Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer

Paskali kalisema sana The Economist ambao wanalaumu Siasa kuingilia mambo ya Uchumi. Lakini katika rejea yake kuhusu mdororo wa uchumi unaotukodorea mimacho kalitaja likielezea suala hili. Ukweli utabaki kuwa kweli hata kama utatafuta njia ya kuupindisha.
 
Kampuni ya New Habari imetangaza kusitisha utoaji wa magazeti yake kuanzia Jumatatu ijayo kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

========

NEW HABARI YASITISHA UZALISHAJI MAGAZETI

KAMPUNI ya New Habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji wa magazeti yote kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo.
Duh...!. Could it be
Or sababu hizi

P
 
Wanabodi

Kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania ya Magufuli, ambayo umekuwa ukikua kwa asilimia zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ukuaji huu is not reflected kwa Watanzania wa hali ya chini ambao ndio walio wengi, tunaelezwa uchumi unakuwa, na ripoti ya juzi juzi ya UNDP inaeleza kiwango cha umasikini kinapungua Ripoti: Kiwango cha umasikini kinapungua kwa kasi - JamiiForums lakini hali za maisha kwa walio wengi, zinazidi kuwa ngumu siku hadi siku, uchumi wa taifa unakuwa, huku uchumi wa watu individual na sekta binafsi ukizidi kuporomoka ambapo sekta binafsi ambayo ndio inategemewa kuwa the drivers we uchumi wa nchi ikiwemo Tanzania ya viwanda, ndio mhanga mkuu wa mdororo wa uchumi na ndiye anaye suffer the most.

Kwa upande wa maendeleo, ni kweli nchi yetu inapiga hatua kubwa za maendeleo, majengo, miundombinu, mabarabara, flyovers, viwanda, midege mikubwa, SGR, Stigler Gorge etc, lakini haya yote ni maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu.

Je, Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?-
Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?. - JamiiForums


Japo Beggars Can Not Be Choosers, Tuache Siasa Kwenye Uchumi. We Have to Choose Or. .. - JamiiForums

Tena msije kusema kuwa tulinyamaza, Sisi jf tumesema sana, tumeuliza sana humu

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT - JamiiForums

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi? - JamiiForums

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Kwa sasa naona kama sisi sekta binafsi tuna suffer. Ku suffer huko kulianzia kufungwa kwa maduka makubwa ya bidhaa na supermarkets. Zilianza super markets za Shoprite, zikaja Uchumi, piteni maeneo ya Shoppers Plaza mshuhudie frames tupu wenyewe wamefungasha. Hata mtaa wa Samora lile jengo jipya la NHC mtaa wa Samora, lilikuwa full, sasa kuna mapengo.
Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago! - JamiiForums

Yakafuata baadhi ya mashirika na makampuni kufilisika hivyo kupunguza wafanyakazi,Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Yakaja mabenki, kabla ya Magufuli, ukiingia benki kubwa zote, NMB, CRDB na NBC, unakutana foleni ndefu za wateja. Sasa kuna branches unaingia unakwenda straight to counter, anangoja wateja, IMF: Nearly half of Tanzania's banks vulnerable to financial shocks - JamiiForums

na sasa ni maduka ya fedha.

Wakati yote haya yakitokea, sisi media hatukuyaangazia vya kutosha kwa kudhani hayatuhusu!.

Sasa kibano hicho cha hali ngumu ya uchumi, kimeigusa sekta ya Media ambapo media kubwa kabisa nchini zimeanza kutikisika.

Kwenye media ilianza Star TV, kati ya wafanyakazi 500, ililazimika kupunguza wafanyakazi 100, mwaka 2016 wakabaki 400, mwaka jana wakapunguza 200 wakabaki 200, sijui mwaka huu, lakini kipindi chake most popular cha Jicho letu ndani ya habari, kinachoendeshwa na Mkongwe Dotto Bulendu, hakipo hewani!
Star Tv na Redio Free kupunguza wafanyakazi - JamiiForums

Hapa ninapo zungumza, najua kituo cha Television cha Channel Ten kinapumulia mashine. Kusipofanyika juhudi za ziada kukinusuru, Channel Ten itafuata mkondo wa Radio Uhuru na magazeti ya Chama ya Uhuru Mzalendo.

Leo kumepatikana taarifa ya wafanyakazi wa gazeti kubwa la the Guardian, hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, hivyo kitakachofuata ni kupunguza wafanyakazi.Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited - JamiiForums

Japo familia ya the Citizen Mwananchi, bado hawajatangaza kulia njaa, lakini kama hii ndio hali halisi ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, then hata Citizens, litakuwa halina jinsi, lazima nalo soon litatangaza kupunguza wafanyakazi.

