Uchumi hauwezi kukua bila wawekezaji-JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi hauwezi kukua bila wawekezaji-JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 23, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Friday, 18 September 2009
  Na Mercy James
  Majira

  RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza juhudi za pamoja za serikali yake kuvutia wawekezaji na kubainisha kuwa hakuna uchumi wa nchi yoyote duniani unaoweza kukua kwa uwekezaji wa serikali peke yake bila wawekezaji binafsi.

  Aliyasema hayo jana Ikulu Dar es Salaam alipokutana na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, Taasisi muhimu zinazohusu uwekezaji, wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Phillemon Luhanjo, katika mkutano wa kutathimini hali na kasi ya uwekezaji katika uchumi wa Tanzania.

  Aliwataka maofisa wa Serikali yake kuchukua maamuzi ya haraka kutimiza mahitaji ya wawekezaji mara zinapojitokeza nafasi za wawekezaji kutaka kuja nchini.

  "Uchumi huu wa kwetu hautakua bila wawekezaji, nchi yetu haiwezi kuendeshwa na uchumi wa serikali na hakuna uchumi wa nchi yoyote unaeza kukua kwa kutegemea uwekezaji wa umma pasipo kushirikisha wawekezaji binafsi,"alisema.

  Aliwataka maofisa waandamizi wa serikali pamoja na taasisi za serikali kuchukua hatua za makusudi kuwezesha na siyo kuzuia uwekezaji katika uchumi wa nchi.

  "Lazima tuwe na haraka katika kuvuta wawekezaji badala ya kuwa wazuiaji wa uwekezaji katika nchi yetu, nchi yetu inayo bahati kubwa ya Kijiografia na lazima tutumie fursa hiyo kuvuta watu kuja na kuwekeza katika uchumi wetu,"alisema .

  Mkutano huo ulihudhuriwa makatibu wakuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Sheria na Katiba, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Biashara, Viwanda, Masoko, Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na Wizara ya Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana.

  Taasisi zilizowakilishwa ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
   
  Last edited: Sep 25, 2009
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Kamwe uchumi wa Tanzania hauwezi kukua kwa kuwakaribisha wawekezaji matapeli ambao hawana aibu yoyote ya kusaini mikataba ya kuchukua 97% ya mapato na kuiachia Tanzania 3, akina BARRICK na wajomba zake. Uchumi wa Tanzania hautakuwa kwa kuwa na wawekezaji kama TICTS, RITES, DAR CITY WATER, SASKATEL na wengineo ambao wameonyesha hawana uwezo wowote katika sekta walizowekeza bali ni wezi tu ambao wanataka kutumia kuwepo kwao nchini kuwaibia Watanzania .
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wala sio wezi, hii ndo business. Sidhani hata wewe kama ungekuwa una uwezo ungekuwa mwekezaji wa ndani and you will play to maximize our profit.

  Nasikitika kuwa JK anafikiri wanataka kuondoka au hawaji kwa kuwa kuna urasimu.

  Je ukienda kuwekeza kwao je? Does Jakaya mean what he talking?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu Jamaa ana degree ya uchumi kutoka UDSM!
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Hebu niambie ni nchi gani nyingine duniani ambayo inawakaribisha "wawekezaji" (mimi hawa walioingia kwetu huwaita wachukuaji maana Tannzani hatunufaiki na chochote kwa kuwa nao) katika nchi yao na kuwaruhusu kuchukua 97% ya mapato ili kuvuna rasilimali zao iwe ni madini, mafuta n.k., hawalipi kodi na kuwaachia wenyeji wao 3% tu!?
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Only in Tanzania!
   
 7. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BAK,

  Our legal, policy and instutional frameworks zipo, ni weak enough na hazina wataalam wenye ujuzi, yaani they are too ACADEMICIANS kuliko field experiencer.

  Based on that watu walioko huko they are too selfish. kuanzia family, udugu, ukoo, ukabila na kimaeneo. They are not thinking of national interests or their kids. They just think of their stomachs. Bado wanaamini tanzania ya leo ni sawa na ya kesho.

  Kukua kwa uchumi sio kukusanya kodi tu ambazo ends upto RA na dugu zake.

  Ngoja niwape fumbo, ajuaye ajaze....

