Uchumi wa ‘Machinga’ na Mama Lishe: Muhimili Usioonekana wa Maendeleo ya Tanzania

Uchumi wa ‘Machinga’ na Mama Lishe: Muhimili Usioonekana wa Maendeleo ya Tanzania

Fascinating

Member
Joined
May 14, 2025
Posts
93
Reaction score
224
Unapokatiza mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, Mwanjelwa jijini Mbeya, au soko la Nyakato jijini Mwanza, zile sauti za wafanyabiashara wadogo na harufu ya vyakula vya mama lishe zinazotawalaga kwa mbali, unaweza kudhani ni shughuli za kawaida za kujitafutia riziki, lakini ripoti mpya kutoka taasisi ya TICGL inabainisha ukweli mpya wa kushtua: Huku ndiko kuliko moyo wa uchumi wa Tanzania.

Sekta isiyo rasmi (Informal Economy) si tena suala la "kimbilio la waliokosa ujuzi au nafasi" kama tulivyozoea; ni injini inayofanya nchi isiteseke na mawimbi ya ukosefu wa ajira na mdororo wa kifedha.


Kwa ujumla muonekano wa Sekta hii upoje?
Jibu lake ni raisi tu, "sekta hii ni zaidi ya Vijibiashara vya Mtaani". Ripoti ya TICGL inaweka wazi kuwa shughuri za kiuchumi zisizo rasmi zinachangia kati ya 31% hadi 52% ya Pato la Taifa (GDP) ukitoa shughuri za kilimo. Tukizungumzia Pato la Taifa kwa ujumla kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi purchasing power perity(PPP), sekta hii inabeba takriban 44.9%.


Hii inamaanisha kuwa karibia nusu ya mzunguko wa fedha nchini unatokana na watu ambao wanajishughurisha na ajira zisizo ramsi. Ukiacha hilo, sekta hii inaajiri kati ya 60% hadi 75% ya nguvukazi watu nje ya shughuri za kilimo. Jambo linalo staajabisha zaidi ni kuwa wanawake ndio wanaoendesha gurudumu la sekta hii, wakijumuisha 60% ya shughuri zote zisizo ramsi, Ingawa ni dalili nzuri kuonesha kujumusishwa kwa wanawake katika shughuri za uchumi lakini bado kunazua maswali juu wingi huu unaweza kuashiria kundi hilo linakosa ujuzi na taalamu zinazohitajika kwenye sekta rasmi.

Hii sekta ni "Shock Absorber": Kinga Dhidi ya Bomu la Ajira
Ripoti ya TCIGL inaonesha kuwa kila mwaka, takriban vijana 900,000 wanaingia katika soko la ajira nchini Tanzania. Hata hivyo, sekta rasmi (serikalini na makampuni makubwa) ina uwezo wa kuzalisha ajira chini ya 100,000. Swali ni: Je, wale wengine 800,000 huenda wapi?

Hapa pia jibu raisi tu, kundi hili lote linaenda kumezwa na sekta isiyo rasmi.
Sekta isiyo rasmi ndio unaingilia kati kutatua janga la ukosefu wa ajira, suala ambalo si hatari tu kiuchumi bari hata kiusalama. Sekta hii inachukia mara 8.5 zaidi ya sekta rasmi kila mwaka. Bila sekta hii, Tanzania ingekuwa inakabiliwa na janga kubwa la kijamii kutokana na ukosefu wa ajira. Kitu ambacho kingeweza kuchuchea matukio ya uvunjifu amani au uhalifu

Vikwazo Vinavyozuia Mageuzi
Licha ya umuhimu wake katika kuhakikisha hali ya jamii inakuwa shwari, ni 10% tu ya biashara ndogo ndogo na za kati (MSMEs) zinazofanikiwa kuvuka daraja na kuwa biashara rasmi.

