Uchumi hauwezi kukua bila wawekezaji-JK

Swali bado linabakia vile vile kuwa bila wawekezaji kutoka nje(kama JK anavyoamini) tunaweza kweli kuendelea? Tutaweza vipi? isije kuwa tunajaribu kukataa kitu ambacho kina ushahidi waukweli wake.

Mwanakijiji,
Naona hii ndiyo mindset na imani ya Kikwete. Umemsikia UN akiwaomba marafiki zetu watusaidie kuunda ajira ya vijana wetu. Hata ajira sasa ni jukumu la wafadhili.
 
Mwanakijiji,
Naona hii ndiyo mindset na imani ya Kikwete. Umemsikia UN akiwaomba marafiki zetu watusaidie kuunda ajira ya vijana wetu. Hata ajira sasa ni jukumu la wafadhili.

sijasoma bado hotuba yake; lakini siwezi kushangaa. Sijui kwanini asiombe wafadhali waendeshe ikulu?
 
Kwa uelewa wangu, JK anataka kuweka vivutio kwa wawekezaji wa ndani na nje. Hakuna mahali ambapo taarifa imeeleza kuwa wanaotakiwa ni wawekezaji wa nje tu.

Ukweli unabaki kuwa, hakuna nchi duniani ina/itakayopata maendeleo ya kweli bila uwekezaji na hasa katika viwanda.

Kinachotakiwa kwa serikali ni kuhakikisha kuwa nchi iko tayari ku-support uwekezaji huo kwa vitendo. Vile vile, serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa wawekezaji pamoja na Taifa wananufaika na uwekezaji huo.

Uwekezaji wa ndani ndio uwekezaji wa maana kuliko ule unatoka nje, ambao mara nyingi unatushinda katika ku-negotiate terms.
Recta,
Mkuu ebu isome tena hotuba hiyo vizuri maanake inachosha kuzungumzia sana na maelezo mengi marefu ktk kitu ambacho kipo wazi kabisa..hivi kweli ktk fikra zako unafikiri JK anakuzungumzia mwekezaji mwananchi!...hivi kweli utawezaje kumvuta AJE kuwekeza ikiwa mwekezaji huyo yupo ndani!..anatokea wapi?..

Ebu nambie Jk anaposema:- Aliwataka maofisa waandamizi wa serikali pamoja na taasisi za serikali kuchukua hatua za makusudi kuwezesha na siyo kuzuia uwekezaji katika uchumi wa nchi.
"Lazima tuwe na haraka katika kuvuta wawekezaji badala ya kuwa wazuiaji wa uwekezaji katika nchi yetu, nchi yetu inayo bahati kubwa ya Kijiografia na lazima tutumie fursa hiyo kuvuta watu kuja na kuwekeza katika uchumi wetu,"alisema
 
UWEKEZAJI WA WACHINA -WAISHIO TANZANIA BILA VIBALI.
KAMA SIO WIZI NI NINI?
JK TAFADHALI SHUGHULIKIAA SUALA LA WAHAMIHAJI HARAMU WAPO WENGI SANA TANZANIA WENGI TOKA KENYA,DRC,UGANDA- AJIRA ULIZOAHIDI ZITAPATIKANA KWELI.KWANI WANAODHI HATA KADA ZA CHINI KABISA.

MDAU ,
Lusungo Ipinda Kyela.
 
Back
Top Bottom