  Mgodi wa Resolute Nzega ni wa muongo sasa. Swali mbalo nilipenda kumuuliza JK japo sijui kama litajibiwa ni kuna tathimini yeyote ya mdogi huu ambao ulitakiwa kufungwa 2008 na kukua kwake? anaweza kutupa takwimu ili huu mradi uwe ni model?
  cheki hapa;
  - Wafanyakazi wa kizalendo wanapelekwa kazini na kampuni ya GPH. Huyu mmiliki wa hii kampuni si Mweusi ni mzungu. Uraia wake mwenye nao aseme. Uchumi unakuwa au unahamishwa?
  - Wanakula kwa kulishwa na Mansons; sina data zake mwenye nazo aseme. Kule tulawaka tulikuwa na kampuni moja nao nimeisahau jina but nilikaa muda mfupi tu.
  - Msafirishaji wa mizigo kutoka nje ya nchi ni FFT na kwa ndani ni Karama wa Mwz. Je, hawa ni watanzania?
  -Drillling contractors in Major, Stanley/Layne ni watz?
  -Mining contrators ni Caspian, angalau una uraia wa Tz. Where the money go?
  -Who is feeding mining industries? Allied Mining? Who owns alllied minings? you?
  -Halmashauri zinalipwa $250k per annual, wanazipeleka wapi? Nilikuwa pale Ushirombo na maeneo ya jirani. I have got some pics hapa. People can not even differentiate from having investors against wachimbaji wadogo.
  -Ni nani anaeenda kufanya hata extension services kuchange peoples mind? kuwa ili uwe na indirect benefits from investors do this and that?

  Nitaandika mengi buree, kumbe KILIMO KWANZA while GOLD IS GOING?

  Welcome investors, Welcome DR. SLAA in power 2010.
   
 8. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BAK,

  Nina kupata ila huenda approach zetu zinatofautiana. Maana Mkuu wa kaya hajui anachokiongea BUT naungana nae kuwa tusiwe kikwazo kwa wawekezaji.

  Kuna nchi nyingine hazipati hata hio 3%.

  Learn this. nilishawahi kuongea na Environmental Manager mmoja wa Barrick akaniambiwa kuwa anakuwaga na budget ya let say $500K out of this $300K zinakwenda nje SA au australia, UK or CA kwaajili ya consultation. Kuna vitu can be made locally but who knows? ila ni kwa wachache tu kwa kuwa wanajua mipango but kuna mfumo ambao unampa majority hizi opportunities?

  Ukiwa nao pamoja na mtaji make connection na wazito you will make but still quality is poor.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Wakati bei ya Dhahabu katika soko la dunia ikiendelea kupaa na kuwanufaisha Barrick na Shareholders wao, Tanzania bado tunaambulia 3% ile ile ambayo tulisaini nao mkataba tangu mwaka 2000 mkataba ambao hadi hii leo ni siri kwa wenye mali (Watanzania)…Kweli Tanzania itatafunwa na wenye meno!

  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~

  Gold nearing 18-month highs, now is the time to invest in bullion: analysts

  Published: Thursday, September 10, 2009 | 2:55 PM ET


  TORONTO - With the price of gold again approaching lofty peak it hit last March, analysts say now is a good time to invest in the yellow metal, particularly if you have a long-term investment horizon.
  "Gold is not only an investment but it's a store of value, it's a financial hedge," said John Ing, a gold analyst and CEO of Toronto-based investment dealer Maison Placements.

  The short-term outlook on gold remains "mildly risky," but if you're a longer-term investor and are willing to part with your cash for a few years, then gold is one of the safest bets out there, said Jeffrey Nichols, managing director of American Precious Metals Advisors.

  "I think (the price of gold) is going to have some difficulty getting through the US$1,000 area in the near term," Nichols said.

  "But with prices around $1,000 an ounce, I think if you look back two years from now you will think that was an attractive price. I see it going easily to $2,000 or maybe even $3,000 an ounce before we're through."

  With U.S. dollars flying off the printing presses to cover the government's massive economic stimulus package, concerns about inflation are growing and investors are increasingly turning towards gold as a safe-haven investment to protect against currency fluctuations.

  On Tuesday, the price of bullion rose above US$1,000 to its highest point since March 17, 2008, when it hit a record of $1,033.90. Since then, it has been hovering around the $1,000 mark.