Mimi mwenyewe na kale kajikampuni kangu ka PPR, ambapo tulibamba sana tenda za serikali, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, serikali inatangaza moja kwa moja na TBC, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu hapakaliki hivyo tumehama, tumehamia jengo la Posta House kwenye kajichumba.

Wito kwa waandishi wenzangu, walioajiriwa kwenye media industry, kwa hali hii ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, usitegemee ajira pekee na usisubiri kupunguzwa kazi, bali sasa kwa sisi wanaume tufuge kuku na njiwa, na Kwa waandishi wa kike ni mambo ya ndoo na kidumu.

Kwa sisi wanaume, kuku ni kazi ya kujiajiri) na njiwa (kazi ya kuajiriwa), ili njiwa akiruka, ubaki na kuku.

Kwa waandishi wa kike, kwenye kazi ya kuteka maji, teka maji kwenye ndoo (kazi ya kudumu) na kidumu (kujiajiri), ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, angalau unabaki na kidumu.

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki rais Magufuli aweze kufanikiwa kukuza uchumi wa nchi yetu na kuifanya, Tanzania ya Viwanda kufanikiwa, Tanzania ya uchumi wa gesi, Tanzania ya uchumi wa kati, tukielekea kuwa nchi ya ahadi kwa mabomba nchi mzima yatatoa maziwa na asali
Jumatano Njema.
Paskali
Mitano tena
Na bado Mayala ataitwa njaa
Wakati Bereu de change zetu zinavamiwa na TRA na JWTZ kutunyang'anya hela zetu kwa nguvu mlichekelea
Dhulma haina tija.. Watu wangapi wanalia na kusaga meno kwa uonevu wa Magufuli?
Ndugu tusitegemee maajabu maana imeandikwa '' muovu akitawala watu huumia ''
Aidha muovu awe mwema au tuendelee kuumia
 

mtanzanianews

NEW HABARI YASITISHA UZALISHAJI MAGAZETI
-
KAMPUNI ya New Habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji wa magazeti yote kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo.
P
Bora Mugalifu wao hana hayo mambo.
Mugafilu anazingatia haki za binadamu
Anazingatia utawala bora
Anazingatia utawala wa sheria
Hana upendeleo
Anazingatia usawa kwa kila mwananchi
Anazingatia ulaji sawa wa keki ya taifa.
Anawapenda sana wapinzani wake ikiwemo Tundu Lissu na Chadema kwa ujumla.
Anapenda sana kukubali kukosolewa
Ni msikivu wa kiwango cha rami.
Anazingatia misingi ya ukuzaji uchumi
Anazitumia vizuri pesa mabeberu(wanaume wachapakazi wa Uraya)
Anahakikisha afya za wananchi zinastawi
Ana ruhusu upatikana wa habari hata zile zinazomkosoa.
Anazingatia uwepo wa usalama wa kila mwananchi hata uwe wa Chadema.
Amekuwa kiongozi wa mfano ulimwenguni hata serikali za peponi zinajitahidi kumuiga yeye.
Anazingatia kutokuwepo kwa wasaliti duniani kwa kuwapa ulinzi(Tundu Lissu amiminiwa marisasi huko Dodoma)
Mambo ni mengi muda mchache

Kidumu chama chetu chakavu cha mapinduzi kisichojali tena matatizo ya wananchi.

Kigumu chama kinacho impoverish watanzania kwa speed ya mwanga.
 
Wanabodi

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki rais Magufuli aweze kufanikiwa kukuza uchumi wa nchi yetu na kuifanya, Tanzania ya Viwanda kufanikiwa, Tanzania ya uchumi wa gesi, Tanzania ya uchumi wa kati, tukielekea kuwa nchi ya ahadi kwa mabomba nchi mzima yatatoa maziwa na asali
Jumatano Njema.
Paskali
Media chini ya JPM tuli suffer, tulibanwa mbavu, jee sasa chini ya Samia, media tuna afadhali?, tuna pumua?.

MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Media chini ya JPM tuli suffer, jee sasa chini ya Samia, media tuna afadhali
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
Uhuru wetu umerudi sasa tunapumuwa.

Yule Ibilisi alikuwa anaipeleka hii nchi kuzimu, Asante Mungu.🙏🙏
 
Back
Top Bottom