Ripoti ya TICGL inataja changamoto kuu sita:
  • Urasimu na Sheria: Kati ya 80% na 90% ya wajasiriamali wanakwama kwenye milolongo mirefu ya kiusajili na kikanuni.
  • Ukata wa Mitaji: Asilimia 94% ya biashara hizi hazina nufaiki na mikopo ya kibenki. Wengi wanategemea akiba binafsi au mikopo ya "vikoba" na familia. Japo serikali imetangaza nia ya kuwawezesha vijana waweze kukopesheka lakini jitihada hizo zinaweza zisifikie malengo kama kutakosekana mkakati utakao wezeshe biashara hizi kuweza kufikia vigezo vya kukopesheka bila ya masharti magumu ikiwemo mali zisizo hamishika, kitu ambacho wamiliki wengi wa biashar hizi wanakosa
  • Miundombinu: Kati ya 67% hadi 80% ya wafanyabiashara wanalalamikia masoko duni, ukosefu wa nishati ya uhakika, na barabara mbovu.
  • Teknolojia Duni: Zaidi ya nusu ya wafanyabiashara hawa wanatumia mbinu za kizamani zinazopunguza ufanisi ni ushindani sokoni.
  • Kodi na Sera zisizotabirika: Hofu ya kodi kubwa za ghafla na wakati mwingine rushwa inawafanya wengi waone ni heri kubaki "majaribuni" kuliko kujitokeza rasmi.
Mapinduzi ya Fedha Kidigitali (Mobile Money)
Mwaka 2025, miamala ya fedha kwa njia ya simu ilifikia rekodi ya TZS 223.4 trilioni (takriban 95% ya pato la taifa GDP). Licha mchngo huo, ipoti ya TICGL inaonya kuwa ni asilimia 5% hadi 7% tu ya fedha hizi ndizo zinazoweza kufuatiliwa kwenye mifumo ya kikodi au kutumika kama dhamana ya mikopo. Hii inaonyesha kuwa kuna sehemu kubwa ya fedha inayozunguka mitaani ambayo bado haijanufaisha mfumo rasmi wa kifedha wa nchi.

Kimkakati, kuelekea 2025–2030 imekaaje?
Tanzania inatarajiwa kukua kwa asilimia 5.5–6.0% katika miaka ya 2025-2026, kasi kubwa kuliko wastani wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (4%). Lakini ili ukuaji huu uwe na tija kwa mwananchi wa kawaida, TICGL imeashauri yafuatayo:
  • Kubadili Mtazamo: Wawekezaji na Serikali wasiione sekta isiyo rasmi kama "kero" au "uchafu wa mjini," bali kama mshirika muhimu wa biashara na soko kubwa.
  • Urahisishaji wa Kodi: Badala ya kutoza kodi kubwa za awali, kuwepo na mfumo rahisi wa usajili (Single Window) na msamaha wa kodi kwa biashara changa ili kuzivuta rasmi.
  • Haki za kumiliki Ardhi: Kuimarisha milki za ardhi kutawezesha wafanyabiashara wadogo kutumia rasilimali hizo kama dhamana ya kupata mitaji mikubwa.
Sekta isiyo rasmi nchini Tanzania si sekta ya yanakotupwa masalia ya watu waliokosa ujuzi au nafasi ya katika sekta rasmi; ni mfumo thabiti uliojengeka kutokana na uhalisia wa kijamii. Ikiwa mageuzi sahihi yatafanyika kati ya mwaka 2025 na 2030, sekta hii ina uwezo wa kukua kwa asilimia 5–7% zaidi, jambo ambalo litaongeza mapato ya kodi, kupunguza umaskini, na kuleta usawa wa kiuchumi.

Safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati na juu haitapita kwenye viyoyozi wala maghorofa marefu pekee, bali itategemea sana jinsi itakavyowatengenezea mazingira wezeshi wale wanaopambana juani kila siku.



Chanzo: TICGL - Tanzania’s Informal Economy
 
Katika changamoto kuu nashangaa hakuna changamoto ya ukosefu wa maeneo rasmi ya kufanyia biashara. Asilimia kubwa hawana maeneo rasmi la kufanyia biashara, zoezi la kuondoa machinga likianza huwa ni shida sana.
 
Katika changamoto kuu nashangaa hakuna changamoto ya ukosefu wa maeneo rasmi ya kufanyia biashara. Asilimia kubwa hawana maeneo rasmi la kufanyia biashara, zoezi la kuondoa machinga likianza huwa ni shida sana.
Yapo ila hawaendi, hayakuwekwa kwa misingi ya human centered development design
 
Back
Top Bottom