  Gold is typically bought as an alternative to the U.S. dollar among safe-haven assets favoured by investors seeking to preserve capital. So its rise often correlates to a drop in the value of the American currency.

  The fact that 20 of the world's rich and developing countries promised over the weekend to keep in place their stimulus measures - which include both spending as well as low interest rates - reinforced the appeal of gold.
  "All is not right with the mightiest nation in the world, and when that happens, the dog wags the tail, and maybe alternatives are what people should be looking at," Ing said.

  Every investor should have some money in physical gold, whether it's in the form of bars or coins, Ing said. These can be bought directly through your bank's bullion desk.

  However, buying physical gold can be complicated, Nichols said.
  Instead, Nichols recommends putting money in gold exchange-traded funds, or ETFs, which invest in physical gold but trade like equities on stock exchanges.

  Nichols said these have soared in popularity in the last two or three years, and ETFs now hold around 54 million ounces of gold, making them "a rival of major central banks as a major holder."

  "Gold ETFs have made it very easy for investors around the world to buy gold and have increased the access to investors who might not have bought physical gold for one reason or another in the past," Nichols said.

  "It's as easy as buying any other equity, so for the investor it's simply a phone call to his stock broker. He doesn't have to open up some new-fangled account, he doesn't have to worry about where he's going to store the gold and take delivery of the gold and all that stuff."

  Nichols said ETFs also allow investors to sell their gold investments quickly and easily without having to worry about the large commissions it's common to pay when buying or selling gold coins, for example.
  However, he cautioned that this could also allow for substantial profit-taking by gold investors down the road - a liability to which gold has historically been immune.
  If you're feeling particularly bullish about the price of gold, Ing said you should consider investing in gold equities as well as physical gold.
  "Stocks give an investor much more leverage to the price of gold, particularly when there's a rising price of gold. You get generally four times the leverage with gold stocks," he said.

  Ing said Canadian gold miners, which include major players like Barrick Gold Corp. (TSX:ABX) and Goldcorp Inc. (TSX:G), make good investments, as they tend to be particularly well situated with quality assets.
  "The fact is there have been no real big gold finds since Bre-X and that was a fake, so there's less gold coming onto the market from the gold miners as the mines get deeper and more expensive," he said.
  The world's biggest gold miner announced this week that it's betting the price of gold will continue to rise. Barrick said it plans it raise up to US$4 billion through a massive share offering in order to eliminate its gold hedges.
  Barrick decided to eliminate its hedges because of an increasingly positive outlook on the gold price. The company also said it believes the gold hedges hurt its appeal to the broader investment community and the company's share price.


   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  mkuu, unatakiwa ukumbuke kuwa waliosaini hiyo mikataba wananufaika na mikataba yenyewe. Kama ingekuwa hawanufaiki hakunba ambaye angesaini. It is only now that the nation has come to light that catutally this 97 percent inagawiwa kwa hao walioshiriki kusaini mikata hiyo. Ndio maana ukitaka kuvunja mikata hiyo leo, wakawanza watakao kupinga ni watanzania wenyewe na sio wawekezaji wenyewe.
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa uelewa wangu, JK anataka kuweka vivutio kwa wawekezaji wa ndani na nje. Hakuna mahali ambapo taarifa imeeleza kuwa wanaotakiwa ni wawekezaji wa nje tu.

  Ukweli unabaki kuwa, hakuna nchi duniani ina/itakayopata maendeleo ya kweli bila uwekezaji na hasa katika viwanda.

  Kinachotakiwa kwa serikali ni kuhakikisha kuwa nchi iko tayari ku-support uwekezaji huo kwa vitendo. Vile vile, serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa wawekezaji pamoja na Taifa wananufaika na uwekezaji huo.

  Uwekezaji wa ndani ndio uwekezaji wa maana kuliko ule unatoka nje, ambao mara nyingi unatushinda katika ku-negotiate terms.
   
