Uchumi wa China ni wa kidunia zaidi, vita kubwa haiwezi kuwa chaguo sahihi kwao kamwe

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,694
46,401
Tazama listi ya nchi ambazo ni wananunuzi wakubwa wa bidhaa za China na kiasi walichonunua kutoka China mwaka jana.

1. USA - $531 billions
2. Hong Kong- $313 billions
3. Japan- $151 billions
4. Korea Kusini- $135 billions
5. Vietnam- $125billions
6. Ujerumani-$103 billions
7. Netherlands- $92billions
8. India- $88billions
9. Uingereza- $79billions
10.Taiwan- $71 billions

China Uchumi wao umeunganika mno na uchumi wa dunia. Mizozo,vurugu au vita yoyote kubwa na mojawapo ya haya mataifa itakuwa na athari mbaya sana.

Katika washirika wake wakubwa wa kibiashara ni India na Vietnam ambazo zingeweza kusimama naye lakini nazo zina matatizo na pride zao za muda mrefu dhidi ya China jambo ambalo linaifanya China kukosa mshirika mkubwa wa Uhakika katika mgogoro wowote na USA au West.

China imetanguliza busara na maslahi ya uchumi wake mbele zaidi kuliko sifa za kijinga katika mgogoro wake na Taiwan, China ni wazuri sana katika jambo hili.
 
... ifike mahali uhuru wa Taiwan utambulike rasmi na wapate seat UN badala ya vitisho vya kila mara toka kwa watawala katili wa China wasiojua maana ya neno demokrasia wala haki za binadamu. Hope suala hili litapewa msukumo mpya.
 
Ni Jambo ambalo haliwezekani . Ni bora ufute Hilo wazo kichwani mwako.
 
Kwani China[ PRC ] ili sema inahitaji mshirika yoyote wa kuwa saidia kwenye hii ishu ya Taiwan Unification?🤔
 
Ni Jambo ambalo haliwezekani . Ni bora ufute Hilo wazo kichwani mwako.
Tuseme tu Haliwezekani kiwepesi sio haliwezekani sababu Hii mipaka imewekwa na watu, watu hao hao wanaweza kuamua vinginevyo. Huenda miaka mingi mbele kukawa na serikali moja dunia nzima. Huenda.
 
Tuseme tu Haliwezekani kiwepesi sio haliwezekani sababu Hii mipaka imewekwa na watu, watu hao hao wanaweza kuamua vinginevyo. Huenda miaka mingi mbele kukawa na serikali moja dunia nzima. Huenda.
Sawa wacha tuupe muda nafasi.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Maana yake tunahitaji maelfu ya miaka tena?
Sio lazima maelfu mkuu. Pamoja na kuwa tunarithi tamaduni ila kila kizazi huwa kinakuwa na vipaumbele na mtindo tofauti wa utawala. Angalia vijana enzi za nyerere na vijana enzi za samia wanavyouchukulia muungano.

Miaka 20/50 ijayo masalia ya kina nyerere na walioshuhudia utawala wake hayatakuwepo kabisa, hapo sasa unakuta kiu ya kushikilia muungano inaweza ongezeka au ikapungua au muungano ukawa wa mtindo tofauti na wa sasa.
 
Sio lazima maelfu mkuu. Pamoja na kuwa tunarithi tamaduni ila kila kizazi huwa kinakuwa na vipaumbele na mtindo tofauti wa utawala. Angalia vijana enzi za nyerere na vijana enzi za samia wanavyouchukulia muungano. Miaka 20/50 ijayo masalia ya kina nyerere na walioshuhudia utawala wake hayatakuwepo kabisa, hapo sasa unakuta kiu ya kushikilia muungano inaweza ongezeka au ikapungua au muungano ukawa wa mtindo tofauti na wa sasa.
... you've nailed it! Mao akifufuka leo hataamini atakachokiona kulinganisha na China aliyoiacha! Leo hii China ina-compete na mabeberu kwa mabilionea? Haiwezi kumwingia akilini asilani ila ndio hivyo - wakati ukuta.
 
Kabisa mkuu. Ujamaa wanautelekeza kadri muda unavyoenda.
 
Back
Top Bottom