofuata ni kupunguza wafanyakazi.

Japo familia ya the Citizen Mwananchi, hawajaniingizia kibano, lakini kama hii ndio hali halisi ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, then hata Citizens, litakuwa halina jinsi, lazima nalo soon litatangaza kupunguza wafanyakazi.

Mimi mwenyewe, Kampuni yangu ya PPR, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu Kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu tumehama, tumehamia jengo la Posta House!.

Wito kwa waandishi wenzangu, kwa hali hii ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, usisubiri kupunguzwa kazi, bali sasa kwa sisi wanaume tufuge kuku (kazi ya kujiajiri) na njiwa (kazi ya kuajiriwa), ili njiwa akiruka, ubaki na kuku.

Kwa waandishi wa kike, kwenye kazi ya kuteka maji, teka maji kwenye ndoo (kazi ya kudumu) na kudumu (kujiajiri), ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, ubaki na kidumu.

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Magufuli aweze.
Jumatano Njema.
Paskali
Hahaaa!!nacheka km mazuriii
 
Nadhani umeongelea kwa kifupi sana. Wafanyabiashara tuna hali ngumu sana wenye mitaji mikubwa wamekwisha hamia Rwanda,Kenya ,Zambia na South Africa. Tunasubiri kuzikwa tu kwa sasa sijui kwa sekta zingine hali ipoje
 
Mim
Rais akishindwa ni jukumu la wananchi wa nchi ile kumuondoa madarakani kwa lazima. Magufuli alishashindwa kitambooo..Mimi nilimuona ni Rais wa ajabu sana mwanzoni tu mwa mwaka 2016 na nikamchukulia kama nyoka anayeninyemelea. Niliamua na sasa nimesepa. Huyo mtu siyo kabisa....Sijui kwanini haelewi? Mtu huwezi kuongoza nchi lakini bado king'ang'anizi. Ondoka! Mimi ni mmoja wa wanaoamini kuwa muuaji wa Tanzania kwa sasa ni Rais John Pombe Magufuli.
I niko tayar mkuu kuingia bara barani
 
Back
Top Bottom