 12. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mimi mbona siwaelewi hawa viongozi wa Tanzania, ni nani aliyewaroga?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Mkuu Recta hebu soma hiyo para hapo juu.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuwa lazima uwekezaji katika viwanda ukue ndipo na uchumi nao unaweza kuwa na la maana kwa watu especially agro processing industries. Lakini naona tatizo kubwa lipo kama tunafikiri ni wawekezaji wa nje tu ndo wanakaoweza kuinua uchumi. Kufanya biashara kama mtanzania mazingira bado ni magumu sana ukilinganisha na wawekezaji wa nje ambao huchukua karibu faida yote na kuipeleka nje.
  Hivi hatuwezi kuwa na wawekezaji wa ndani wanaofanya vizuri mpaka tuwapate toka nje? Kama kazi ya urais ingekuwa ni kuzunguka dunia yote kuwaomba wawekezaji waje TZ basi ni kazi rahisi sana.
  Hivi kama wakiamua kuja kwa maelfu umeme uko wapi? barabara na airport ziko wapi maana nchi yetu ni kubwa , huduma bora za afya na mawasiliano je? We should keep our house in good order before rushing into calling people to come and invest
   
 15. K

  Koba JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  JK inabidi awasaidie wawekezaji wa ndani kwa serikali yake kujenga policy nzuri za kuwasaidia kupata mikopo na usalama wa biashara zao,pigana na rushwa na wape unafuu wa kodi kama hao wa nje wanaowapa tax holiday ,na serikali lazima imwage pesa nyingi sana kwenye umeme,barabara na Elimu maana hivyo ndio kama engine ya maendeleo...bila kuwapatia mikopo na kuondoa rushwa/urasimu wawekezaji wa ndani itakuwa ngumu sana kufanikiwa so na Taifa kwa ujumla!
   
 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ama kweli hizo degree za uchumi za mlimani inabidi zifanyiwe uchunguzi. Nina wasiwasi labda degree yake ni kati ya zile za political economy za miaka ile ...... ile ya wana TANU.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mhhhhh yawezekana!
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe mwenyewe si unaona maamuzi yake ya kiuchumi kuanzia apate kula. Kwanza anaulizwa swali kuwa kwa nini nchi ni masikini anakosa jibu - wale wataalamu wa political economy huwa wanavuka hili swali.

  Pili - anatumbua pesa zote kwenye akiba ya nje

  Tatu - anatumia mabilioni kusafiri nje ya nchi ili kupata mamilioni (wawekezaji).

  Nne - anatoa trilioni moja ili kufanya stimulation ya kilimo (hata cuba wasingefanya hivi).

  Tano ---- dont get me started , Nisijetoa speech ndefu kama Gadafi bure
   
 19. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa penye nyekundu ndo ameniacha hoi kabisa. Yaani kutimiza mahitaji ya wawekezaji na siyo watanzania? Mahitaji ya wawekazi siku zote ni KUPATA FAIDA KUBWA. Ana maana wapewe wanachohitaji? Hiyo haraka gani aliyonayo

  Hivi hajui kuna marais kibao nyuma yake na vizazi kibao wanategemea rasilimali hizi hizi? Zingeanza kuchukuliwa enzi za nyerere angeendeshaje nchi na anategemea hao wanokuja nyuma yake wataendeshaje nchi kama amemaliza rasilimali zote leo? Akumbuke tuna pewa misaada kwa sababu wawekezaji kutoka huko wanakuja kuchuma rasilimali zetu.

  Hakuna rasilimali hakuna muwekezaji hao marais na vizazi vyetu watapata wapi wawekezaji?

  Technololojia yetu haikui kwanza inadidimia cheki enzi hizo za UFI. Leo hata kiberiti inatoka kenya. Nafikiri usalama wa taifa na jeshi wawe wanaangalia maamuzi kama haya. Tanzania itabaki hata baada ya Kikwete na mimi kuondoka. Technolojia pamoja na elimu hatuna tukikosa na ardhi itakuwaje?

  Wauze hayo madini, wanyama, gesi, mafuta pesa zinazopatikana serikali itumie kwa wananchi kuwekeza kwenye kilimo. Sisi tuwalishe hao waarabu, wazungu na waasia kwa sasa hatuwezi kuzalisha bidhaa za viwandani tukasafrisha Ulaya na Asia, kwaiyo jukumu letu lingekuwa ni kuwalisha sasa kama na hili wanakuja kufanya wenyewe, what role then Africans will play in world economy?

  Haiwezekani, uwekezaji wa kwenye ardhi ufikiriwe tena na tena.
   
 20. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa somo la uchumi na siasa ni kwamba kila mtu ana PhD.
   
Loading...